Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,717
- 41,495
Mtu yeyote anaweza kuserma lolote dhidi ya Dr. Slaa, lakini nina hakika, hakuna mwenye akili na utimamu wa akili anayeweza kuhoji super intelligence ya Dr. Slaa, ukweli wa nafsi yake, ujasiri na katika kusimamia anachokiamini. Siyo mtu wa kuyumba katika anachokiamini kuwa ni sahihi au siyo sahihi.
Ni ukweli wa sifa hizi, ndio uliomfanya kuonfoka CHADEMA licha ya kuwa alikuwa ametumia muda wake mwingi kuijenga CHADEMA. Dr. Slaa aliamini kuwa Lowasa alikuwa fisadi. Alilisema hilo wazi. Na hata CHADEMA walipoamua kumpokea Lowasa, yeye aliendelea kusimama katika alichokiamini.
Leo, Dr. Slaa, baada ya uchafu uliofanywa na Serikali na bunge batili kuhusiana na kuzigawa Bandari zote za Tanganyika kwa Mwarabu, ametoa kauli iliyonyoka, iliyo dhahiri na isiyopepesa. Amesema wazi kuwa:
1) Mkataba wa bandari ni mkataba batili kwa sababu unakiuka katiba.
2) Mbarawa na wenzake, wameuza nchi.
3) Hofu za watanganyika kuwa wazanzibari wanauza rasilimali za Tanganyika, ni hofu za halali.
4) Mauzo ya bandari za Tanganyika yalianza tangu mwakajana kwa siri, na kuna mikataba mingi imekwishasainiwa kabla ya huu wa mwisho uliopelekwa bungeni.
5) Mkataba huu wa hovyo wa bandari, umepelekwa bungeni kwa sababu unahusisha kubadilisha sheria za nchi ili matakwa ya mwarabu yaweze kutekelezeka.
6) Mwenye haki na rasilimali za nchi ni wananchi. Rais ni msimamizi tu, siyo mwenye mali.
7) Serikali inataja tu vile vifungu vizuri vya mkataba, haivitaji vile vifungu vibaya vinavyohatarisha sovereignity ya nchi.
8) Mkataba hauna muda, ni wa kudumu. Huku ni kuuza nchi.
9) Katiba UAE hairuhusu Dubai kuingia mikataba ya kimataifa, lakini kwenye hili, Dubai ambayo ni mji tu imesaini mkataba na nchi.
10) Bunge ni batili kwa sababu mle ndani kuna wabunge 28, akiwemo Waziri Mkuu, ambao mahakama ilikwishatamka kuwa ni wabunge batili, ambao wanatakiwa kurudisha hata mishahara waliyokwishalipwa.
11) Raia yeyote ana haki ya kufungua kesi dhidi ya Bunge na Serikali kwa kukiuka katiba kuhusiana na huu mkataba unaokiuka katiba na sheria za nchi.
12) Maelezo ya Mbarawa, kama yeye Dr. Slaa angekuwa mwalimu wa sheria wa Mbarawa, angempa 0%.