RC Sendiga, azindua kampeni "Mpe maua, atabasamu asome kifalme

John Walter

Member
Aug 14, 2017
64
62
IMG-20240126-WA0021.jpg
John Walter-Manyara
Kampeni Mpe Maua atabasamu asome kifalme imezinduliwa wilayani Simanjiro mkoani Manyara.

Kampeni hiyo inalenga kuboresha sekta ya Elimu mkoani humo ikiwa ni adhma ya serikali ya awamu ya sita kila mtoto apate elimu ambapo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameelekeza elimu ya awali mpaka kidato cha sita iwe bila malipo.

Akizungumza wakati akizindua kampeni hiyo, Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amesema kuwa kwa sasa shule nyingi bado zinakabiliwa na changamoto ya madawati, hivyo kupitia kampeni hiyo wataweza kushirikisha wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuweza kufanikisha zoezi hilo na kwa haraka.

"Nimewaita leo ili kuwaomba wadau na wazawa wote wa Mkoa wa Manyara kuja kuungana nasi kuwapa watoto tabasamu kwa kuwawezesha kusoma katika mazingira yanayovutia", amesema Mhe. Sendiga.

Matarajio ya kampeni hiyo ni kuhakikisha vinapatikana viti na meza 4,664 na madawati 28,336 ili kuweza kukidhi mahitaji ya mkoa kwa ujumla.

Aidha, Sendiga amesema katika kipindi cha uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hassan mkoa umepokea bilioni 91.4 katika sekta ya Elimu, ambazo zimetumika kutengeneza na kurekebisha miundombinu ya shule.

Wadau uchimbaji madini ya Tanzanite Kampuni ya FRANONE, wameunga mkono kampeni hiyo kwa kuchangia madawati 142.
 
Back
Top Bottom