Hongera dar-es-salaam young africans

Right eye

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
716
1,214
Twende.
Mmeonyesha utofauti na ukomavu mkubwa,Kila jicho lililopata nafasi ya kutazama mechi hii ya Dar es salaam Young Africans na waarabu litakiri hili nalokwenda kulisema.

Kiwango cha timu kupambana na kutafuta matokeo chanya uwanjani ni kikubwa sana.

Utimamu wa miili na akili za wachezaji uwanjani ni wa hari ya juu sana.

Hongera kwa uongozi wa Dar es salaam Young Africans kwa kuleta benchi bora la ufundi likiongozwa na Prof Nabi na wachezaji imara na wenye viwango vya kimataifa ambao wanao uwezo wa kupambana kwenye kila kiwanja na kupata matokeo,Hii ndio inafanya Dar es salaam Young Africans kujitofautisha na timu nyingine za ukanda huu wa CECAFA.

Rai yangu kwa uongozi wa Dar es salaam Young Africans wakiongozwa na Rais Eng Hersi kwasasa timu imeshajitafuta na kujipata hivyo tunaomba usiruhusu mchezaji yoyote ambae yupo kwenye mipango ya mwalimu atoke nje ya timu bali kwasasa tufanye maingizo mapya machache kwenye nafasi ambazo zitapendekezwa na mwalimu kwaajiri ya kuijenga Dar es salaam Young Africans kua imara zaidi na tishio kwa msimu ujao wa mashindano ya Africa.
Tamati.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom