Nipe Andiko
Senior Member
- Jan 20, 2017
- 133
- 133
Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza sana tume ya vyuo vikuu nchini (TCU), kwa huu mfumo mpya wa kuchagua vyuo waliouanzisha, ambapo mwanafunzi anatuma maombi moja kwa moja kwenye chuo anachokipenda, (utaratibu ambao ndio ulikuwa ukitumika mwanzoni kabla ya kuanzishwa kwa mfumo wa udahili wa pamoja/CAS-Central Admission System)
Huu ndio mfumo bora zaidi kuliko ule wa CAS, ambao umefutwa! Kwa sasa mtu una uhakika wa kwenda chuo ulichochagua, sio kama zamani ambapo kupata chuo ilikuwa bahati nasibu, mwisho wengi walijikuta wanapangiwa na TCU vyuo na kozi ambazo haikuwa malengo yao, hasa ulipokuwa unakosa chuo kwenye ile round ya kwanza, basi ujue round ya pili utapangiwa popote ambapo hukutegemea!
Lakini sasa hivi, unachagua programmes kuanzia 3 na kuendelea kwenye vyuo hata vitano au zaidi, ni wewe tu utakavyojisikia, kati ya hizo programmes sio rahisi kukosa, maana ukikosa moja utachaguliwa nyingine, watu walikuwa wanaponda utaratibu huu mpya, lakini kumbe huu utaratibu ndio bora zaidi na unampa mwanafunzi uhakika wa kuchaguliwa kwenye chuo alichoapply.
Kilichowafanya wengi wauponde huu utaratibu mpya ni bei uliyoanza nayo, wakati ambapo kila chuo kilikuwa kinajipangia bei yake, kabla TCU hawajaweka bei elekezi, lakini hivi sasa gharama zimepungua, bei imeshushwa vyuo vingi kuapply chuo haizidi 10,000/=
Hivyo (binafsi) nina kila sababu ya kuusifia utaratibu huu mpya, sioni sababu ya kuuponda huu utaratibu, ukizingatia mpaka sasa sijaona mapungufu au changamoto zozote ndani yake. Nawasilisha!