Hongera sana Bondia Twaha Kiduku

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Jana usiku nilishuhudia pambano baina ya Twaha Kiduku na Bondia kutoka DRC Congo.

Kwa kweli Twaha alipambana kiume na akaweza kumshinda kwa alama(points). Kwa Tanzania ya sasa hakuna bondia anayeweza kupambana na Twaha na kuweza kumshinda.

Tunaiomba Serikali yetu sikivu bondia kama Twaha ni wa kumsaidia li baadaye apeperushe bendera ya yetu kimataifa.

Twaha kwa kweli ni bondia ambaye hapo baadaye atailetea Taifa letu sifa kubwa.

Kwa zawadi ya Twaha leo nimewachinjia wajukuu wangu jogoo kubwa ili kusherekea ushindi wa Twaha.

Majaji walifanya uamuzi wa haki ila alama za Twaha kidogo zilikuwa juu sana kuliko bondia mwenzake.

Hongera sana bondia Twaha.
 
Hivi kina Mayweather, Mike Tyson, Mohamed Ali etc walikuwa wanasakdiwa na Serikali zao? Something is Wrong with Tanzanians and Serikali. Sitashangaa kuona anaalikwa Bungeni alafu na ahadi kibao za uongo na kweli kutoka kwa wanasiasa.
 
Round nane 8 tu siyo sawa...
Waliopendekeza round 8 walipuyanga kweli. Sijashangaa kuona hata yule Mcongoman akilalamika matokeo!

Wangeweka tu round 10 au 12, ili kumpata mshindi wa kweli. Sijaona kabisa mantiki ya kuweka roundi 8 mwenye pambano la kuwania mkanda! Tena mkanda wa Afrika wa UBO!
 
Wamebugi sana aisee...

Na yule mzee kumpiganisha na kijana siyo sawa kabisa...
 
Back
Top Bottom