Hongera TCU Kwa Utaratibu Mpya Wa Kuapply Vyuo Mlioanzisha:

Nipe Andiko

Senior Member
Jan 20, 2017
150
250
Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza sana tume ya vyuo vikuu nchini (TCU), kwa huu mfumo mpya wa kuchagua vyuo waliouanzisha, ambapo mwanafunzi anatuma maombi moja kwa moja kwenye chuo anachokipenda, (utaratibu ambao ndio ulikuwa ukitumika mwanzoni kabla ya kuanzishwa kwa mfumo wa udahili wa pamoja/CAS-Central Admission System)

Huu ndio mfumo bora zaidi kuliko ule wa CAS, ambao umefutwa! Kwa sasa mtu una uhakika wa kwenda chuo ulichochagua, sio kama zamani ambapo kupata chuo ilikuwa bahati nasibu, mwisho wengi walijikuta wanapangiwa na TCU vyuo na kozi ambazo haikuwa malengo yao, hasa ulipokuwa unakosa chuo kwenye ile round ya kwanza, basi ujue round ya pili utapangiwa popote ambapo hukutegemea!

Lakini sasa hivi, unachagua programmes kuanzia 3 na kuendelea kwenye vyuo hata vitano au zaidi, ni wewe tu utakavyojisikia, kati ya hizo programmes sio rahisi kukosa, maana ukikosa moja utachaguliwa nyingine, watu walikuwa wanaponda utaratibu huu mpya, lakini kumbe huu utaratibu ndio bora zaidi na unampa mwanafunzi uhakika wa kuchaguliwa kwenye chuo alichoapply.

Kilichowafanya wengi wauponde huu utaratibu mpya ni bei uliyoanza nayo, wakati ambapo kila chuo kilikuwa kinajipangia bei yake, kabla TCU hawajaweka bei elekezi, lakini hivi sasa gharama zimepungua, bei imeshushwa vyuo vingi kuapply chuo haizidi 10,000/=

Hivyo (binafsi) nina kila sababu ya kuusifia utaratibu huu mpya, sioni sababu ya kuuponda huu utaratibu, ukizingatia mpaka sasa sijaona mapungufu au changamoto zozote ndani yake. Nawasilisha!
 
Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
6,916
2,000
Maoni yangu ya awali. Kwa kuanzia kuna swali kama 10000 ni gharama halisi au ni za kisiasa. Kwa hizi 10000 chuo kitapokea maombi, admission officers watapanga maombi ya kila program na kuchuja wasio na vigezo, orodha itapelekwa idara/kitivo/college inayohusika ili kamati ichague wa kudahili, orodha zitarudishwa kamati ya senate na mwisho seneti kupitishwa. Baada ya hapo orodha za waliochaguliwa au kuachwa zitapelekwa TCU nao watapitia kila moja na kuhakiki. Orodha iliyohakikiwa ndo itarudishwa vyuoni na kila chuo baada ya kuipitia itatangaza. Wakati ho huo TCU itaviarifu vyuo nani kahaguliwa zaidi ya chuo kimoja (hapa hata sijaelewa kama muombaji atajulikana anakwenda chuo gani kabla ya kufunguliwa). Sasa fikiria processs yote hiyo -je ni kweli 10000 ni gharama halisi? Bila kujali kama hiyo kumi ni ya kiasa au vipi-itasaidia kuwezesha wengi kuomba vyuo vya kutosha kulinganisha na gharama zilizotangazwa awali. Elfu kumi sio bei elekezi bali ni government fixed price. Pili kuna vyuo havija jipanga vinatumia technology ya zamani ambayo ina usumbufu (download form jaza halafu peleka maombi chuoni). Hopefully mwakani watajipanga vizuri. Hizo OAS zinapishana-kuna ambazo hawakutoa maelezo ya kutosha, na nyingine kwa sababu ndo mara ya kwanza kutumika zimezingua sana. Option za malipo nyingine sio rafiki sana kama zile zinazokuhitaji kwenda bank hopefully with time zitaboreshwa. Changamoto kubwa ni kama kila muombaji ambae ana minimum entry qualifications atapata chuo na jinsi ya kuminimise nafasi kubaki wazi (inaelekea tutakuwa na round moja tu). Huduma za simu na e-mail nyingi hazifanyi kazi ukiwa unataka taarifa muhimu, unashangaa kama vyuo vina admission officers wakutoa hii huduma (nimeandika e-mail mbili kwa zaidi ya siku 5 hakuna jibu, nimepiga simu si chini ya mara 10-ni moja tu niliyompata mhusika nyingine zinaita tu kwenda mbele).
 
ivan don

JF-Expert Member
May 26, 2017
337
500
Kama we hufanyi maombi msimu huu basi una kila sababu ya kutokujua yanayoendelea

1.tangu TCU utangaze bei mpya vyuo vinavyofata hilo tamko havifiki ata 4 Tanzania nzima

2 kabisa unasema hujaona upungufu wala changamoto basi ata hizi threads humu kutwa watu kulalamika mara Sua hivi, mara UDSM vile, mara UDOM kalikwenda, mara ARDHI kakarudi kwahiyo we huzioni na kama unaziona basi tu umeamua kama wale wanaotaka kuanzisha campaign ya kumbakiza mkulu

Huu mfumo kila mtu atakubali kuwa ni mzuri sana kwa mwanafunzi kama tu ungeenda sawa na matarajio ya wanafunzi na TCU pia ila tukubali tu kuwa hatukujiandaa, umefeli kwa sababu ya kukurupuka, vyuo havikujiandaa vizuri kwenye system zao za udahili, ulipaji wa fees ya application na mengine mengi na mwisho wake imegeuka kuwa kero

Wangepewa muda wa kujiandaa vizuri may be hadi mwakani mambo yangekuwa safi ila kwa sasa kuna uwezekanao wa wanafunzj wengi kutokwenda chuo kwa ajili ya huu mfumo, kuna uwezekanao hadi deadline itafika kutakuwa na wanafunzi wanaohangaika namna ya kuapply

Mwisho, huu mfumo hadi hapa tulipofkia kwa yoyote yule ambae amefanya maombi atakubaliana na mimi kuwa una hasara nyingi kuliko faida,..! ila kama ilivo binadamu hatuwezi tukawa sawa kwenye mtazamo hivo naheshimu mawazo yako pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ivan don

JF-Expert Member
May 26, 2017
337
500
Maoni yangu ya awali. Kwa kuanzia kuna swali kama 10000 ni gharama halisi au ni za kisiasa. Kwa hizi 10000 chuo kitapokea maombi, admission officers watapanga maombi ya kila program na kuchuja wasio na vigezo, orodha itapelekwa idara/kitivo/college inayohusika ili kamati ichague wa kudahili, orodha zitarudishwa kamati ya senate na mwisho seneti kupitishwa. Baada ya hapo orodha za waliochaguliwa au kuachwa zitapelekwa TCU nao watapitia kila moja na kuhakiki. Orodha iliyohakikiwa ndo itarudishwa vyuoni na kila chuo baada ya kuipitia itatangaza. Wakati ho huo TCU itaviarifu vyuo nani kahaguliwa zaidi ya chuo kimoja (hapa hata sijaelewa kama muombaji atajulikana anakwenda chuo gani kabla ya kufunguliwa). Sasa fikiria processs yote hiyo -je ni kweli 10000 ni gharama halisi? Bila kujali kama hiyo kumi ni ya kiasa au vipi-itasaidia kuwezesha wengi kuomba vyuo vya kutosha kulinganisha na gharama zilizotangazwa awali. Elfu kumi sio bei elekezi bali ni government fixed price. Pili kuna vyuo havija jipanga vinatumia technology ya zamani ambayo ina usumbufu (download form jaza halafu peleka maombi chuoni). Hopefully mwakani watajipanga vizuri. Hizo OAS zinapishana-kuna ambazo hawakutoa maelezo ya kutosha, na nyingine kwa sababu ndo mara ya kwanza kutumika zimezingua sana. Option za malipo nyingine sio rafiki sana kama zile zinazokuhitaji kwenda bank hopefully with time zitaboreshwa. Changamoto kubwa ni kama kila muombaji ambae ana minimum entry qualifications atapata chuo na jinsi ya kuminimise nafasi kubaki wazi (inaelekea tutakuwa na round moja tu). Huduma za simu na e-mail nyingi hazifanyi kazi ukiwa unataka taarifa muhimu, unashangaa kama vyuo vina admission officers wakutoa hii huduma (nimeandika e-mail mbili kwa zaidi ya siku 5 hakuna jibu, nimepiga simu si chini ya mara 10-ni moja tu niliyompata mhusika nyingine zinaita tu kwenda mbele).
Uko sawa mkuu, huyu nina wasiwasi hafanyi application huu mwaka, na kama anafanya basi ndio wale wenzangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
massaiboi

JF-Expert Member
Jan 4, 2016
993
1,000
Vp ukichaguliwa course zote ulizoapply huoni kama ni kunyima wengine nafasi. Siijui vizuri lkn inabd mwisho wacoordinate admission ya vyuo vyote ili kuondoa wale waliokubaliwa kwny course zaidi ya moja
 
Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
6,916
2,000
Vp ukichaguliwa course zote ulizoapply huoni kama ni kunyima wengine nafasi. Siijui vizuri lkn inabd mwisho wacoordinate admission ya vyuo vyote ili kuondoa wale waliokubaliwa kwny course zaidi ya moja
Nimemsikia mkurugenzi wa udahili TCU akiliongelea hili kwa mintarafu ya mkopo kwamba chaguzi zikitoka wenye multiple selections watapewa siku 3 kuamua wanataka waende wapi ili waweze kufikiriwa mkopo. Mimi sijaona TCU itawasaidia itawasaidia vipi waliokosa bafasi kutokana na nafasi zilizowekwa kujaa. Tuombe vijana wapate machaguo yao raundi hii ya kwanza na ya mwisho.
 
mkulungu mkuyengo

JF-Expert Member
Feb 5, 2015
778
1,000
Maoni yangu ya awali. Kwa kuanzia kuna swali kama 10000 ni gharama halisi au ni za kisiasa. Kwa hizi 10000 chuo kitapokea maombi, admission officers watapanga maombi ya kila program na kuchuja wasio na vigezo, orodha itapelekwa idara/kitivo/college inayohusika ili kamati ichague wa kudahili, orodha zitarudishwa kamati ya senate na mwisho seneti kupitishwa. Baada ya hapo orodha za waliochaguliwa au kuachwa zitapelekwa TCU nao watapitia kila moja na kuhakiki. Orodha iliyohakikiwa ndo itarudishwa vyuoni na kila chuo baada ya kuipitia itatangaza. Wakati ho huo TCU itaviarifu vyuo nani kahaguliwa zaidi ya chuo kimoja (hapa hata sijaelewa kama muombaji atajulikana anakwenda chuo gani kabla ya kufunguliwa). Sasa fikiria processs yote hiyo -je ni kweli 10000 ni gharama halisi? Bila kujali kama hiyo kumi ni ya kiasa au vipi-itasaidia kuwezesha wengi kuomba vyuo vya kutosha kulinganisha na gharama zilizotangazwa awali. Elfu kumi sio bei elekezi bali ni government fixed price. Pili kuna vyuo havija jipanga vinatumia technology ya zamani ambayo ina usumbufu (download form jaza halafu peleka maombi chuoni). Hopefully mwakani watajipanga vizuri. Hizo OAS zinapishana-kuna ambazo hawakutoa maelezo ya kutosha, na nyingine kwa sababu ndo mara ya kwanza kutumika zimezingua sana. Option za malipo nyingine sio rafiki sana kama zile zinazokuhitaji kwenda bank hopefully with time zitaboreshwa. Changamoto kubwa ni kama kila muombaji ambae ana minimum entry qualifications atapata chuo na jinsi ya kuminimise nafasi kubaki wazi (inaelekea tutakuwa na round moja tu). Huduma za simu na e-mail nyingi hazifanyi kazi ukiwa unataka taarifa muhimu, unashangaa kama vyuo vina admission officers wakutoa hii huduma (nimeandika e-mail mbili kwa zaidi ya siku 5 hakuna jibu, nimepiga simu si chini ya mara 10-ni moja tu niliyompata mhusika nyingine zinaita tu kwenda mbele).
maelezo meeengi lakini hogwash!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom