Hongera sana 'Captain' Mbwana Samatta 'Poppa' kwa kuamua 'Kujivunja' ili ukwepe 'Aibu' ya Taifa Stars 'Kubugizwa' Magoli na Tunisia

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,571
108,926
Hata ningekuwa ni Mimi GENTAMYCINE ndiyo Wewe Samatta kwa jinsi Watanzania walivyo na nongwa hadi kisununu na wakisahau Kushukuru nami pia ningeongopa (ningejivunja) kama Wewe kwa kusema kuwa 'ninaumwa' ili nikae pembeni na niwaachie Wachezaji wengine wa Taifa Stars waliobaki 'wapambane' Mechi zote hizi mbili tena za muda mfupi tu zijazo na Tunisia.

Kwanza najua kabisa kuwa kwa uwezo walionao Tunisia katika hizi Mechi zote mbili Tanzania (Taifa Stars) inaenda kupokea 'Vikapu' vingi tu vya 'Magoli' yanini 'nijichoshe' na nicheze wakati najua fika kuwa Mimi kama Samatta na CV yangu nikiwemo katika Mechi hizo Mbili tunazoenda Kupokea Vipigo vya 'Kishalubela' thamani yangu nayo itashuka na hata Kudharaulika?

Hongera sana 'Poppa' na nimekukubali mno kwa hii 'Mbinu' yako. Na waliokuwa wakikusema vibaya ni Mashabiki wa Yanga SC sasa wacheze Wao.
 
Mi nachojua ni kua tunakamilisha ratiba tuuu...jumla ya goli kwa mechi zote mbili inaweza kua 9
Nasikia Kikosi kitakachocheza huko na hata hapa Dar es Salaam wakirudi kitajumuisha Michezaji yote 'Mibovu' tu ya Yanga SC je, unadhani kwa zile Winga Mbili 'Viberenge' wa Tunisia na Viungo Wao watatu 'Wanyumbulifu' na 'Fowadi' zao ambazo kila Siku tu zinacheza na Mabeki wa Hispania, Ufaransa, Uingereza, Italia na Ujerumani huyo sijui Bakari Nondo Mwamyeto wako atawaweza? Naona Goli za Kufungwa kama 37 hivi.
 
Goli 37 😅😅😅
 
Wabongo wana nongwa sana yani mbali na mafanikio aloyapata unakuta kuna bwege linamlinganisha na Msuva. Alichofanya Samatta yuko sahihi na ningekua yeye ningeacha kabisa kuichezea taifa stars make wabongo wana nongwa sana.
 
Back
Top Bottom