Hongera Marando kwa kumpangua Masati:Vita ni Vita Muraa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera Marando kwa kumpangua Masati:Vita ni Vita Muraa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Simple, Feb 12, 2010.

 1. Simple

  Simple JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2010
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 249
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Pongezi zangu kwako Bwana Marando kwa kupangua hukumu ya kipambavu na ya uonevu aliyoitoa Jaji Masati kwenye kesi ya Nguza family.
  Jaji Masati ni mtu makini, mwenye uzoefu mkubwa wa sheria, mcha Mungu na asiyekuwa biased. Lakini ilipofika kwenye kesi hii,,mzee huyu alichemsha mno kwa kutumia jazba, upendeleo kwa upande wa mashitaka na kutoa hukumu upesi upesi bila kuzingatia uzito wa kesi yenyewe.(Sijui alishinikizwa au utashi wake ndo uliishia pale)
  Binafsi nilikuwepo Kisutu siku Nguza family wanahukumiwa jela ya maisha, niliingiwa na mshtuko mkubwa baada ya Jaji yule kumaliza kusoma hukumu yake kwa maneno ya jazba na chuki.

  Pongezi zangu kwa Marando kwanza kabisa kwa kuisaidia familia ya Nguza kutendewa haki( vijana wawili wako nje sasa), pili kwa kuanisha upuuzi wa Jaji Masati.

  Sijui Jaji huyu anajisikia hivi sasa, ukizingatia amewapotezea vijana wale wawili miaka saba, ambayo walifungwa. Wangekuwa wanawe sijui angejisikiaje?

  Imefika kipindi sasa, waTanzania tuachane na sheria za jazba na uonevu na kuiacha haki isimame.
  Aliyekosea aadhibiwe TU pale inapothibitika beyond reasonable doubt, sio kutumia mitazamo binafsi.

  Mapambano yanaendelea Marando,,usikate tamaa...kama vipi wapeleke kina papii wakafungwe Congo maana hapo Bongo ngoma yao ishakuwa ingwe.
   
 2. b

  bnhai JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2010
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,234
  Likes Received: 1,385
  Trophy Points: 280
  Huna uhakika na unachokiongea na pia huna ufahama wa kile unachokizungumza. Hiyo haitoshi bado wewe si mkweli. Unasema Jaji Masati ndio alimuhukum babu Seya? Km unakumbukumbu nzuri utakumbuka kuwa Jaji Masati alikuwa miongoni mwa majaji waliosikiliza rufaa ya kesi ya kina Seya.
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,534
  Likes Received: 1,542
  Trophy Points: 280
  na wewe hujui .Jaji Masati alikuwa mwenyekiti wa jopo la majaji hao..
   
 4. b

  bnhai JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2010
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,234
  Likes Received: 1,385
  Trophy Points: 280
  Pls sijatoa details za mwenyekiti wala makamu mwenyekiti. Nimeongelea majaji as a group. Read between lines
   
 5. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #5
  Feb 12, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Na wewe pia huna unalolijua,kwenye mahakama ya rufaa JAJI NATALIA KIMARO ndio alikuwa mwenyekiti,jana nilisaidia kupost nakala ya hukumu hiyo,tafuta thread iliyoandikwa HUKUMU YA BABU SEYA HII HAPA usome,na wewe mwenye thread hii Jaji MASSATI hajamuhukumu Babu SEYA kule Kisutu aliyemhukumu ni hakimu anaitwa mama Lyamuya.,tena ujue hao jamaa hawawezi kupelekwa KONGO
   
 6. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #6
  Feb 12, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 8,117
  Likes Received: 2,415
  Trophy Points: 280
  Ndio sababu ya kuweka appellate machinery ili kuondoa matatizo kama haya. Mara nyingi interpretaion ya sheria na ushahidi sio straight forward hivyo na maamuzi ya majaji/mahakimu wawili yanaweza kuwa tofauti.
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Feb 12, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,534
  Likes Received: 1,542
  Trophy Points: 280
  mwenyekiti wa kijiji chenu au
   
 8. I

  IMBOMBONGAFU Senior Member

  #8
  Feb 12, 2010
  Joined: Jun 7, 2009
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sawa tumpe Ubunge kwa kutetea wabakaji
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...