Mkuu DENAMWE , asante sana, hapa hapa unaponiona ujue ni tayari nimeisha staafu utangazaji rasmi, kwa sasa mimi ni mtangazaji wa kujitegemea kwa kujitolea tuu, walionifaidi ni wale walioniona zamani nikiwa newsroom na vipindi vyangu vya Mada Moto on DTV, Kiti Moto, on DTV na ITV na Ulingo wa Siasa on TVT, vilikuwa moto!.Nimefuatilia utangazaji wako kwenye kipindi chako cha PPR kwenye wiki ya ubunifu.
Nimeuona umahiri wako. Kama kawaida nimefurahia utangazaji wako
Hongera sana Bwana Paschal.
Mkuu Number ni 26 , asante sana kuni tag, ni wewe ndio amenistua na kutembelea uzi huu, bila wewe nisingejua kuwa nimefagiliwa mahali, ila pia humu JF, kuna mijitu ni mi minders sana, ukifagiliwa tuu na mtu yoyote, wataibuka na kusema ni multiple ID, nimejianzishia ID ya kujifagilia!.Ukishatoa shout out una tag ubavu Pascal Mayalla