Hongera Serikali yetu, kuwatosa Acacia kwa kutowatambua huu ndio uanaume!. acacia kula jeuri yake, faces hostile take over, soon itakuwa kwishney!.

I hope they pay the $190 bilion bill.
Nijuavyo Budget yetu kwa mwaka ni Trilion 33, wakitulipa hizi trilion 424 zinatosha kabisha kusimamia budget yetu kwa miaka 13.
 
Kwa iyo P umekubali kama $190 bl ni professional Rubbish na $300m za kishika uchumba ni pipi iliyomo ndani ya plastic ambayo tunalishwa Watanzania huku tukiamini kuna utamu utakuja Yani kama napata Nafasi ya Urais Cheti Cha uprof wa Kabudi nakichoma moto uwanja wa Taifa na nishani anarejesha akiwa nyuma ya nondo za keko huku akiwa kwenye Record ya Msomi mjinga kuwahi kutokea nchini
 
Paskal ni sawa unachokisema na tunakubaliana.Tunapotofautiana ni kwenye uchaguzi wa maneno (hostile takeover) na muda wa kuyatumia hayo maneno.Na kwa mfano wa yule mama mtalakiwa angalia amekwenda chumba cha wageni na siyo nje ya nyumba kabisa; na bwana yule alichoweza kufanya ni kuleta mke mwingine ndani tu. Barrick kama wako serious wawalipe ACACIA- 35+% SHAREHOLDER wasepe. Au labda wanawapeleka mpaka share zishuke thamani?
 
Ahhahhaha nchi hii, Barrick akitulipa 2020 nitampa kura Magufuli.
ntakukumbusha hii, unajua kwamba hiyo siyo sababu pekee ya kumpa au kumnyima Magufuli kura, zipo sababu nyingi saba , mfano itategemea Wapinzani wamemsimamisha nani? itategemea kama hata wewe mwenyewe utakuwa hujabadili msimamo wako juu ya afanyayo Magufuli na msimamo wa upinzani,

Mi siamini kama ACCACIA/BARRICK watatulipa kirahisi hivo,
 
Ahhahhaha nchi hii, Barrick akitulipa 2020 nitampa kura Magufuli.
Kama hii ndio sababu ya kumchagua Magufuli 2020, then rais Magufuli atapata kura nyingi sana 2020, akina sisi tumependekeza uchaguzi wa rais usifanyike to save time, money and resources.

P
 
Bro, umeanza vizuri na presupposition halafu unarudi kulekule kwenye contradiction.
 
Mkuu Chagu wa Malunde, haya ya kuitana ex soldier ni hatari, mambo mengine ya historia za watu ni siri.

Ule ujumbe wako ulionitumia kwenye ndoto, na mimi ni kweli nilikula nae ugali na sato kwenye ndoto na nikamfikishia. Hawa jamaa hawasepi bali wanabadili tuu jina kutoka Acacia kurudia jina lao la zamani la Barrick ila ule mpunga wetu wa kile kishika uchumba chetu cha US $ 300 milioni, kitalipwa.
P
 
Wayakitoa wapi? Kumbuka mabepari wa dunia wanacheza game zao tu.
Kwa nini wasilipe kabla ya kumwondoa Acacia? Kumbuka pia, viongozi wa Acacia wamepewa offer ya kununua hisa zao zilizopo kwa jina la Acacià., huu ni mchezo.
Bepari hana urafiki na mtu asiye bepari.
Hisa zote zikishachukuliwa, na Jina la Acacia kutoweka basi Barrick ni mpya na hakuna deni. Inapaswa serikali ikamate Mali za Acacia kabla hawajauza Mali zao
Kishika uchumba chetu $ 300 mil Barrick watatulipa sasa bila kisingizio sasa, ila ujue Barrick wahuni sana
 
Copy
 
Copy that
 
Baba na mwana tegemea yale yale tu hapo
 

These are business men and women. They care for making money. They can humble themselves if need be. For me, yes, they are one and the same. But for the sake of their assets lying idle and losing the chance to make money, then that is a different ball game. They will allow Acacia to disappear in the face of earth
 
Wanabodi,
Hatimaye huu mtanange wa Acacia kununuliwa na Barrick, hatimaye umefika mwisho jana, kwa Barrick kutoa tangazo la kuinunua Acacia, na Acacia kutoa tango la kukubali kununuliwa na Barrick.

Tangazo la Barrick la Kifo cha Acacia ni Hili
PRESS RELEASES
Recommended Final Offer For Acacia Mining Plc By Barrick Gold Corporation – July 19, 2019

Tangazo la Acacia kukubali kununuliwa na Barrick ni hili

Hii maana yake ni
  1. Sasa mgogoro wa Acacia na serikali yetu, umemalizika rasmi kwa sababu sasa Acacia doesnt exist anymore.
  2. Migodi yote mitatu iliyokuwa chini ya Acacia, sasa itakuwa chini ya Barrick
  3. Yale makubaliano ya serikali yetu sasa yatatekelezwa.
  4. Kwa kuanzia tutalipwa dola milioni 300 zilizokuwa ni kishika uchumba, lakini sasa sio kishika uchumba tena bali ni kifuta machozi cha kusamehe lile deni kubwa la kodi la dola bilioni 190.
  5. Barrick ataunda kampuni mpya ya ubia na Tanzania kuchukuwa shughuli za Acacia
  6. Kwenye hiyo kampuni mpya, serikali ya Tanzania itakuwa na shares asilimia 16%.
  7. Bodi ya hiyo kampuni mpya itakuwa na Watanzania.
  8. Makao Makuu yatakuwa Tanzania
  9. Menejiment itakuwa na Watanzania.
  10. Tutagawana manufaa ya kiuchumi pasu kwa pasu, yaani 50/50.(NB.Manufaa ya kiuchumi ni economic benefits na sio faida profits)
Huu ndio utakuwa ushindi wa kwanza wa kishindo wa rais Magufuli na awamu ya Tano kwa kuanza rasmi utekelezaji wa kwanza wa sheria mpya ya madini.
Hongera Kabudi, Hongera Magufuli, Hongera Watanzania, ila kwenye makinikia, bado kuna lakini!.
Leo tupongezane kwanza, lakini tuzijadili baada ya kusainiwa makubaliano yenyewe!.
Paskali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…