tatum
JF-Expert Member
- Jan 16, 2018
- 5,786
- 4,490
Moja ya Wakuu wa Wilaya katika awamu hii ya tano ambaye kiukweli amekuwa mstari wa mbele kutembea nje ya ofisi na kuona ukweli wa miradi ya maendeleo ,huduma za jamii ktk sekta ya afya,elimu ,maji na huduma zingine kujua namna zinavyotolewa na mamlaka husika kwa kushirikiana na jamii husika naona kabisa Kisarawe mpya inakuja.
Kwa hakika huyu dada atafika mbali sana watumishi wengi wanampenda na huwezi kusikia akitoa matamko yenye utata wala kuwatumisha wananchi wake na viongozi wao maana amaeona jinsi wanavyokabiliwa na hali ngumu na umasikini uliokithiri na hasa ukichanganya na mila na desturi za mikoa ya pwani kwahiyo anakazi ngumu sana kuibadili jamii hiyo ambayo wao kwao umasikini ni kitu cha kawaida tu kwao kutoenda shule wao wanaona sawa tu.
Hongera sana DC Jokate kwa kiliona hilo na kuamua kuwa nao sambasamba ili kuwafanya wabadilike kiumtazama na kimaendeleo.Mungu na akupe nguvu na uweze kufikia malengo uliyojipangia.
wasahili wanasema ukienda kwa wenye chongo vunja lako jicho