Hongera Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera Chadema

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nickname, Mar 20, 2011.

 1. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2011
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Uchaguzi mkuu wa Rais,wabunge na madiwani nchini Tanzania ulifanyika mwezi Oktoba,2010.Uchaguzi ulikwisha na kila chama kiliambulia chake.

  Pamoja na CDM kulalamika kuwa matokeo ya Urais yalipikwa na kutotambua njia zilizotumika kumweka Rais madarakani lakini viongozi wa Chadema kwa busara hawakutumia nguvu ya umma kupinga matokeo ya Urais.Kwa hili nawapongeza sana.

  Maandamano ya kupinga uchaguzi wa meya wa Arusha yalifanyika,nasikitika kwa vifo vya watu watatu kulikosababishwa na Polisi kutumia nguvu kupita kiasi.

  Nikirudi kwenye mada kuu ni hivi baada ya uchaguzi mkuu kumalizika kumejitokeza kampeni zilizofanywa na CDM katika mikoa ya kanda ya ziwa,kampeni hizi zimekuwa zikianza kwa maandamano ya AMANI na baadae mikutano ya hadhara.Nashukuru kuwa lengo ni kupinga malipo kwa DOWANS,kuwatetea watanzania kuwanusuru na maisha magumu yaliyopo sasa.

  CCM wameogopa sana wakisema kuwa CDM inafanya uchochezi wa kutaka kuipindua serikali ya JK.CCM hawajui kuwa wanachokifanya Chadema ni kazi mojawapo ya chama cha upinzani ya kuikosoa serikali iliyo madarakani.Kulingana na matamko ya viongozi wa CDM,CCM walipaswa kujibu hoja.Kwa hili safi sana kwa kuwa baada ya viongozi wa Chadema kulalamikia upandaji bei wa vitu hususani sukari serikali ikaamua kushusha bei ya sukari toka sh.2000 mpaka sh 1700.

  Tumejionea nao CUF na NCCR baada ya kuipinga Chadema nao wameamua kufanya mikutano ya hadhara huku maudhui katika mikutano hiyo ikishahabiana na na kile kilichosemwa na Chadema.CUF wameanza mikutano yao katika mikoa ya Tanga,Mtwara,Lindi,Pemba,Unguja n.k huku NCCR wakifanya mikutano yao katika mkoa wa Kigoma.CCM wao wamekuwa wakifanya kampeni zao za kujibu mashambulizi ya Chadema kupitia vyombo vya habari hasa TBC1.

  Tunachoendelea kujionea ni kampeni za kuwatetea wananchi na kuona kuwa maisha ya wananchi yanaboreka.Uzuri wa kampeni hizi ni kuwa hazina muda maalum na hakuna uchakachuaji wa kura na matokeo yake ni kwa serikali kuboresha maisha ya wananchi kwa msukumo wa wapiga kampeni.HOngera kwa walioanzisha kampeni hizi.HOngera Chadema.Alamsiki
   
 2. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Nimekusoma mkuu...
   
 3. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mzee Mwinyi kakaa miaka 10 hakuyamaliza, Mzee Mkapa nae kakaa miaka 10 hakuyamaliza. Mie nimekaa miaka mitano hayakwisha na nitamaliza mitano hayataisha yote

  Hiyo inaonyesha jinsi gani raisi hatoshei
   
 4. M

  MZAWATA JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  CCM wajipange vizur sambamba na kutafuta watu wenye upeo wa mambo mbalimbali,nakin kwa busara za hii ni aibu kwao, wanajua dhahiri walipigwa chin,lakin kwa busara za Chadema waliamua yaishe lakin mwaka 2015 HATUTAKUBALIU TENAAAAAAAAAAAAAAAAA!
   
 5. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Dalili ya mvua ni mawingu; tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu CDM ndiyo inayoanzisha mjadala, CCM wanaishia kujibu mapigo. Kama hiyo siyo dalili ya CCM kufilisika kimawazo ni nini basi?
   
 6. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mtazamamo wangu ni kwamba, viongozi wenye upeo kwa ccm; ni wale wenye uwezo wa kupiga propaganda zaidi kuliko kutenda, na hii ni kwa sababu ccm inataka kuhakikisha inabaki kwenye madaraka milele, (ni haki yao). Ccm inazingatia hilo zaidi, ndio maana unapozuka mjadala juu ya utendaji wa wake, kwa ccm inatafsirika kama kitisho cha kunyang'anywa madaraka.

  Ninakubaliana na wewe kwamba ni lazima ccm iwe na timu yenye watu wenye lengo la kuboresha maisha ya mtanzania au angalau wanaoonekana kuwa na nia hiyo pamoja na kwamba wanakutana na vikwazo, vinginevyo itakuwa ngumu sana kwa ccm kurudisha heshima yake na imani ya watanzania kwake.

  Lakini pia ni mtazamamo wangu kuwa kwa sasa ccm ina muda mfupi sana kutimiza hilo, 2015 sio mbali sana.
   
Loading...