Hongera kaka Makonda, mateja wa Dar sasa wanaisoma namba

Babu Kijiwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
4,775
2,000
Kwakweli jiji lilikuwa limefikia pabaya sana, kila kona mateja, vituo vya mabasi ndo usiseme, ila baada ya vita ya jemedari Makonda.

Sasa jiji limeanza kuwa safi na salama kwa upande huo, pole kwa kupewa jina la Bashite, nakusihi ulipokee kama watang'ang'ania kukuita lakini endelea kukaza kwenye vita dhidi ya madawa ya kulevya.

Hata kama dunia imeshindwa, naamini sisi tutashinda.

Hongera sana kaka.
 

DomieLe

JF-Expert Member
Sep 1, 2016
809
1,000
Bila unafiki, Paul Makonda amefanya vitu ambavyo vinagusa jamii. Tumezoea wakuu wa mikoa wakiwa busy na kufungua na kufunga mikutano, wakihudhuria sherea na kutoa light statements, na wakifanya cha ajabu sana kushiriki kwenye utatuzi wa migogoro defensively. Makonda has changed this traditional way of leadership, he has changed from reactive to proactive approach. He is a daring person, with vision!. Tumpe nafasi
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,135
2,000
Unaishi Dar es salaam ya wapi isiyo na mateja wala uchafu?! Au unaishi city center tena city center ya Posta kuelekea Magogoni?!

Btw, vipi mrejesho wa wale wafanyabiashara wakubwa na wengine wanaojihusisha na za kulevya?
-Yusuf Manji
-Freeman Mbowe
-Idd Azzan
-Mkurugenzi wa NAS
-Wamiliki wa Slipway
-Mfanyakazi wa BP
-Swahiba wake wa hivi sasa DJ Majizo

Hakika ni walevi tu ndio wanaweza kuamini drama za Makonda kwenye isuse mzima ya dawa za kulevya

NB: Haitwi Bashite kwa sababu ya drama zake kuhusu Mihadarati bali kwa sababu ndio jina lake... Daudi Albert Bashite!!

Hii thread hapa chini ni ya December 2015 hata kabla hajawa RC let alone kuanzisha hizo drama za mihadarati....
Nilikutana naye Koromije Misungwi Mwanza miaka ya 2000 enzi hizo akiitwa DAUDI Bashite. Sifahamu kivipi anaitwa Paul Makonda. Namfahamu in and out
Kwa mara ya kwanza JF, Member kutoka Kolomije ndie alifichua jina halali la the so called Paul Makonda na hiyo ilikuwa ni December 2015.

So, porojo eti kwamba ameanza kuitwa Bashite baada ya "kuwaripua wauza unga" ni porojo zinazoaminiwa na walevi wa drama zake kama zile drama za kuleta meli ya Wachina wakati Wachina wameanza kuja Dar na ile meli wakati Daudi bado yupo kwao Kolomije!!!
 

Emmadogo

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
4,136
2,000
Mbona kitaani wamejaa wananesa kama kawa. Au unaishi darusalaam sio dar es salaam
 

kinyama nje

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
1,731
2,000
Kwakweli jiji lilikuwa limefikia pabaya sana, kila kona mateja, vituo vya mabasi ndo usiseme, ila baada ya vita ya jemedari Makonda.

Sasa jiji limeanza kuwa safi na salama kwa upande huo, pole kwa kupewa jina la Bashite, nakusihi ulipokee kama watang'ang'ania kukuita lakini endelea kukaza kwenye vita dhidi ya madawa ya kulevya.

Hata kama dunia imeshindwa, naamini sisi tutashinda.

Hongera sana kaka.
bado wapo sana tu.jana nilikua napiga story na teja huyu kwao mambo safi hajachoka sana. Amesha ingiza madogo wawili kwenye janga hilo ye anaita kuwatoa kwenye reli siku mbili tu zinatosha machimbo yote wanayatafuta wenyewe
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom