Hongera intelejensia ya CCM kumuibua game changer, Paul Christian Makonda (PCM)

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
8,538
17,473
Katika kipindi ambacho wapiga Dili wapo kileleni mwa zamu Yao baada ya kubanwa takribani miaka SITA ya mwenda zake,kelele na vilio vinasikika Kila Kona nchini kwa ubadhirifu na upigaji unaoendelea!


Ilihitajika nguvu mpya chanya Ili kuenzi zama za awamu ya Tano kurudisha chama kwenye msitari ndipo chama kilipomuibua mthubutu asieogooa lolote na si mwingine Bali ni huyu!

Hakuna ambaye anaweza kuleta nguvu ya chama katika kushughulika na mabwanyenye yaliyoanza kukita mizizi yao ndani ya chama!

Tutarajie falsafa mpya ndani ya chama ya kiutendaji na uwajibikaji wa pamoja Ili kufikia malengo,ninaomba chama kimpe mamlaka yote huyu game changer na wasimwekee spidi gavana Ili ale nao mbele kwa mbele wabadhirifu wote hata wale wasemao CCM Ina wenyewe watambue CCM Haina mwenyewe!

Nikupongeze,nakuunga mkono kwa uamuzi huu ulioufanya ewe mheshimiwa Rais samiah nakupongeza kwa kutaka kurudisha chama kwenye msitari baada ya dalili za wazi za kukiuka misingi kujionesha!

Mungu ibariki Tanzania yetu!
 
Back
Top Bottom