Hongera Lowassa kwa kuiadabisha CCM

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
122,490
96,054
Pongezi za kipekee mh Edward Ngoyai Lowasa,rais kipenzi wa mioyo ya mamilioni ya watanzania kwa kuendelea kukaa kimya hata pale unapo dhihakiwa na viongozi hata wana chama wa ccm na mawakala wao,uamuzi wako umekuwa ni adhabu tosha kwa maadui zako ambao sasa wameamua kuajiri vijana kwenye mitandao mbali mbali ili kukukebehi na madharau mbali mbali,adhabu hii kwa ccm ni hatari kuliko kuwachapa bakora.
 
Mkuu Mmawia hakika una moyo wewe! Hata baada ya kipigo chote mlichopata unaona Lowasa anaiadabisha ccm?
 
Chadema ilikuwepo kabla ya Lowassa kuhama CCM, na tena ilikuwa ni chama imara, pendwa na chenye nguvu na ushawishi wa kutosha, hasa katika miji mikubwa ya Tanzania.

Hata Ukawa iliasisiswa kabla ya Lowassa kukatwa na kuhamia CDM. Kwa misingi hii hamna mtu anayeweza kuja na takwimu halisia eti bila Lowassa mambo yangekuwaje UKAWA?? Kama yupo azilete.

Hoja yangu ni hii;
Lowassa mpaka sasa amegeuza kila aina ya mafanikio ya UKAWA kuwa yake binafsi na kujinasibu kuwa yeye ndo ameyaleta. Amekuwa akijinasibu kwa kauli za kujisifia binafsi kana kwamba Chadema na Ukawa havikuepo na yeye ndo alikuja kiuasisi Chadema na muungano wa Ukawa.

Kauli za Lowassa zinakiweka chama mikononi mwake, na si mikononi mwa wanachama waliosumbuka kukijenga chama hiki kwa machozi, jasho, damu, vifo, njaa, na kudhalilishwa na Nguvu za Dola.

Mfano wa kauli za Lowassa;

1. "Nimewawezesha wapinzani kufikisha wabunge zaidi ya 100, tukiweka na viti maalum"
2. "Nimewasaidia kushikilia jiji la Dar es salaam"
3. "Nitagombea 2020, najiandaa na uchaguzi mkuu "
4. "Nimeufanya upinzani kuwa na nguvu kuliko wakati wowote"

Na nyingine nyingi zenye utata!

Swali ni je, kwanini hizi "nime" zisiwe "chama kime"? Halafu toka lini Lowassa amefuta taratibu za kumpata mgombea urais ndani ya chama na kujihakikishia nafasi ya kugombea uchaguzi mkuu 2020??

Lowassa apewe onyo, na afunzwe kuwa siasa ni collective and intergrated efforts na sio One man show or else mtwambie kama amekabidhiwa chama mikononi mwake, na lini ilifanyika hivyo.
 
Nafikiri yeye ameadabishwa na mbowe,maana hela zake kaliwa na urais alioaminishwa kuupata kapigwa na Magufuli na mbowe kafanya kusudi maana alijua kama Magufuli lazima awagalagaze
Kwa wenye akili tunajuwa wewe nenda jikoni uandae mlo wa usiku
 
Mkuu Mmawia hakika una moyo wewe! Hata baada ya kipigo chote mlichopata unaona Lowasa anaiadabisha ccm?
Ungekuwa unajua hesabu hata ile ya kujumlisha na kutoa husinge leta hiyo post yako,kati ya ccm na cdm nani alipoteza kwenye uchaguzi uliopita?
 
Akili gani utakuwa nayo wewe wakati hapo ulipo hata hujielewi maana toka lowassa apigwe chini umekuwa kama umechanganyikiwa hata unashindwa kuangaika kila ukikaa lowasa utafikiri basha wako
Kumbe wewe unayeshinda lumumba kuikingia ccm unakazi nyingine iliyo jificha siyo?
 
Pongezi za kipekee mh Edward Ngoyai Lowasa,rais kipenzi wa mioyo ya mamilioni ya watanzania kwa kuendelea kukaa kimya hata pale unapo dhihakiwa na viongozi hata wana chama wa ccm na mawakala wao,uamuzi wako umekuwa ni adhabu tosha kwa maadui zako ambao sasa wameamua kuajiri vijana kwenye mitandao mbali mbali ili kukukebehi na madharau mbali mbali,adhabu hii kwa ccm ni hatari kuliko kuwachapa bakora.
WEWE MMAWIA NI BWEGE KWELI. LOWASSA AMEADABISHA NINI WAKATI KAANGUKIA PUA NA UROHO WAKE WA MADARAKA????
 
Wewe ndio unaona noma na kuanza kubadili mada baada ya kuona nimejua unachoangaika nacho kila wakati unatuletea habari zisizokuwa na kichwa wala miguu za huyo mende wako
Naona ban ilee inakunyemelea
 
Pongezi za kipekee mh Edward Ngoyai Lowasa,rais kipenzi wa mioyo ya mamilioni ya watanzania kwa kuendelea kukaa kimya hata pale unapo dhihakiwa na viongozi hata wana chama wa ccm na mawakala wao,uamuzi wako umekuwa ni adhabu tosha kwa maadui zako ambao sasa wameamua kuajiri vijana kwenye mitandao mbali mbali ili kukukebehi na madharau mbali mbali,adhabu hii kwa ccm ni hatari kuliko kuwachapa bakora.
Kwani Lowasa kakaa kimya ama kaishiwa na hoja? Mbona kila tukio linapotokea haachi kujitokeza kwenye media? Kaanza mara ooooh wafanyabiashara waliounga mkono UKAWA wananyanyaswa na serikali; akaja na ngonjera nyingine eti wabunge mizigo wa ukawa watashughulikiwa. Akaja tena na hoja ya kupinga bomoa bomoa. Almradi anafanya siasa za matukio
 
Hahahahahaaaaa! Mmawia! Mbona unamtisha? Kisa ni kukuambia ukweli?
Mkuu siyo namtisha ajiandae kwanza kwa kweka kifurushi cha kutosha na pia kwa kupigwa ban maana naamini atarusha ngumi hewani
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom