Hongera mbunge Shah na ITV

kingadvisor

Senior Member
Dec 21, 2011
109
30
Napenda kumpongeza mbunge Abudulkarim Shah kwa moyo na kujitolea aliouonyesha kusaidia wahanga wa mafuriko Dar es salaam.kajitolea kukodi boti na kujitolea yeye mwenyewe kufanya kazi ya uokoaji katika mazingira hatarishi .

Wabunge wangekukuwa wanajitolea hivi kama huyu mbunge kwenye maeneo hatari ya majanga kama huyu ningeunga mkono waongezewe posho lza ubunge akini kwa sasa HAPANA.Labda aongezewe huyu Abdulkarim SHAH.Wengine wasubiri.

Pia niipongeze ITV kwa taarifa murua ya habari iliyokuwa na muda mrefu sana wa kuonyesha taarifa za mafuriko.Ndivy hata CNN na BBC wanavyofanya litokeapo jambo kubwa coverage ya taarifa inakuwa ndefu.Taarifa za habari za TV zingine walionyesha taarifa muda mdogo utafikiri ni Non issue na walionyesha zaidi taarifa zenye kuonyesha picha ya msomaji taarifa ya habari sura yake na anayosoma na viongozi na watoa maoni wakiongea,badala ya kuonyesha muda wa kutosha mafuriko yenyewe yalivyokuwa na waokoaji wakiwa kazini.Nadhani iko haja wenye TV kujua tofauti ya taarifa ya habari ya TV na radio kuwa tofauti yake si kuwa kwenye radio humwoni mtangaziji bali kwenye TV unamwona siyo hivyo.Tofauti ni kuwa Kwenye TV unaliona tukio linalotangazwa wakati kwenye Radio hulioni.Hawa wahariri wa TV wanatakiwa warudishwe shule za utangaziji au waende ITV,BBC,CNN ,AL JAZEERA N.K wakajifunze.Hata MLIMANI TV warudi shule.
 
mkuu wa kaya na yeye ashukuriwe kwa kuchukua picha za mafuriko kwa helikopta..
 
Angekuwa ni mbunge wa Dar es salaam tungesema katimiza wajibu wake lakini huyu Abdulkarim Shah ni mbunge wa Mafia hivyo kusaidia watu wa Dar es salaam ni zaidi ya kutimiza wajibu wake!
Mkuu! hakuna wana-mafia katika hayo mafuriko!? wapiga kura wake walikuwepo...ofcourse ni mbunge wa jamuhuri ya muungano wa tanzania not unless otherwise hilo ni jimbo tu anawajibika kwa watanzania hivo ni wajibu wake.
 
katimiza wajibu wake said lead by example

Wewe umepotelewa na fuse za akili? kwani huyu ni Zungu, huyu ni MBUNGE WA MAFYA! yeye ameonesha uungwana wa kuwa sisi sote TAnzania ndugu, halafu naomba kuuliza! huyu si yule alikuwa anasemwa kuwa amegawiwa kiwanja mafya au sio huyu? Ama kweli amesakamwa kumbe ni mtu mzuri wa mfano! wengine mbona hatuwaoni! Zito kabwe yuwapi? kina Mbowe na Slaa wapo wapi? zile helicopter zao imekuwaje? au ??? maana huwa kitu kidogo wapo mstari wa mbele au mnapendsifa za bure? kweli nimewadharau sana !
 
Mkuu! hakuna wana-mafia katika hayo mafuriko!? wapiga kura wake walikuwepo...ofcourse ni mbunge wa jamuhuri ya muungano wa tanzania not unless otherwise hilo ni jimbo tu anawajibika kwa watanzania hivo ni wajibu wake.

Anyway yote heri mkuu ila wabunge wa Dar sikuwaona kwenye hayo mafuriko wakihangaika kuokoa ,labda wanaanda waraka wa kisomi na kitaalamu wa rambi rambi ambao utatolewa kwa vyombo vya habari badala ya kupelekwa kwa wahanga wa mafuriko kama ule wa DR.slaa uliotolewa na Chadema kuonyesha masikitiko yao kwa maafa yaliyotokea

Nadhani vyombo vya habari nao siku hizi ni wabunge.Maana wakuu wa vyama na serikali wakitoa hizo salamu za rambi rambi huwa zinapelekwa kwa vyombo vya habari .Yaani mazishi kinondoni salamu za rambi rambi zinapelekwa ukumbi wa habari maelezo katikati ya jiji.Vyombo vya habari jiandaeni kupokea nyaraka za kusikitishwa na yaliyotokea.Hivi mkizipokea huwa mnazipeleka wapi wakati nyie sio wahanga wa hayo majanga?
 
Mkuu! hakuna wana-mafia katika hayo mafuriko!? wapiga kura wake walikuwepo...ofcourse ni mbunge wa jamuhuri ya muungano wa tanzania not unless otherwise hilo ni jimbo tu anawajibika kwa watanzania hivo ni wajibu wake.

Huo haukuwa wajibu wake ! wewe ulikuwepo? maana kama hiyo ni tija basi na wewe kama Mtanzania ulitakiwa ukakodi boti pale ferry ukawaokoe wenzetu mnapenda sana kusema sema , nadhani angekuwa mbowe hapo au slaa sifa zingetoka! muwe na shukrani hebu sifieni siku moja moja jamani looh!
 
Sifa mojawapo ya Kiongozi bora!
Tukisema JK ni mtawala siyo kiongozi wengine wanabisha!
 
Sifa mojawapo ya Kiongozi bora!
Tukisema JK ni mtawala siyo kiongozi wengine wanabisha!

Wewe kwani ulitaka JK afanye nini? nini maana ya RAis na mawaziri wake, wabunge, wakuu wa mikoa, wenyeviti wa serikali za mitaa, hao wabunge wenu kina mbowe na slaa mbona hatukuwaona? na mbona hawakuonesha mfano tukawaona wa maana sana ! Rais aliota kuwa yangetokea mafuriko? na hata angekuwepo angezuia? mbona mnashindwa kufikiri kama kweli ni great thinkers! ile ni QUDRA ya Mwenye Ez Mungu , alie juu,.. na huwezi kuiepuka tunatakiwa tu kumshauri RAis nini kifanyike kwa wale wenzetu wa MAbondeni na sio kulaumu!
 
kwa haya maandishi..hivi na wewe ni great thinker??
 
waandishi wetu miezi 3 pale buguruni tsj...wao wasanii wa bongo movie na bongo flavour ndo habari
 
Nampongeza sana Huyu mbunge ila nina swali moja tu kwake!!!angejitahidi kutafuta suluhu ya usafiri hasa wakati wa kushuka toka kwenye meli....kuja nchi kavu!!angetafuta boti isaidie ....anakimbilia dar kwenye media sisi wakaazi wa mafia tunazama kila siku na shida kibao hasa kwa wamama na watoto!!!!!cheap popularity!!
 
Asee sijaelewa yaani
naona kama hapa ni kiwiliwili cha hii report
hebu nambie ilikuwaje
make tangu nimevamiwa
na mafuriko hapa tabata
no umeme
ni mawasilianoi yoyote
kafanyaje huyu mhishimiwa member of parliament?
 
Kwa suala la umeme ni la TANESCO,Barababara kuna wenyewe.Mpaka wapende.Mimi kuna siku barabara ilifumuka nikaamua kubeba mavifusi ya mawe n.k ili nitengeneze nilihojiwa kama mimi ni engineer,kibali nimetoa wapi nilihojiwa kuanzia serikali ya mtaa hadi wale akina wafanyakazi koko ambao ukiwauliza kwani wewe unayenihoji ni nani? wanakwambia hunijui mimi utajuta!! usipende kunijua wala kunitaka kitambulisho.Anyway kama mnabisha tafuta mtu wa kujitolea awe wewe,mbunge au nani ajaribu kutengeneza hayo maumeme,na madaraja yaliyobomoka uone mziki wake.Labda ujaribu wewe siamini kuwa ukoo wenu wote ni maskini na wachovu atakuweko walau mmoja mwenye uwezo mwambie ajaribu.Mbunge kafanya sehemu yake.
 
Nimejifunza kitu hapa, na ninatoa pendekezo....kuna umuhimu gani wa wasomaji habari wa tv kuonekana? kwani sisi tunawaangalia wao au tunawasikiliza na kuangalia matukio? Kuanzia sasa wawe wanatokea kujitambulisha na kuendelea na habari bila kuonekana na mwishoni waonekane wanapoaga watazamaji.
 
Back
Top Bottom