hongera STAMINA kwa hii...

hongera STAMINA kwa hii...

zubedayo_mchuzi

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2011
Posts
4,873
Reaction score
1,220
Kwenye Nyimbo yako ya kabwela ulio mshirika Rich Mavoko...kuna misemo ifuatayo...

>Nimepigwa msumari wa
kichwa mwili unangoja
kaburi maisha yamenipiga picha nega zimetoka vivuli
dunia tambala bovu nalidekia kwa shida
jitahidi kui'solve bila
kutumia four figure
natamani nisimame ili
nione magharibi
moyo umejaa ukame kuhema unajitahidi
macho yote yana ukungu
utadhani chungu cha bibi
nataka, kumuomba mungu
shetani ananzidi spidi men
vizuri viko wapi navisaka havionekani dah
napata makapi vinono
navitamani sina baba, sina mama, sina babu sina bibi uchumi wangu umesimama kama behewa la itigi
umaskini unanipodoa, bila
kutumia cosmetics
daily unanizodoa,
unanivuta bila magnetics maisha yangu hayana
swagga kama mmasai wa
Njiro,
Natamani kula burger
naishia viazi vya Gairo dah

leo nimepata kesho nimekosa nnachohifadhi maumivu tu life ni ngumu bado inanichosha nakula mbichi sili mbivu boo huwezi amini bado kabwela sina uhuru kama niko jela,
huwezi amini bado kabwela sina uhuru kama niko jela,

sikusoma, kitajiri kichwa
kimejaa madufu
maisha hayana tafsiri
usidhani yanamjua lufufu
naichora, lami na mkaa
kwa kudhani nitaona chochote
atleast, basi ningekaa
nisingeitwa kiokote
pesa imegeuka yuda, daily
inanisaliti
mishale inazidi muda, utajiri unaninyima seat
maisha kama gwaride,
kuna wa mwisho na wa
kwanza
ikisikika nyuma geuka, wa
mwisho anakuwa wa kwanza
taifa la kichwa changu
Raisi wake naona kichaa
na kitabu, cha dhambi
zangu kwa Mungu
kimeshajaa ah, napatwa wazimu shida zinanitia madoa,
pesa imekuwa adimu
kama bikra kwa changudoa,
banda nnalofugiwa sihemi halina dirisha,
wasichana wananikimbia
wananiita nyoka wa
kibisa
msosi wangu sio wa drafti
sili mpaka nijitume,
maisha yana super shaft
yashanizidi nguvu za
kiume dah....

leo nimepata kesho
nimekosa
nnachohifadhi maumivu tu
life ni ngumu bado
inanichosha
nakula mbichi sili mbivu boo..

huwezi amini bado
kabwela
sina uhuru kama niko jela
huwezi amini bado
kabwela
sina uhuru kama niko jela...

ushindi wangu ni wa
uchafu kwenye vita ya
wasafi
kila nnayemuomba tafu
anataka afanye na ulafi
maisha ni kombolela masikini ndio mlinda kopo
cha msingi ni kuunga tela
mpaka utoke kwenye
msoto
kila jua linapozama
natamani pasikuche hasi inageuka chanya
kapeto anageuka sunche
naona alama za mlango ila
sioni pa kutokea
hii pesa imetoka jando
inataka kuni-babu seya nimegeuka konokono
natembea na mzigo wa
shida
silali, nimekuwa pono
maisha unakwenda na
mida shida zishanipa ustaa,
zaidi ya kanda ya loketo
tumbo umezoea njaa hadi
shibe naiona mseto
vikombe vya uaminifu
nishavivunja mtaani na vijiko vya uhalifu
nishaviweka kwenye
sahani
mi nadhani, haya maisha
yana ramani
na aliyewachorea masikini peni ilimgomea njiani
ah

leo nimepata kesho
nimekosa nnachohifadhi maumivu tu
life ni ngumu bado
inanichosha
nakula mbichi sili mbivu boo

huwezi amini bado
kabwela
sina uhuru kama niko jela
huwezi amini bado
kabwela
sina uhuru kama niko jela
 
Kwa hapa na nyimbo zake kibao nazikubali he real thinks

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom