Simple
JF-Expert Member
- Feb 6, 2009
- 249
- 121
Pongezi zangu kwako Bwana Marando kwa kupangua hukumu ya kipambavu na ya uonevu aliyoitoa Jaji Masati kwenye kesi ya Nguza family.
Jaji Masati ni mtu makini, mwenye uzoefu mkubwa wa sheria, mcha Mungu na asiyekuwa biased. Lakini ilipofika kwenye kesi hii,,mzee huyu alichemsha mno kwa kutumia jazba, upendeleo kwa upande wa mashitaka na kutoa hukumu upesi upesi bila kuzingatia uzito wa kesi yenyewe.(Sijui alishinikizwa au utashi wake ndo uliishia pale)
Binafsi nilikuwepo Kisutu siku Nguza family wanahukumiwa jela ya maisha, niliingiwa na mshtuko mkubwa baada ya Jaji yule kumaliza kusoma hukumu yake kwa maneno ya jazba na chuki.
Pongezi zangu kwa Marando kwanza kabisa kwa kuisaidia familia ya Nguza kutendewa haki( vijana wawili wako nje sasa), pili kwa kuanisha upuuzi wa Jaji Masati.
Sijui Jaji huyu anajisikia hivi sasa, ukizingatia amewapotezea vijana wale wawili miaka saba, ambayo walifungwa. Wangekuwa wanawe sijui angejisikiaje?
Imefika kipindi sasa, waTanzania tuachane na sheria za jazba na uonevu na kuiacha haki isimame.
Aliyekosea aadhibiwe TU pale inapothibitika beyond reasonable doubt, sio kutumia mitazamo binafsi.
Mapambano yanaendelea Marando,,usikate tamaa...kama vipi wapeleke kina papii wakafungwe Congo maana hapo Bongo ngoma yao ishakuwa ingwe.