Nachukua nafasi hii kuwapongeza Chadema na Mhe. Lema kwa ushindi kwenye kesi ya Ubunge wa Arusha. Nilidhani na leo mtasema CCM, Nape na Ikulu wameingilia kesi....MKISHINDA HAKI IMETENDEKA, MKISHINDWA KUNA MIKONO YA IKULU...! Ndo mnakua lakini, mkikua mtaacha mtajifunza majibu ya watu wazima kwenye mazingira kama hayo. Mdogo wangu Lema umeiona Arusha ilivyokuwa imetulia bila maandamano na kelele zisizo na msingi... Endeleza utulivu huu ambao naamini umejifunza kwa kipindi ulichokaa nje ya bunge....!
Kiongozi ni kuonyesha njia, onyesha njia ya maendeleo sio maandamano na fujo. NARUDIA KWA HILI HONGERENI CHADEMA,HONGERA LEMA!!!
Nashukuru kwamba umeona haki imetendeka, nadhani kinachofanya watu wasiwe na imani na mahakama zetu ni mfumo wa upatikanaji wa majaji, hata hivyo tujitahidi katiba mpya iweke misingi mizuri ya seperation of power ili mahakama iwe huru na wewe uweze kukubaliana na mahamuzi ya mahakama hata kama ccm itakuwa imegeuka chama cha upinzani. Pili arusha na Tanzania itatulia na kuwa na Amani kama tu haki itatendeka na si vinginevyo.