Hongera JWTZ

Hongera JWTZ

Huwa nikiwaangalia askari polisi wetu kisha nikawatizama JWTZ huwa najiuliza kama kweli haya majeshi yote yapo kwa ajiri ya watanzania kweli ama labda ni kama mbingu na ardhi,JWTZ mmesimamia nidhamu yenu na kweli Mara zote mnaombewa mema sana na wananchi wa kitanzania kwa kuwajari na kuwasaidia bila karaha na ubaguzi kama wenzenu wa Kova
 
jwtz linafanya kazi nzuri ya kulinda wananchi wake,ila usiharbu kazi yao wanakuua kabisa
 
Uzalendo wao unatokana na uongozi uliotukuka walio nao,nasikia kiongozi wao kaomba kustaafu baada ya kupangiwa mikakati ya kipuuzi kufuatia uchaguzi mkuu ujao itakayopelekea umwagaji wa damu.

Are you serious mkuu???
 
Huwa nikiwaangalia askari polisi wetu kisha nikawatizama JWTZ huwa najiuliza kama kweli haya majeshi yote yapo kwa ajiri ya watanzania kweli ama labda ni kama mbingu na ardhi,JWTZ mmesimamia nidhamu yenu na kweli Mara zote mnaombewa mema sana na wananchi wa kitanzania kwa kuwajari na kuwasaidia bila karaha na ubaguzi kama wenzenu wa Kova

Lakini hapo nawe unakosea, majukumu ya jwtz ni tofauti na polisi, hawa polisi shughuri zao za kila siku ni za kukutana na raia, ndio maana ni raisi kuona mabaya yao, ni kutokana na majukumu yao. Hata hao unaowasifia tena wao ndio wanyama kweli kuliko hata hawa polisi, wa kova, waulize watu wa mtwara, na waathirika wa operation tokomeza.
 
Ukiingia kwenye kumi na nane zao utajaza popa maji kwa kisoda.......
 
Uzalendo wao unatokana na uongozi uliotukuka walio nao,nasikia kiongozi wao kaomba kustaafu baada ya kupangiwa mikakati ya kipuuzi kufuatia uchaguzi mkuu ujao itakayopelekea umwagaji wa damu.
Una uhakika na usemacho?

Kumbuka tetesi zinabainisha kuwa tayari mkulu keshaisaini ile sheria inayolalamikiwa sana na wananchi ya cyber crimes.

Usije wewe ukawa mhanga wa kwanza kupelekwa Segerea kwa comments zako hizo.
 
Jeshi lolote lile Duniani
(People Defence Forces), jukumu lao kubwa ni kutoa msaada usio na malipo. Msaada wowote ule unaohitajika, na ndio maana ndani ya majeshi hayo, kuna wataalamu wa kila fani, yaani ni Serikali tosha kabisa. Kwa kufanya hilo uliloliona na mengine unayoyasikia, ndiyo moja ya majukumu yao, na bahati nzuri naamini walifikishwa ktk vituo vyao, ila katikati hapo dereva angepewa signal ama alarm ya kutakiwa mahala haraka, angewashusha wote na kuifuata amri iliyotolewa / aliyopewa. Kama kuna wale waliokwisha panda ndege za kijeshi, miaka ya awali kidogo, watalithibitisha hili, unaweza tokea Ruvuma kuelekea Mbeya, root ikabadilika na kujikuta mpo tabora, kama huna pesa ya ziada, ni kuwasubiria tu hadi wamalize yao
 
Ni rahisi zaidi kuona meme yao kuliko mabaya kulingana na nature ya kazi zao tofauti na Polisi au mahakama japo unaweza kukataa kwenye hilo.Ulinzi wa ndani ni mgumu zaidi kuliko nje mf;rushwa mwanajeshi ataipata wapi yeye he is not dealing with people kama ni uaminifu hata Magereza ni waaminifu
 
Kama ni hilo hata Magereza ni waaminifu maana hawali rushwa
 
Leo jioni majira ya saa kumi na moja au kumi na mbili wakati mvua inanyesha pale Mwenge kituo cha kwenda Tegeta, basi la JWTZ lilisimama na kuwapa lift watu waliokuwa wanaelekea njia yao: Lugalo na Kawe. Wamenigusa sana kwa moyo huo wa kizalendo na mapenzi kwa wananchi wenzao. KWELI NYIE NI WALINZI WETU....... MBARIKIWE SAAAANA kwa sababu kitendo mlichofanya magari ya serikali (yaliyonunuliwa kwa kodi zetu) hayawezi kufanya hivyo!

Umewapa sifa watu wanaostahili sifa kwa kweli. Kama kuna taasisi katika taifa hili ambayo najivunia sana ni JWTZ. Ingelikuwa ni nguo ningeivaa kila siku watu wajue ni nguo yangu.
 
Kuna jamaa mmoja nae alijishoboa kuomba lifti kwa wajeda mbona alijuta kwanza walipiliza nae hadi kambini halafu alivyo fika kule alianza kupewa mateso walimpa lundo la kombati na wakamjazia maji kwenye ndude na miche miwili ya sabuni alafu wakamwambia amalize kufua hizo kombati zote
 
Back
Top Bottom