Umeongea point sana kwasababu hatujawazoea hadharani tunahisi wanaakili lakini ukweli ni mamburula kama tulivyoona jana very shame swali dogo nionyeshe kitambulisho anatoa bastoramaybe kitambulisho chake ni pistohahaahah kwa kuwa kazi zao wanafanya kwa siri basi tumejenga picha ni watu wenye akili za hali ya juu, kumbe ukiwaleta hadharani ni ma bashite sana. amini mkuu ndo hao vilaza
Povu la nini tena mkuu
Hahahaaaa kwa hiyo ni polisi au sio?sekta ya vilaza?Mambo yakusema uyo alietoa silaha ni usalama ni uongo akuna kitu kma icho uyo sio usalama akuna usalama pumbavu kma uyo usalama wanatumia akiri na nguvu inakuja baada yaa
Silaha inakaa kishamba vile. Mbona ingechomolewa na yeyote wa nyuma. Sio mwana usalama wala nini, ni lofa tu wa Bashite.Kinga ni bora kuliko tiba, usalama alikuwa sahihi kutoa silaha bila kuitumia ili kupunguza uwezekano na ulazima wa kuitumia. watu wakijuu kuwa kuna silaha wanabadilisha tabia.
Kitenge alikuta kitambulisho kimesharudishwa, angekiona angekimbia kama Harmorapa.Mtamponza jamani.
Ila nilifurahia show... au hakujua kua jamaa ana 'KITAMBULISHO'?
ILA
Nimejaribu kujiuliza kwa hali ya kawaida kuna raia wa kawaida anaweza kuwa na ujasiri wa namna hiyoo. Nikapata jibu inawezekana na yeye ni wale watu wanaovaa suti nyeusi(mashushu).mpaka sasa bado sijapata jibu sahihi .
Ule mguu wa kuku hakuuona alikuta umesharudishwa, waliuona walimbia hadi Mtwara.Kwangu kafanya Kosa Kubwa Sana na la Hatari kwake .
Unapokwenda Kuoka Tukio la Mtu anayefanyiwa Attack kwa Kutumia Silaha ya Moto ..nilazima uwe Umejiandaa na Silaha Mfanano wa adui anayoitumia , iki pakitokea mazungira ya Matumizi basi uweze kujihami .
Yeye kaenda na koti la Suti la Pink na simu Kubwa Kama Bomu , Halafu anakaribiana na Adui almost Zero Distance.
Mnaomsifia Shame on You
kwa hiyo atakuwa nani labda !?Mambo yakusema uyo alietoa silaha ni usalama ni uongo akuna kitu kma icho uyo sio usalama akuna usalama pumbavu kma uyo usalama wanatumia akiri na nguvu inakuja baada yaa
Naunga mkono kwa hili, ndio maana tulikuwa tukikaa nao kwenye moja moto moja baridi walikuwa wanakauli zao " unajua mimi ni nani", hakuna maadili tena kwenye hili.Wenye akili walikuwepo enzi za mwalimu, siku hizi wanapeana nafasi kidugu hasa wamu ya nne imeingiza mabashite wengi wasio na vigezo
Actually ni kinyume chake. Hongerah kijana wa Usalama wa Taifa kwa ni alitumia tu Busara na ukumbuke hakuwa peke yake. They are trainded usifikirie alishindwa bali alitumia tu busara ya kumuachia kitenge na kiduku chake!Siku ya leo kumetokea tukio la kustaajabisha ktk tasnia ya siasa nchini tanzania. Tukio hilo limetokea dar es salaam wakati aliyekuwa waziri wa michezo na tamaduni Nape nauye akitaka kuongea na waandishi wa habari baada ya kuondolewa katika nafasi yake ya uwaziri. Nape ameondelewa leo hii katika nafasi yake baada ya mh rais kufanya marekebisho madogo katika wizara mbili.
Baada ya mh Nape kuwasili maeneo ya Pritoria hotel kulitokea tafrani baada ya watu walitambuliwa kuwa ni maafisa usalama kumzuia asiongee na waandishi na kumtaka arudi ndani ya gari. Wakati sakata hilo likitokea mmoja wa maafisa usalama alitoa bastola na kumtishia Mh Nape ambaye naye hakustuka . Afisa huyo aliirudisha silaha hiyo kiunoni kisha kuanza kumsukuma Mh nape kumrudisha ndani ya gari. Pasipo kutarajiwa kijana mmoja mtanashati aliyevaa koti jekundu alionekana kujongea kujua kinachoendelea baada ya kuona tafrani ikitokea.
Kijana huyo aliweza kutambuliwa kuwa ni mtangazaji maarufu Maulid Kitenge. Kijana huyoo aliweza kuingilia kati na kumtoa afisa usalama kwa nguvu eneo la tukio huku akimsukuma bila kuogopa. Hakika alifanikiwa akamuondoa eneo hilo na afisa huyo alitii bila shurti. Wengi tumeona na kustaajabu na hatuna budi kumpa hongera maulidi kitenge kwa ujasiri aliouonesha.
ILA
Nimejaribu kujiuliza kwa hali ya kawaida kuna raia wa kawaida anaweza kuwa na ujasiri wa namna hiyoo. Nikapata jibu inawezekana na yeye ni wale watu wanaovaa suti nyeusi(mashushu).mpaka sasa bado sijapata jibu sahihi .
Waungwana ninyi mnaonaje nawasilishaView attachment 485865View attachment 485866View attachment 485867View attachment 485868
Bongo buana, ndio maana hata Bashite sasa amebatizwa kuwa TISS!Kwani kuna mtu asiyejua kwamba kitenge ni usalama. Yule yupo katika ivi vyombo vya habari kwa kazi maalum. Jezi nambari 9 mgongoni Maulidi mbaraka wa kitenge