Hongera tanzania daima!

WILLY GAMBA

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
211
87
Wengi wetu tunaridhika na habari mnazo tupasha na pia mikakati yenu ya kufanya magogoni wakasikika. Mbinu na mikakati yenu ya kujifanya mnakosea spelling haina mbadala, ina wapumbaza timu ya magogoni na kuwafanya kuropoka...next time napendekeza heading iwe MKUWU WA MAGWOGONI ndio RICHMONDOL tuone watakavyofyatuka..
 
Tanzania Daima siku hizi naona wanaandika kama Mwanahalisi. Wanajilipua sana kama habari ya leo ya mkuu wa nchi kuongoza dunia nzima kwa safari!
 
gazeti la udaku linapigiwa chapuo? likiendelea umaarufu wake utakwisha labda tu kama linawalenga na kusomwa na chadema na wafuasi wake tu.
 
Tanzania Daima siku hizi naona wanaandika kama Mwanahalisi. Wanajilipua sana kama habari ya leo ya mkuu wa nchi kuongoza dunia nzima kwa safari!

uko nchi gani mwanahalisi na tanzania daima yote ni ya chadema. mwenye hisa nyingi mwanahalisi ni anthony komu yule mkurugenzi wa fedha na utawala wa chadema unategemea nini kwao?
 
uko nchi gani mwanahalisi na tanzania daima yote ni ya chadema. mwenye hisa nyingi mwanahalisi ni anthony komu yule mkurugenzi wa fedha na utawala wa chadema unategemea nini kwao?

Kimantiki, sioni kama ni tatizo. So far yanaandika habari za kweli na zenye maslahi kwa wananchi, sioni mantiki ya kuhoji wamiliki wake.
Mbona hata TBC1 kuna wakati watu wanalalamika kuwa wanachakachua habari zao. So, tuseme wao wanamilikiwa nanai?

Hata hii jamii forum kuna wakati watu fulani fulani wanalalamika kuwa ina upendeleo, ingawa bado wanaendelea kuitumia. Tuache mitazamo isiyo na tija kwa watu. Mbona hatuhoji huduma zingine zinazotolewa na makada wa vyama hivi, kwa mfano, vyombo vya usafiri, tv stations na radio, sehemu za biashara nk. Tunatumia kila siku tena sana tu, iweje kujadili haya magazeti wamiliki wake. Kama huridhiki na habari wanazotoa, acha kuyasoma. Nadhani yanakukuna ndio maana unayanunua na kusoma huo upuzi unaoona. Siku zote, mti wenye matunda ndio utupiwao mawe. Tuache unafiki.Ufike wakati watu tuonekane kutumia akili za utu mzima kufikiri, ala?!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom