Hongera Rais Kenyatta kwa maneno ya busara

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
98,180
2,000
KWA HILI RAISI UHURU KENYATA UMESIMAMA MAHALI PA MAKUHANI.

Kwanza pole kwa majukumu ya kuijenga Kenya na Afrika ya mashariki.

Hili ulilosema umenifanya nifumbue macho maana pia Mimi ninamabinti na ninatamani niwaone wakiwa Bora.

Wapo ambao hawajui umesema Nini ngoja niwasimulie hapa.

Umesema hata Kama watakasirika wakasirike lakini huu ndio ukweli wanaopaswa kuupokea.

Kumuamsha mdada wa kazi saa 11 alfajiri na kuwaacha binti zako wamelala Ni kumuandaa binti wa kazi kuwa mke Bora kuliko wanao.

Eti kumtumikisha dada wa kazi apige deki, apike, afue nguo, aoshe vyombo wakati wanao wanaangalia TV. Ni kumuandaa mdada wa kazi kuwa mwanamke anayewajibika kuliko wanao.

Kumuacha binti wa kazi aandae watoto kwenda shule, awaandalie uji mapema, awalishe, awasafishe wakati wanao wanacheza gemu kwenye simu au computer Ni kumuandaa binti wa kazi kuwa mama na mlezi bora kwa watoto kuliko wanao.

Na kwakuwa yote hayo unayafanya kwa masimango na manyanyaso unamfanya mdada wa kazi kuwa jasiri mwenye kuzikabiri changamoto za ndoa yake kuliko wanao.

Ukimaliza kwa kusema mwanao akiwa hajui hayo yote, ndoa ikiharibika mnazungukuka kutafuta maombi kwa wachungaji kumbe ninyi mmeharibu ndoa za watoto wenu.

Msiwasumbue wachungaji.

Nimefikisha Ujumbe wako mzee nami nakaza hapohapo

Msiwasumbue wachungaji.

Hawa ndiyo viongozi tunao wahitaji maana wana mengi sana ya kujifunza kutoka kwao
FB_IMG_1575800076739.jpeg
 
Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
13,992
2,000
Mods wakiendelea kuvumilia uzi wa kijinga kama huu kwenye jukwaa la siasa nao watakuwa wajinga sana
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,612
2,000
Kwa hiyo unataka Mwanaume mwingine Magufuli asikie wivu? Ili iweje? Au una nia ya kugombanisha Wanaume? Mimi nijuavyo ni Watoto na Wanawake ndo huwa na tabia ya kugombanisha aidha Wazazi au kwa Wanawake mabwana wawili, sasa sijui wewe mwenzetu uko wapi? Utoto au Udhaifu?
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,962
2,000
Asante
Uhuru Kenyatta ni rais mshikaji.

Naunga mkono hoja yake ya watoto wasidekezwe, ila watoto wapate true love from home, wasipopendwa tangu nyumbani, then they will never love kwenye maisha yao.

I can imagine baadhi ya wazazi, I doubt kama wanachekaga na wake zao au watoto wao, they were not loved during their childhood, as a result, they never love now.

Unhappy home, makes unhappy family, unhappy family makes unhappy society, unhappy society makes unhappy nation. Ile position ya Tanzania kwenye world happiness index is deserving.
P
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
98,180
2,000
Ndiyo liwe fundisho kwa wale wenye mtazamo tofauti na kujiona kama wao ndiyo malaika wa dunia
Asante
Uhuru Kenyatta ni rais mshikaji.

Naunga mkono hoja yake ya watoto wasidekezwe, ila watoto wapate true love from home, wasipopendwa tangu nyumbani, then they will never love kwenye maisha yao.

I can imagine baadhi ya wazazi, I doubt kama wanachekaga na wake zao au watoto wao, they were not loved during their childhood, as a result, they never love now.

Unhappy home, makes unhappy family, unhappy family makes unhappy society, unhappy society makes unhappy nation. Ile position ya Tanzania kwenye world happiness index is deserving.
P
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
98,180
2,000
Kwa hiyo unataka Mwanaume mwingine Magufuli asikie wivu? Ili iweje? Au una nia ya kugombanisha Wanaume? Mimi nijuavyo ni Watoto na Wanawake ndo huwa na tabia ya kugombanisha aidha Wazazi au kwa Wanawake mabwana wawili, sasa sijui wewe mwenzetu uko wapi? Utoto au Udhaifu?
Tuliza akili wee mnyarwanda
 
jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,603
2,000
Asante
Uhuru Kenyatta ni rais mshikaji.

Naunga mkono hoja yake ya watoto wasidekezwe, ila watoto wapate true love from home, wasipopendwa tangu nyumbani, then they will never love kwenye maisha yao.

I can imagine baadhi ya wazazi, I doubt kama wanachekaga na wake zao au watoto wao, they were not loved during their childhood, as a result, they never love now.

Unhappy home, makes unhappy family, unhappy family makes unhappy society, unhappy society makes unhappy nation. Ile position ya Tanzania kwenye world happiness index is deserving.
P
"TRUE LOVE" ni njia panda kuelekea kusikojulikana.

Upendo wa mkulima kwa mwanae ni kumfunza kulima mchana kutwa (unaweza kumlimisha mtoto wa Mufuruki?)

Jeesika kagradueti huku kilaza! Pascal Mayalla unabisha? Sasa huo ni mfano wa true love?

"Beauty is in the eyes of the beholders"

Uhuru Kenyata kaongea neno la msingi sana.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom