Hongera KBC: Wasanii Tanzania bure kabisa

Hongera KBC: Wasanii Tanzania bure kabisa

Mmekalia majungu tu wenzenu rwanda na Burundi wanawakubali hao wabongo, kama kitu hukipendi wewe piga kimya filamu za bongo zipo nzuri na mbaya pia kama ilivyo huko kenya mnakosifia nzuri zipo na mbaya kama kawaida,,
 
Mi sio msanii wa bangi muvi wala gongo muvi!!ila mleta mada nanyi nyote mliomsapoti mmeshaziona muvi zote za bongo?au mnaongea kwa hzo mbili tatu mlizoziona?!Mleta mada nanyi mlomsapoti km hamna vielement vya ukenya cjui,mana mnataka kuendelea kuwabrain wash watz waendelee kujiona si mali kitu na waendelee kutukuza na kushadadia vya nje!unajua unapolinganisha vitu hakikisha kuna fair ground!!hv mmeshaziona muvi zote za wakenya nyie?!mm ninachojua kwa east africa and central industry ya filamu inayokuwa kwa kasi ni ya bongo,congo,rwanda,burundi,kenya na uganda kote huko kuna watu wanatazama bongo muvi!kenya upande wa uigizaji walianza mapema zaidi kulinganisha na tz lkn film industry ya tz ndo imekuwa kwa kasi zaidi!so,its the mata of time tu,hata wasanii wa holywood walianzia hukuhuku tulikoanzia sisi!JIKUBALI,JIPE MUDA ILI UFANYE MAZURI ZAIDI!

Tunapenda tuendelee ndio maana tunawasema Hata vitabu vya dini vinatuasa hivyo - Soma Mhubiri 7:5

Heri kusikia laumu ya wenye hekima, kuliko mtu kusifia wimbo wa wapumbavu.

Hatuwezi kuwa wasanii wote ila anayechagua kwenda huko atuletee best product. Jamani miaka zaidi ya 15 sasa tupo pale pale?
Mbalamwezi1
, hata kupanga viti na meza vionekane kama mandhari ya mahakama kunahitaji fair ground? Tubadilike bwana hata sisi walaji ifikie mahala tukatae bidhaa mbovu!
 
Futuhi jamani,huwa najiuliza hawa jamaa wanafanya nini haswaaaa!!!!
Wanakera sana.
Sasa hizi movie duh ngoja niache tu
 
Mi sio msanii wa bangi muvi wala gongo muvi!!ila mleta mada nanyi nyote mliomsapoti mmeshaziona muvi zote za bongo?au mnaongea kwa hzo mbili tatu mlizoziona?!Mleta mada nanyi mlomsapoti km hamna vielement vya ukenya cjui,mana mnataka kuendelea kuwabrain wash watz waendelee kujiona si mali kitu na waendelee kutukuza na kushadadia vya nje!unajua unapolinganisha vitu hakikisha kuna fair ground!!hv mmeshaziona muvi zote za wakenya nyie?!mm ninachojua kwa east africa and central industry ya filamu inayokuwa kwa kasi ni ya bongo,congo,rwanda,burundi,kenya na uganda kote huko kuna watu wanatazama bongo muvi!kenya upande wa uigizaji walianza mapema zaidi kulinganisha na tz lkn film industry ya tz ndo imekuwa kwa kasi zaidi!so,its the mata of time tu,hata wasanii wa holywood walianzia hukuhuku tulikoanzia sisi!JIKUBALI,JIPE MUDA ILI UFANYE MAZURI ZAIDI!

Una insight nzuri sana mtu wangu. Mimi pia naziona hazina viwango. Ni kwakua tu nafananisha na Hollywood.

Kwa Afrika mashariki na kati, bongo muvi iko juu sana tu. Angalia Africa Magic Swahili, asilimia kubwa ya muvi ni za tz. Nenda DRC, Malawi, Zambia, n.k. zinabamba sana.

In fact, nyota yetu kushindana kiutamaduni, ukiacha lugha ya kiswahili na uchawi/uganga ipo kwenye muvi/filamu za kibongo.

Sawa tuwakosoe kwani ni moja ya elimu ila pia tuwashauri ya kufanya wasonge mbele. Wakifanikiwa zaidi, ni heshima kwetu sote.

Mfano, kuna suala la wasanii wa filamu kuongeza zaidi elimu na ujuzi. Hili halikwepeki kwa walipofikia sasa.

Kingine, wanahitaji kuboresha vifaa vyao na uchukuaji wao wa picha. Ili wapate soko kubwa ndani na nje, ni lazima uwe wa kisasa kabisa na wenye mwafaka na kanuni hususa.

Zaidi zaidi, nawapa pongezi kwa walipofikia. Then kama kawaida, wafanye maboresho makubwa.
 
Tunapenda tuendelee ndio maana tunawasema Hata vitabu vya dini vinatuasa hivyo - Soma Mhubiri 7:5

Heri kusikia laumu ya wenye hekima, kuliko mtu kusifia wimbo wa wapumbavu.

Hatuwezi kuwa wasanii wote ila anayechagua kwenda huko atuletee best product. Jamani miaka zaidi ya 15 sasa tupo pale pale?
Mbalamwezi1
, hata kupanga viti na meza vionekane kama mandhari ya mahakama kunahitaji fair ground? Tubadilike bwana hata sisi walaji ifikie mahala tukatae bidhaa mbovu!

Umeona sasa!!ndo tatizo letu baadhi ya wabongo!kupenda kubemenda watoto,mtoto kazaliwa tu unataka umlishe maugali eti apate nguvu za miguu atembee!miaka 15 mtoto cjui ndo yuko form one bado ana akili za utotoutoto hawezi hata kujitegemea bado anahitaji malezi na muongozo zaidi!sasa miaka 15 fuatilia hata historia ya wale ambao wengi tunafikiri kwmba they are the best in film industry hlf uone walikuwa wapi!Tuwape changamoto wasanii wetu na si kuwaponda!
 
Kwenye music hakuna nchi inayoifikia tz afrika mashariki na kati..
 
Me sifuatilii sanaaa. Nipo busy sana na kujenga uchumi wangu.

Ila nachukia sana watu wasiopenda vya kwao. Chariry begins at home.

Hata maandiko yanasema asiyependa wa kwao ni sawa na ibilisi tu..
 
Unachosema ni kweli,mimi kuanzia filamu z maehemu Kanumba na hizi za sasa hivi za akina Ray,na wengineo zinakosa uhalisia,mtu anaigiza kulia lakini shavu lina tabasamu,majumba ya kukodi wanayoigizia kujifananisha na wanaijeria sio hali halisi ya majority ya watanzania,ni nadra sana kuona muigizaji kachukua scene ya uswazi,au nyumba ya kupanga uswahilini,mimi nazimia kipindi cha mizengwe tu cha akina ------
k
 
unapotazama chanel za kenya hadi raha.
Vihoja mahakamani
papa shilandula
ngumbalu skool
almasi
naswa
vitimbwi
insekta mwala
machachali
je huu ni uungwana
k24 saamoja
makala ya mungu wetu

citizen nipashe "ukweli wa mambo"
 
Me hizi filamu za kibongo zinachonikera ni kukosa uhalisia wa maisha ya kawaida ya mtanzania. Kila filamu wanaigiza wako katika majumba ya kifahari wakati watanzania wengi maisha yao ni ya kawaida tu. Nyumba za kupanga na kuishi uswahilin.
 
Offside ntv
hik wabongo wamejarbu kuiga kanjanja time channel 10 bt wanazngua tu hawana ubunfu wwte na n waoga wenzao wanaonyesha mpk vtuko vya viongoz wa serikalin
 
tatizo mahindi waliyotumia yalikuwa na dawa...ile ya kutunzia mahindi dats de problem
 

Mjasiria
mdogo wangu, usidhani tunawachukia wasanii wa Bongo, la! twawapenda sana ila tunataka watupe kazi bora, Ninachoongelea hapa ni miaka hii - 2010+ siyo miaka 10 iliyopita, we cant move ahead bila kujitoa kasoro na kuyasema mapungufu ili tujirekebishe - call a spade a spade! Watu wanaosifia kama wewe ndio mnaofanya tubaki pale pale miaka nenda rudi. Tusisifie uwezo ambao hatuna.
Ni bahati mbaya kuwa hata wateja (watazamaji) wengi bongo uwezo wa uchambuzi wa kujua kazi bora hawana! Nilitangulia kusema "kama ulipitia somo la Fasihi" - hasa sanaa za maonyesho utakubali kuwa tuko nyuma. Rejea post mdogo wangu!
Kaka kumbe bado hujanisoma. Sisemi kwamba tusitoe kasoro ila kuna tabia ya kuponda sana utanzania wetu ambayo imeota mizizi ndiyo mimi inayonikera.

Hivi unadhani unaweza kumsahihisha mwanao kwa kumwambia mburula wewe huwezi kufanikiwa kamwe ona unavyopata alama za kipumbavu darasani. Hapo utakuwa umemsaidia huyo mtoto???!!! Sasa na sisi wabongo japo sio wote ndio utaratibu wetu wa kukosoa na kusahihisha.
 
Jamani, huwa nashangaa sana wasanii wa Tanzania wakitokwa na povu kulaumu kuwa kazi zao zinadhulumiwa, huwa najiuliza kazi zipi? Ni kazi kweli au upuuzi? Labda huko kwenye miziki hatujambo - huko nawapa pongezi zao.

Lakini, ukiangalia filamu, tamthilia au vichekesho(comedy) za Kitanzania, hasa kama ulipitia lile somo la fasihi utaishia kukasirika na wala si kuburudika.
Nimejitahidi kuangalia filamu nyingi za Tanzania nimeishia kujawa na hasira tu, ukirejea fasihi unaona kabisa hakuna uhalisia; Kuanzia mandari (scenes) hadi uwasilishaji (act) haziwasilishi dhana kamili iliyokusudiwa katika uasili na uhalisia wake (sense of reality).

Mimi nimeshindwa kutazama filamu hata moja ya kibongo mwanzo - mwisho kwa sababu hizi, na siwazii kununua CD/mkanda wowote wa kibongo kwa sababu ya viwango kuwa chini sana!

Ebu angalia comedy hii kutoka Kenya utaelewa nina maana gani. Kuanzia mandari ya kimahakama, namna uendeshaji wa kesi unavyofuata uhalisia, hisia za wasanii, uhalisia wa kujieleza, no foolish exagerations, n.k. - na bado wanakuchekesha!
Hongera Wakenya kwa Comedy maridhawa.Wasanii wa kibongo amkeni acheni kazi za kitoto!!





Ni kweli ulichosema lakini liangalie pia jambo hili kwa upande mwingine ukiacha ubovu WA wasanii.

Na basata wanabana sana wanawachugulia mahudhui ya michezo.

Kwa mfano ukiigiza visa vinavyohusu shekh au mchungaji unaambiwa unakashifu dini wanazuia.

Ukiigiza mambo ya mashoga utaambiwa unaaribu jamii.

Kwa iyo na ukiritimba upon pia!.
 
Last edited by a moderator:
hata makala za kiuchunguzi kama JICHO PEVU ya Mohamedi Ally hatuna hovyo kabisa..
 
Back
Top Bottom