Hongera Job Ndugai

Hongera Job Ndugai

ccm huwa siwaamini kabisa , wana hila mbaya sana hawa watu. Ngoja tutaona mwisho wa hii movie.

Tushikamane kama taifa kuwasihi viongozi wa ccm kurudisha imani kwa wanachi maana huku mtaani hali haiko shwari.
 
Mi nilitarajia baada ya UKAWA kuondoka bungeni ingewachukua CCM less than an hour kupitisha rasimu yao. As long as wana rasimu yao tayari na wanakubaliana kwa 100% kuna haja gani ya kujadili tena

Wanafiki wanapiga pesa
 
Jamaa kamuua kusheherekea pasaka kiroho saaaaafi kabisa.CCM wakiwa kwenye vikao huwa hawashauliki hata kwa leki.Ndiyo maana kaamua kwenda kuwashauri kupitia media, kama wana maskio wamesikia.
 
Serekali 3 zinawatesa sana wabunge wengine wanasema hayo ni mawazo ya Waryoba wengine pamoja na Waryoba wanasema kuwa hayo ni maoni ya wananchi.Ndani ya bunge hilohilo wapo wabunge waliolishana yamini kuwa wahakikishe rasimu ya katiba haipenyi ikiwa na maoni ya serekali 3.Wapo wanaopambana kuhakikisha rasimu ya katiba inapenya bungeni ikiwa na maoni ya serekali3 kwa vile wanaamini kuwa hayo ndiyo maoni ya wananchi.Katika hili wabunge walikuwa hawana sababu ya kurushiana maneno machafu kuimbiana tarabu kuongea maneno ya mipashomipasho kama watoto kitu ambacho kimewafanya wabunge wawe kituko mbele ya jamii.Kitu walichopaswa kukifanya kwa vile kuna wanaoamini kuwa serekali 3 ni mawazo ya Waryoba,Waryoba na baadhi ya wabunge wanasema kuwa hayo maoni ya serekali 3 yametoka kwa wananchi kwa vile rasimu inatakiwa irudi kwa wananchi ikapigiwe kura kuliko kuendelea kurumbana wanatakiwa waiache rasimu ya katiba ikiwa na maoni ya serekali3 ili mwananchi ambaye inaonekana kupakaziwa maoni ambayo hakuyatoa akayakatae hayo maoni kwa njia ya kura.

Kweli kabisa mkuu hiyo rasimu ingerudi kwa wananchi waipigie kura ni simple like that,,,Jaji Warioba kafanya kazi yake kwa uweledi mkubwa na hakutaka kuleta tikadi ya chama ikiwa na yeye ni CCM
 
Nami niungane pamoja nanyi wanajamvi jf kumpongeza Job Ndugai kwa sauti yake kuu hakika itarudisha matumaini kwa ccm walau kijitafakari upya na kuachana na misimamo isiyo na tija kwa Taifa letu.

Warioba ni ccm mkongwe lakini aliamua kuchukuwa maoni kama yalivyo na kuyaweka hadharani kwa nini viongozi wengine wa chama wampinge.ccm tuitakayo ni ile ya warioba na wala siyo ya Nape mnauye.

Wapi Willison Mkama jamani mbona uko makini sana au umemezwa na mafisadi? Mkama funguka usikae kimya wewe ni jembe Sema utasikika.
 
kwani nyinyi hamjue ukigeugeu wa viongozi wa ccm kinachofatia hapo ni kusema kuwa hamkumwelewa,kama sasa walivyofanya
 
Saa nyingine huwa siwaelewi wanasiasa, hasa wa CCM. Ni vigeu geu wa kufa mtu!. Wakati wa maoni weengi walitaka serikali tatu, leo wakabadilika wanataka mbili! Wakaja na rasmu yao, mara wakatishia UKAWA, hivi sasa ndo wanakumbuka kuwa bila MARIDHIANO hakuna katiba! Wanastaajabisha kweli kweli.!
 
Mm nampongeza angalau,,,amesema ukweli na wengi wamesikia hata km kwakuchelewa cyo mbya jamani
 
Aliyosema Ndugai ndio hali halisi ya kila ccm na wote wanajuwa vyema walivyouteka mchakato wa katiba bungeni lakin katika ccm kuna kuna kitu 1 kibaya sana wawo hawawezi kufanya kitu au kuamua kitu kwa matakwa binafsi ya mtu siku zote hufuata misimamo ya mtu au kundi la watu hata uongozi wa juu, naamini kabisa ndugai amefkiri na akapata maumivu na siyo yeye tu wapo wengi ila ni ngumu mtu kwenda kwenye katika media akaeleza ya moyoni au hata pale bungeni ni hisia ambazo baadae hufa ndani ya nyoyo zao. Tuombe Mungu sana wazidi kupata hii Ilhamu ili sisi tusio na vyama tuje tufaidike na hii katiba pamoja na generation yetu ijayo
 
Kinachonishangaza na hao CCM ni kwamba wana mashaka na takwimu za Judge Warioba, that is fine. Lakini kwa busara ya kawaida kama wana maahaka na takwimu, wangemuita Judge Warioba kwenye BMK ili kuzitolea ufafanuzi. Na kama angeshindwa kuwaondolea mashaka basi ndio wangekuwa na haki ya kuziponda. Lakini CCM hawataki kufanya hivyo! Guess why? Kuhusu misimamo ya makundi CCM v UKAWA, mimi ningeshauri kama CCM msimamo wao ni serikali 2 na UKAWA msimamo wao ni serikali 3, basi wengekubaliana NEUTRAL MUUNDO yaani SERIKALI 1. Hiyo ndiyo ingekuwa WIN WIN SITUATION for both CCM AND UKAWA
ukizungumzia serikali moja kwa wenzetu wa Zanzibar ni bora muungano ufe maana wazanzibar wote wanachotaka vyovyote itakavyokuwa seikali yao iwepo na nchi yao iwepo,kwa wazanzibari serikali mbili au tatu kwao sio tija ili mradi kuwe na serikali ya zanzibar hata serikali zikiwa kumi ili mradi kati ya hizo kumi kuna ya zanzibar tofauti na watanganyika ambao baadhi yetu hatuitaki serikali ya tanganyika yetu,wengi wa tanganyika ni mbumbumbu,hasa hasa wabunge wa ccm
 
Tuendelee kuchangia hasa tujikite kwenye nini kifanyike ili kupata katiba mpya.
 
Mi nilitarajia baada ya UKAWA kuondoka bungeni ingewachukua CCM less than an hour kupitisha rasimu yao. As long as wana rasimu yao tayari na wanakubaliana kwa 100% kuna haja gani ya kujadili tena...

Technically analilia posho yake maana vikao vya Bunge vitakuwa vichache ...
 
Nani jasiri kama mh. Ndugai ndani ya ccm athubutu kusimama mbele ya media aeleze yaliyondani ya moyo wake ambayo ni ya kweli kweli tupu bila kujali misimamo mikali ya wajumbe na viongozi wengine wakuu kama yeye au hata zaidi yake! we need brave leaders who dare and take risks to save the nation in critical time kama tulipo sasa! wapo wanaojuwa njia lakini ni waoga wa kuthubutu! ukweli tuuseme! huwezi kujadili rasimu fake! vinginevyo tumchukulie hatua za kisheria judge Warioba kwa kuchakachua maoni yetu! na kama hakuchakachua basi wajumbe wayajadili kama yalivyo! kama kuna mahali wanamashaka napo, Walioba hajafa wamwite apatolee maelezo! Lengo ni katiba nzuri! misimamo kwa sasa haijengi hata kidogo! nadhani pande zote zimemuelewa Hon. Ndugai! yafuate matendo! waache malumbano! waheshimu maoni yake!
 
Mnyonge mnyongeni na haki yake apewe, Kaongea mawazo yake na kimsingi amekuwa na mlengo wa utaifa zaidi na hajaongea kichama. Apongezwe kwa uthubutu kwa vile ki kawaida mwanaCCM yeyote kuyatamka hayo aloyatamka Mh Job si rahisi kihivyo. Kiukweli kajitoa mhanga. Kiukweli kilichotufikisha hapa ni CCM kuwa na msimamo wa kupitisha wanachotaka wao. Hii ni hatari kubwa sana kwa wananchi kama tutaandaliwa katiba ya nchi na mtawala! Hata siku moja hawatatengeneza katiba inayomhusu mwananchi wao watatengeneza inayolalia upande wao! Sasa kama Mh Job ameliona hili anasitahili kupongezwa na kama ameamua kujitoa mhanga aongee na mwenyekiti wa Baraza la katiba ambaye alijiapiza kuwa atawashughulikia wale wanaotaka serkali tatu.
 
Sababu yoyote iliyofanya akasema hayo sio muhimi. Muhimu ni hayo mawazo aliyotoa. Sasa tunataraji mwanzo mpya. Ukawa kurudi, mijadala yenye upendo, hoja kutoegemea vyama, maamuzi ya pamoja, katiba inayokubalika kwa wote, mawazo ya wachache kupewa nafasi. Nk
 
Back
Top Bottom