Hongera TANESCO kwa mabadiliko

Mahesabu

JF-Expert Member
Jan 27, 2008
5,972
3,830
Nitoe pongezi zangu kwa shirika la umeme Tanzania (Tanesco).

Pongezi hizi nazitoa kwa mabadiliko niliyoyaona ndani ya siku chache toka leo. Sifa na pongezi zinatokana na juhudi za kitengo cha mawasiliano ya umma (mahusiano) ambapo hapa JamiiForums "KOLEBA", na hata baada ya kupiga simu kueleza matatizo ya umeme yamepokelewa kwa njia chanya (positive way) na kutatuliwa haraka na kwa ufanisi PASIPO KUTENGENEZEWA MAZINGIRA YA KUTOA RUSHWA ili kufidia huduma tajwa ama kukosa huduma kama hukutoa.


MAONI:

1. Anzisheni ama boresheni mahusiano/mawasiliano kwa njia ya mitandao kwa kuwa na USERNAME yenye jina na nembo ya Tanesco na ikitatua matatizo mbalimbali kwa wakati.

2. Elimu kwa jamii na kusogeza ukaribu kati ya mteja na shirika

3. Yote yaambatane na kulipa bili zetu ili tushirikiane kwa pamoja

Hakika nimeamini "M4C" ni MAGUFULI FOR CHANGE
..
 
Mimi kinanikela sana Tanesco ni service charges kwani kubwa mno. Nina miaka kama minne bado wanakata tu
 
Hakuna cha pongezi wala nini wametuanzishia mgao tangu siku ile ya uteuzi wa mawaziri huku kwetu ni kukatwa tu umeme daily
 
Too early to congratulate Tanesco. Bado wananchi/watumiaji wengi wa umeme wana malalamiko mingi isiyofanyiwa kazi.
Labda ungesema 'UNAWASHUKURU' the way they handled your case.
Una uhakika wa umeme kesho asb? Bado sana. Mbado.
 
hawa jamaa wa Tanesco wana hasira za kupindukia hapa Dodoma
leo wametangaza kwa yeyote aliyefungiwa Mita ,pua ua LIKU akabakiwa na deni mwisho ni baada ya masaa 24
wakati tulikubaliana kulipa kwa awamu maana wengine tumeyakuta madeni kwenye nyumba za umma zaidi ya 100,000/-
wangefanya maelewano madeni yangekatwa kila ufanyapo kununua umeme hakuna atakayebisha
sijui ni kitengo cha wasoma Mita kukosa ulaji ndio wanakuja na hasira za mwisho?
 
Hakuna kitu, labda wewe ni mfanyakazi /Mdau wao thats why unatoa Pongezi
 
Nitoe pongezi zangu kwa shirika la umeme Tanzania (Tanesco).

Pongezi hizi nazitoa kwa mabadiliko niliyoyaona ndani ya siku chache toka leo. Sifa na pongezi zinatokana na juhudi za kitengo cha mawasiliano ya umma (mahusiano) ambapo hapa JamiiForums "KOBELA", na hata baada ya kupiga simu kueleza matatizo ya umeme yamepokelewa kwa njia chanya (positive way) na kutatuliwa haraka na kwa ufanisi PASIPO KUTENGENEZEWA MAZINGIRA YA KUTOA RUSHWA ili kufidia huduma tajwa ama kukosa huduma kama hukutoa.


MAONI:

1. Anzisheni ama boresheni mahusiano/mawasiliano kwa njia ya mitandao kwa kuwa na USERNAME yenye jina na nembo ya Tanesco na ikitatua matatizo mbalimbali kwa wakati.

2. Elimu kwa jamii na kusogeza ukaribu kati ya mteja na shirika

3. Yote yaambatane na kulipa bili zetu ili tushirikiane kwa pamoja

Hakika nimeamini "M4C" ni MAGUFULI FOR CHANGE
..

Asante sana Mkuu, ntayafikisha sehemu usika. Swala la user name tutalifanyia kazi.

Pia tuna account za Facebook (www.facebook.com/yanescoyetu), Twitter account (www.twitter.com/tanescoyetu), tunablog pia umemeforum.blogspot.com

Pote huko tunapokea maoni, ushauri wa namna ya kuboresha huduma, matatizo mbalimbali kutoka kwa wateja.

Shirika linajitahidi kuboresha huduma, pia mawasiliano ya mameneja wa Kila kanda yatatolewa

Pia ni KOLEBA kaka asante
 
Too early to congratulate Tanesco. Bado wananchi/watumiaji wengi wa umeme wana malalamiko mingi isiyofanyiwa kazi.
Labda ungesema 'UNAWASHUKURU' the way they handled your case.
Una uhakika wa umeme kesho asb? Bado sana. Mbado.

Mkuu unatatizo gani ambalo hujatatuliwa? Naomba tuwasiliane ni pm namba yako
 
Hakuna kitu, labda wewe ni mfanyakazi /Mdau wao thats why unatoa Pongezi

Jamani watanzania bwana..kumpa mtu pongezi ni shida a mmezoea kulalamika ki ukweli hata mm naipongeza sana Tanesco kwani kuna mabadiliko tusiwe na khiyana ya kutoa sifa panapostahili
 
Binafsi napenda kusema ukweli kwamba kwa mtu asiyejua nini kinafanyika pale TANESCO anaweza akaongea maneno mabaya apendavyo, ila laiti angejua ninkiasi gani watu wanajitahidi kuhakikisha umeme unapatikana ikiwa ni pamoja na kufanya kazi usiku kucha ili tu umeme uwake wasingebaki kulaumu tu wangepongeza pia kama alivyofanya mtoa post
 
Kwa nini hawajanifungia umeme hadi leo wakati nililipa mamilioni ya hela?
 
Kwa nini hawajanifungia umeme hadi leo wakati nililipa mamilioni ya hela?

Mkuu naomba unipm contact zako tuweze kufuatilia.

1)Umelipia lini umeme Mkuu?
2) Uliambiwa zinahitajika nguzo? Kama ndio zimahitajika nguzo ngapi ulizo ambiwa?
 
Siku zote ninekuwa nikiwasifu Tanesco lakini kwa hili la uduma kwa wateja nawasifu zaidi. Kwani hata Mimi nilikatiwa Umeme WK iliyopita nikapiga huduma kwa wateja Kimara nilipikewa pia vizuri na isitoshe walichukua namba yangu kujua kama tatizo langu limetatuliwa na baada ya muda mafundi walifika wakatengeza. Haikuishia hapo nilipigiwa Simu kutoka ofisoni kutaka kufamu kama tatizo limetatuliwa na kwa muda gani. Kwakweli kwa hili hongela Tanesco
 
Ningependa kujua nafasi yako katika TANESCO. Hata Mimi nna tatizo la muda siku nyingi siku nyingi , sijui nipeleke wapi malalamiko yangu.
Ukweli TANESCO hawayaishi walioainisha kwenye customer charter Yao. Especially muda wa kusubiri kuunganishwa na huduma baada ya malipo. Ni muda gani exactly utasubiri upate huduma?
 
Bili ya umeme ya hapa nyumbani (wapangaji) imeshuka ghafla, kutoka 120,000 hadi 75,000. Hongereni kwenu,
 
Wewe hayo unaona ni mabadiliko? Kweli tunatofautiana ... Wakinipa sababu ya msingi kwa nini juzi & jana hakukuwa na umeme mtaani kwangu nitawaelewa, otherwise sitaki hata kuwasikia.

Mvua ikikosekana, utaambiwa mabwawa hayana maji na umeme unakatwa; Mvua ikinyesha, utaambiwa miundombinu imeharibika na umeme unakatwa. Hii tabia ni kila mwaka ... Pumbavu zenu.
 
Back
Top Bottom