Hongera sana UDOMASA wa UDOM!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera sana UDOMASA wa UDOM!!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Udomasa, Mar 12, 2011.

 1. U

  Udomasa New Member

  #1
  Mar 12, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WanaJF, naomba nianze kwa kuwapongeza UDOMASA wa UDOM kwa kazi nzuri sana waliyoifanya. Kwanza, wamesababisha mapinduzi pale UDOM. "Wameupindua" uongozi wa kiuonezi, kibabe wa the top three leaders. Hawa jamaa walikuwa wanajiona kama miungu ya UDOM!! They were untouchables. UDOMASA imewaleta down to earth, to reality. I never thought this will happen so soon!! However, kwa ujasiri mkubwa wa hawa viongozi wa UODOMASA, the unthinkable has happened.

  Kwa sababu ya "mapinduzi" haya, wafanyakazi wa UDOM tumeweza kulipwa stahili zetu ambazo uongozi ulikataa katakata kutulipa kwa miaka mitatu na ushee hivi. hongera sana UDOMASA!!

  Kazi iliyobaki sasa ni ya kuhakikisha kuwa aidha wote watatu wanaondoka kwa manufaa ya UDOM, au angalau mmoja anaondoka, hasa PFA. Bila PFA kuondoka, 'mapinduzi" yatapungukiwa na maana yake. Kwa kweli vita dhidi ya UDOMASA na uongozi wa chuo bado inaendelea!!

  Lakini, cha ajabu ni kwamba wiki hii nimeona tangazo lisemalo Uongozi wa chuo kwa kushirikiana na UDOMASA unaandaa get together party for next weekend. Hivi kweli UDOMASA mnataka tukakae meza moja kula chakula na hawa watu hawa amabao wametunyanyasa sana kwa muda mrefu, hasa PFA?? Hivi mnataka tukacheze rumba na wanyanyasaji hawa, hasa PFA?? Mimi sipingi haya moja kwa moja kwa sababu najua suluhu huja baada ya ncha ya upanga!! Ila nasema ni mapema mno!! Tungoje kidogo. Nahisi hii ni njama ya hawa viongozi ya kuombea msamaha ili wazo la kuwataka waachie ngazi tulisahau. mimi sitaki tulisahau hili wazo!! bila PFA kuachia ngazi UDOM will never be peacefull!! Believe me!

  Hivi ile get together tuliyopanga wana UDOMASA kufanya baada ya kupata subsistence imefia wapi!! Tungefanya kwanza hii ndiyo tufikirie kufanya hii ya uongozi.

  Nawasilisha, wasa kwa wana UDOMASA wenzangu
   
 2. S

  SAM wa KILUNGU Member

  #2
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  UDOMASA NA UDOM ndo nini? sijaelewa
   
 3. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Haya hongereni.
  Tualikeni na sisi kwenye party yenu.
  Kama mmeandaliwa party na huyo mlacha si muende.
  Kususa haisaidii.
   
 4. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,533
  Trophy Points: 280

  UDOMASA ni kifupi cha University of Dodoma Academic Staff Association

  UDOM ni kifupi cha University of Dodoma

  Natumaini umeelewa mkuu!
   
 5. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,533
  Trophy Points: 280
  :welcome:
   
 6. emmathy

  emmathy Senior Member

  #6
  Mar 13, 2011
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  hongereni, wazo zuri mana umefikiria beyond line. Uko sahihi kimantiki mana mwili uradhi ila roho haikubali kujumuika kwenye gtgether, mnaweza kwenda ila dhamira isibadilike kuhakikisha siku moja wanaohusika wanaondoka. Kwani CAG hakuona tatizo? Kama hajaona inakuwaje mlipwe hela za miaka 3nyuma?
   
 7. B

  Bibi Kizee JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2011
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 213
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Hongereni sana wana udomasa, lakini ebu tuwekeni wazi haswa nilisikia ripoti ya CAG kuwa hakuna ubadhirifu unaofanywa na menejiment ya UDOM haswa mishahara amabayo wafanyakazi walidai ilikuwa inachakachuliwa, na hela mlizolipwa ni kweli ni stahili yenu ila hazina ilikuwa haiwajawahi kukilipa chuo, na nasikia kuwa mishahara ya zaidi ya watu 400 ilikuwa hailipwi na hazina ni memejiment ilikuwa inalipa, sasa hii menejiment taizo lao liko wapi kama hazina wamewapa pesa mliyokuwa mnadai subsistence na transport ambayo hawakuwahi kukilipachuo, na mishahara ya wafanyakazi hazina wamerekebisha hivi mgomvi wenu sio hazina jamani wana udomasa ebu tuwekeni wazi maana hii agenda ya PFA tunashindwa kuielewa haswa tunaposikia kuwa hakuna ubadhirifu UDOM as per CAG report.
   
Loading...