DOFFA
JF-Expert Member
- Jul 31, 2016
- 425
- 233
Katikati ya mwezi wa Oktoba mpk mwanzoni mwa Nov.kulisikika kelele nyingi sana kuhusu wanafunzi wa vyuo vikuu nchini.Kwa tathmini ya haraka wengi walikuwa wanalalamikia kukosa mikopo,wengine kulalamikia vigezo vipya vya utoaji wa mikopo,nitumie fursa hii kumpongeza mh.Rais kwa kuwawezesha vijana wanaostahili kupata mikopo kuwezeshwa na hali ya hewa kutulia.
Tunaamini kuwa siyo makusudi ya serikali kulalamikiwa na vijana wetu wasomi ila ni mapungufu yaliyopo kwenye mifumo yetu ya utoaji huduma na vilevile nawapongeza vijana wetu kwa kuwa wavumilivu pamoja na mapungufu yaliyojitokeza kwenye mifumo yetu.
Nimepata taarifa mbalimbali kutoka kwa baadhi ya wanafunzi kuwa wameshaanza kulipwa fedha zao na wengine wanaendelea kusaini au kukamilisha taratibu za malipo-hongera serikali yetu.
Vilevile nimedokezwa na personal sources kuwa huenda mpango wa kuwa na dodoso kwa wanafunzi wanaoendelea ukafutwa kutokana na bodi ikatumia taarifa walizonazo kufanya uchambuzi,pamoja na hilo nimetembelea tovuti ya www.heslb.go.tz kuona kama kuna taarifa kuhusu dodoso lakini sijabahatika kuiona.Hongera Mh.Rais na serikali yetu tunawaombea kwa Mungu muendelee hivyo.
Laiti,juhudi zisingefanyika makelele yangeongezeka na kuzua mambo makubwa,hongereni wanafunzi wa vyuo vyetu mf.UDSM,SUA,UDOM,MZUMBE,ST.AUGUSTINE,MUHIMBILI,SEKOMU,MANDELA.MWENGE N.K
NINAWATAKIA AFYA NJEMA NA UTUMISHI ULIOTUKUKA.
WASALAAM