Hongera Asia Mayaga kwa kulisemea hili la ukaguzi wa udhalilishaji kwenye migodi ya madini

Standards Person

JF-Expert Member
Apr 22, 2021
673
859
Imeibuliwa hoja bungeni kwamba watu wanakaguliwa huko Mirerani kwa kuvuliwa nguo. Wanalundikwa kwenye chumba kimoja watu wa rika tofauti wakiwa wamevuliwa nguo eti kisa ni ukaguzi wa madini ya tanzanite.

Akiongea kwa ukali na masikitiko mbunge wa viti Maalum Asia Mayaga amesema haivumiliki na asipopewa ufafanuzi wa kina na wakuridhisha kuelekea kulimaliza tatizo hilo anashika mshahara wa waziri.

Asia amesema hata akinamama wakiwa kwenye siku zao haijalishi wanavuliwatu nguo na kupekuliwa. Hii ni aibu na udhalilishaji mkubwa.

Hao wanaovua wenzao nguo nao wanavuliwa na nani wakiondoka ili kujiridhisha kwamba hawaondoki na madini?

Je, wao watakubali kuvuliwa nguo wakiwa kikundi cha watu wakaguliwe kisa madini? Hii ni aibu kubwa ndani ya nchi huru.

Baadae mh. Kasim Majaliwa Waziri Mkuu ametoa ufafanuzi kwa kusema serikali itanunua mashine za kisasa kwaajili ya ukaguzi. Huo ndio uthubutu kwenye maisha ya watu. Ila hao waliovua watu nguo mnawaachaje?

Hongereni wote mliowasemea wananchi wanaodhalilishwa kwakua mnajielewa.

Turudi kwa wale wasio wasemea wananchi wao. Tanga mjini kwamuda sasa hawana wa kuwasemea. Lakini Mungu atawasemea. Ninasema tena Mungu atasema tena kwa kishindo.

Mbunge wa Tanga ameamua kumsifia RC Martin Shigela kwa kusema eti wakuu wote wa mikoa waige mfano wake maana hagombani na wasaidizi wake.

Anamsifia kwani kuna tetesi kwamba RC huyo atapewa nafasi ya Bashiru Ally au Humphrey Polepole muda wowote. Ummy ni mtu wa fursa inaeleweka. Akapewe hiyo nafasi bwana Shigela na genge lake waiache Tanga iheme Ummy atarekebishwa.

RC gani unapelekwapelekwa na DED? Watu wameporwa viwanja vyao tena wengine wameshaingiza maji. Amemganda Ummy kwenye ziara wakati watu wanaulizana yule baba nae ni nani.

RC nzima kwa miaka mitano hata wananchi wa Tanga mjini hawakujui

Mbunge anajua shida ambayo watumishi wa halmashauri wanapata kupitia Mkurugenzi wake. Wale ambao wake zao waliwavutia hapo halmashauri baadhi yao wameanzishiwa mizengwe na kufutwa kazi.

Wameachiwa wake za watu hapo wanajinafasi. Wengine wametenganishwa kabisa na familia zao. Haya utayakuta Tanga na hata wakuu wa taasisi wameiga kuchukua watu wa chini yao.

Anayekataa kuiba na mkurugenzi anawekwa ndani. Akienda takukuru wanaambiwa muwekeni ndani ili asirudi tena. Ummy anajua tena anawasifia eti wanapendana.

Kwanini wasipendane wakati wanakula pamoja?

Mh.Rais awaonee huruma watu wa Tanga. Pametakaa ubadhirifu na ngono. Takukuru wanachangia kwa kiasi kikubwa kwani wamenunuliwa na Mkurugenzi wa halmashauri. Anajua kutuliza mtu mwenye kiu na njaa.

Hongereni nyie wenye wa kuwasemea,Tanga hawana wa kuwasemea bali yupo wa kumsifia RC.
 
Yaani Ummy bora Lusinde mara elfu moja. Nitampinga hadi awe kinyume na hao madhulumati.
Ila napata faraja,hatadumu Tamisemi arudishwe wizara yake akasimamie uzibuaji wa chemba. Ninasema hatadumu Tamisemi, Mungu atamvaa muda kidogo hivi
 
Huko tanga muda mwingine hamnaga kazi za kufanya.majungu kila wakati.sijajua hata vipaumbele vyenu vya kuwaletea maendeleo ni vipi
 
Shigela amedumu Tanga kwa vile anajua kuishi na wambea, Tanga ni ngozi ya tembo kuishi pale mpaka uwe na akili ya shoka
 
Mkuu umeleta mada nzuri sana,ingawa yangu iko nje kudogo,lakini ni kuhusu huku kuvuliwa nguo kwa kinachoitwa ukaguzi.Hata magerezani waangalie unskuta mtu ana kesi ya ndoa anapelekwa gerezani kwa kukosa dhamana akufika huko anavuliwa nguo na kuambiwa anainamishe matako.Huu pia ni udhalilishaji sana.
 
Mkuu umeleta mada nzuri sana,ingawa yangu iko nje kudogo,lakini ni kuhusu huku kuvuliwa nguo kwa kinachoitwa ukaguzi.Hata magerezani waangalie unskuta mtu ana kesi ya ndoa anapelekwa gerezani kwa kukosa dhamana akufika huko anavuliwa nguo na kuambiwa anainamishe matako.Huu pia ni udhalilishaji sana.
Watu wanaonewa sema hawana wa kuwasemea.
Pakusemea nikwenye majukwaa huru kama hapa.
Kwa mkurugenzi wa Tanga akikujua unasema mabaya yake anakutumia watu utishiwe maisha,ukifika polisi au takukuru ukimtajatu mkurugenzi unaambiwa tutalifanyia kazi. Hapo ndio imetoka hiyo.
Watu hao Ummy ndio anawapongeza Ila wataondoka muda sio mrefu
 
Mkuu umeleta mada nzuri sana,ingawa yangu iko nje kudogo,lakini ni kuhusu huku kuvuliwa nguo kwa kinachoitwa ukaguzi.Hata magerezani waangalie unskuta mtu ana kesi ya ndoa anapelekwa gerezani kwa kukosa dhamana akufika huko anavuliwa nguo na kuambiwa anainamishe matako.Huu pia ni udhalilishaji sana.
Hatari na nusu mkuu. Mungu atupiganie
 
Back
Top Bottom