Hongera Mh. January Makamba

Hongera Mh. January Makamba

"Kila mtoto atakayeanza darasa la kwanza 2017 ataripoti na mche wa mti, ataupanda na kuutunza kwa miaka yote atakayosoma - Waziri Makamba"

View attachment 420974

Mimi ningeshauri elimu ianze ili wanafunzi pamoja na wazazi wapende kupata na kutunza miti. Rais Nyerere alikuwa akitumia hotuba zake kuwaelimisha wananchi kupenda na kupanda miti na watu walitokea kupenda kupanda na kutunza miti. Alizoea kusema: "Kabla ya kukata mti panda mitatu". Binafsi nili'implement' kauli mbiu hii hadi leo hii napanda na kutunza miti si kwa kulazimishwa, bali kwa kupenda mwenyewe kwa sababu nilielimika na pia kilichonisaidia nilisoma shule yenye mchipuo wa kilimo kwa miaka 6 na hadi sasa elimu ya kilimo na mazingira iko kwenye damu yangu. Bado naandaa mazingira ya sehemu nilipohamia na nataka uwe mfano kwa Watanzania wenzangu kujifunza kupenda na kutunza mazingira.
 
Usafi wa mwisho wamwezi umewashinda kilaleo wanaanzisha vijistail vya ajabu...basi kila waziri na naibu wake apande miti100 kila jumamosi na aitunze!!
Bora angeagiza kilashule itengewe eneo spécial lakupanda miti tena ya matunda ili vijana wajifunze kilimo Pia.
tukijua kujipanga ata chakula cha wanafunzi wanaweza kuwa na utaratibu wa kujilimia wenyewe badala ya kuwashindisha njaa
 
Hilo lilitakiwa liwe tamko la pamoja kati ya wizara ya elimu,..., mazingira...., Kilimo... Maji na umwagiliaji ...fedha na mipango,.... pamoja na wizara ya Ardhi.
=====
Nafikiria shule za msingi zilizo mijini wanafunzi watawezaje kutekeleza hili? Tafakuri ya kina kwakushirikiana na wadau wengi ni muhimu .

Wakuu hakuna haja ya kumkebehi kikubwa ni kumuunga mkono kwa kumpa ushauri namna ya kutimiza hili kwa ufanisi kwa manufaa ya watanzania wote.
 
Nawaza tu watoto wanaosoma zile shule za milimani Mwanza watapanda juu ya mawe
 
Shule sizitageuka misitu.
Piga hesabu hii miti itaoteshwa maeneo gani tofauti na shuleni?
 
Sasa afanyeje wakuu ili aandikwepo c kuwazawaza kama hvi wakuu.. Ngoja nami niandae tamko coz nimebaki mmi tu "sipendagi ujinga mimi"
 
Ina maana mtoto akihama shule, atahama na mche wake? Nadhan analeta siasa za majalalani
 
Safi sana Makamba,
Chama la wapingaji chadema watanyooka tu awamu hii
 
"Kila mtoto atakayeanza darasa la kwanza 2017 ataripoti na mche wa mti, ataupanda na kuutunza kwa miaka yote atakayosoma - Waziri Makamba"
View attachment 420974

Loooh, agizo hili linahitaji ufafanuzi. Je, kwa shule za mijini mfano Uhuru Mchanganyiko, Bunge, Olympio etc ambazo hazina maeneo ya wazi ndani ya uzio wake na zina wanafunzi zaidi ya 1,000 hiyo miche 1,000 wataipanda wapi??? Au kuna mtu ana mradi wa kuanza kuuza miche ya miti na analenga kuuza miti bila kujali matokeo bayana.

Hii kauri inanikumbusha mambo ya maagizo ya kufunga speed governor, dawa ya pancha ya OKO etc nayo tunahisi ilikuwa ni miradi ya watu, supply ilipouzwa yote tu na usimamizi wa maagizo ukafifia.
 
Mimi ningeshauri elimu ianze ili wanafunzi pamoja na wazazi wapende kupata na kutunza miti. Rais Nyerere alikuwa akitumia hotuba zake kuwaelimisha wananchi kupenda na kupanda miti na watu walitokea kupenda kupanda na kutunza miti. Alizoea kusema: "Kabla ya kukata mti panda mitatu". Binafsi nili'implement' kauli mbiu hii hadi leo hii napanda na kutunza miti si kwa kulazimishwa, bali kwa kupenda mwenyewe kwa sababu nilielimika na pia kilichonisaidia nilisoma shule yenye mchipuo wa kilimo kwa miaka 6 na hadi sasa elimu ya kilimo na mazingira iko kwenye damu yangu. Bado naandaa mazingira ya sehemu nilipohamia na nataka uwe mfano kwa Watanzania wenzangu kujifunza kupenda na kutunza mazingira.
Mkuu usilinganishe kauli za ajabu na hotuba za Nyerere.
 
Back
Top Bottom