Hawa jamaa kwawatu wanaofanya biashara za China tunawajua sana. Ukienda huko wanakwambia watakuletea mzigo wako na wanakuchaji kwa ukubwa wa mzigo ghara ambayo ni ndogo kidogo ya watu wengine wanaosafirisha mizigo kutoka china. Tofauti yao na wengine ni kwamba wengine ukifika unaonyeshwa umelipia mzigo wako ushuru shilingi ngapi na unapewa makaratasi yako kama ukikamwata njiani na polisi au watu wa idara ya forodha.
Sasa hawa jamaa HSC wakikusafirishia mzigo wakifikisha Dar wanakutolea kabisa lakini HAWAKUPI KARATASI YA AINA YOYOTE! Ukiuliza karatasi unaambiwa tulikubaliana hakuna karatasi. Ukiomba wakupe hata kirisiti cha kwao au karatasi yoyote yanjiani kama delivery note ili kusaidia kama mtu ukiulizwa njiani hawakupi. Ndio maana wafanyabiashara wengi wa Mwanza na Arusha wanaosafirisha mizigo kutoka China wanashindwa kuwatumia kwasababu wamekuwa wakisumbuliwa sana njiani na HSC hawasaidii kitu ukikamatwa maana wanasema hawakujui na hawajui mzigo umeutoa wapi. Yaani wakati wanapokea mzigo China wanaongea vizuri sana na watakwambia usiwe na wasiwasi wowote lakini wakishakukabidhi mzigo wako Tanzania ukakamatwa nao huko nje ukawarudia kuomba msaada watakavyokujeuka na matusi hutaamini hao ndio watu uliokuwa ukicheka nao jana.
Mimi naongea kwa machungu maana nimefanya nao kazi sana na nazijua ofisi zao pale Guangzhou na vitu walivyonifanyia hapa nahasara niliyoipata vitu vyangu vilipokamatwa siwezi kuwasamehe maana niliwalipa kodi zote za serekali na gharama ya kusafirisha kumbe ile kodi hawakulipa ndio wanaitumia kununulia mizigo yao.
Usione wanafungua Maduka mengi ni kwamba wanatumia kodi za wafanyabiashara wadogowadogo wanaosafirisha mizigo kutoka china na zile kodi ambazo hawa wafanyabiashara wangezilipa serekalini wao ndio wananunulia mizigo ya maduka yao.
Hapo nimewafafanulia sehemu moja tu ya biashara yao. Hakuna Polisi, Mtumishi wa idara ya Forodha na TRA kwa ujumla anayeweza kuwasogelea maana watatukanwa na kesho yake wanawasimamaisha kazi au wanawabadili ofisi. Kama ni majungu nendeni Customs Longroom muulizie Manager wa FAST TEAM ambayo ndio inashughulika na kukamata macontena ambayo hayakulipiwa ushuru au yaliyolipiwa kidogo Mr Kahise ni kwanini aliondolewa. Alipewa order yakuachia kontena alilokamata na alipokataa na kusisitiza EIDHA KONTENA LILIPIWE AU MIMI NITOLEWE TRA alikuwa amewekwa kwenye load speaker na kesho yake akapewa barua ya kushushwa cheo na kuamishwa idara!
Hiyo ilikuwa fundisho tosha kwa maofisa wengine wa idara ya forodha baada yakuona bosi wao kilichompata. Sasahivi TRA wakikusumbua ukiwaambia ni mzigo wa HSC tu unapita bila wasiwasi ila wasumbufu ni hawa wahuku nje barabarani ambao hawawajui vizuri.
Mimi sina shaka ya hata chembe kwamba familia ya mkuu wa nchi inahusika maana wao wenyewe wanakwambia waziwazi wakati wanapokupa guarantee ya kwamba mzigo wako utatoka bila wasiwasi na bila gharama yoyote ya storage kwasababu Rais anasimamia mizigo yao na kwamba mtu akiwasumbua wanachukulia hatua mara moja!
Tatizo ni Biashara ikishaingia 'wait haus'....wenye usukani na fedha, wanafanya wapendavvyo na kujua kuwa wasimamia sheria wameshawekwa mfukoni....! Hawajaanzia hapa...!
Baba wa Taifa, Nyerere alishaonya kuwa ukiona mtawala yoyote anachezea 'wait haus' au anaachia tu 'ichezewe' na kuingiliwa na wafanyabiashara kama 'pango la majambazi' nchi imekwisha...ni viongozi wa kuogopa kama ukoma....hilo tunalo na tunalibeba mabegani mwetu kama laana tayari...ndio maana nchi haiendi, haitawaliki...wizi mtupu, raia wanakufa taabu na shida kila siku!
My take...ukombozi ni lazima...!
'Wait haus' ilishakamatwa, mikono ya Utawala imeshafungwa na fedha'...na ili kudhihirisha ukweli, Tazameni historia ya jamaa hawa ktk issue ambayo ilikwishawasilishwa pia na blog ya FeedBlitz kama ilivyo chini:
Serikali imewekwa mfukoni na Said na Ghalib Saad?
WAFANYABIASHA Said Mohammed Saad na Ghalib Mohammed Saad,ndugu wenye uraia wa Saud – Arabia na Tanzania walioripotiwa na gazeti la Raia Mwema hivi karibuni kuiibia serikali wastani wa bilioni 50 kwa mwaka, kwa udanganyifu wanapoingiza mizigo kutoka nje ya nchi kupitia bandari ya Dar es Salaam, hawajaguswa na serikali badala yake wanaoshughulikiwa ni maofisa wa TRA.
Hatua hiyo ya TRA kuwasimamisha kazi baadhi ya watumishi wake inasadikiwa kuwa moja ya janja ya kuwaepuka wakubwa waliofaidi wizi huo kwa kuzima moto uliowashwa na vyombo vya habari, maafisa wa usalama wa taifa na baadhi ya wabunge ambao hivi karibuni walishauri wafanyabiashara hao wachunguzwe ikithibitika wafikishwe mahakamani.
Wafanyabiashara hao wanaomiliki Kampuni ya Home Shopping Center, Kariakoo Mtaa wa Swahili na Msimbazi, sasa wanamwaga fedha kwa vigogo wa TRA ili ukaguzi wa kumbukumbu za bidhaa walizoingiza kwa kukwepa kodi tangu mwaka 2000, walipoanza biashara chini wakitokea nje ya nchi isitekelezwe.
Gazeti la Raia mwema katika matoleo mawili mwezi uliopita, lilianika wizi waliokuwa wakifanya kwa kukwepaji kulipa kodi kwenye bandari ya Dar es Salaam, wakishirikiana na baadhi ya maafisa wa TRA, TICTS na TPA.
Ilielezwa, kila kontena la futi 40 la nguo waliloingiza walikwepa kulipa ushuru wa sh milioni 10 kwa mwezi huku wakiingiza wastani wa makontena 200, kupitia kampuni mbalimbali za Clearing and forwarding ambazo wamekuwa wakizifungua kama uyoga, mahsusi kwa kazi hiyo.
Wanamiliki Kampuni nyingine China na Uarabuni ambazo zinaendeleza mtandao wa wizi huo, wanapoingiza bidhaa bandalini huku nyalaka zikionyesha bei ndogo kiasi cha kutia shaka, TRA wanapotaka kuthibitisha kwa muuzaji hujikuta wakiuliza mtu kampuni inayomilikiwa na mwenye mzigo husika.
Mbunge wa Viti Maalum, Chadema, Lucy Owenya, wiki iliyopita aliitaka serikali kutoa ufafanuzi kwa nini wafanyabiashara hawa wasichukuliwe hatua wakati wameibia nchi kiasi kikubwa cha fedha.
Alihoji, kwa nini serikali inapata kigugumizi kuwachukulia hatua? Kwa sababu ni wanaifadhili CCM ambao uchaguzi wa mwaka huu wameahidi kukichangia Sh milioni 500? Au nini?
Mengine yamebainika kuwa, waliingia nchini kinyume na taratibu ingawa walipita uwanja wa ndege wa Julius Nyerere na kutokomea mitaani kabla ya kutumia fedha kuhalalisha uwepo wao nchini.
Mwaka 2005, Said Mohammed, alimpiga risasi mfanyakazi wake alipokuwa akishusha bidhaa dukani kutoka kwenye gari lake, akamaliza shauri hilo kwa kumwaga fedha kwa aliyepigwa risasi, ndugu bila shaka na kituo cha polisi Msimbazi ambapo shauri hio lilifikishwa.
Agosti 15, 2006 saa 1:00 usiku kwenye Mtaa wa Msimbazi na Swahili Kariakoo jijini Dar es Salaam, wakati mashabiki wa Simba wakipita mbele ya duka lake wakisherehekea ushindi wa timu yao alimpiga risasi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Vingunguti, Deo Vicent. Shauri hilo pia lilifikishwa polisi Msimbazi, likaisha kama la awali.
Said na mdogo wake Ghalib wanamiliki genge la Wahalifu linaitwa Ze Popobawa ambalo linalowalinda na kuwaadhibu wapinzani au adui zao.
Miongoni mwa matukio yaliyofanywa na kundi hilo ni kumteka nyara, kumlawiti kisha kumpeleka Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere ili kumrejesha kwao kwa nguvu, mwanaume mwenye asili ya Lebanoni anayefanya biashara Dar es salaam.
Alikuwa anamiliki duka la vifaa vya nyumbani lililokuwa jirani na makutano ya barabara ya Morogoro na Bibi Titi, lakini baada ya tukio hilo duka hilo limehamishwa kwa sababu baada ya kukataa kurejeshwa kwao kwa nguvu, anaishi kwa kujifichaficha kuwaepuka wakina Saad.
Sababu ya Mlebanoni huyo aliyekuwa rafiki wa karibu wa Saad ni kumpa mimba mdogo wa Said aitwaye Salha bila kuoana kama mila zao za Yemeni zinavyotaka. Kwa sasa Said ana uraia wa Saud Arabia.
Kwa kupata mimba, Salha alipigwa na hao kaka zake, akanyolewa nywele zote na kunyweshwa vidonge ambavyo havikujulikani aina yake na alimpa kwa sababu zipi?
Binti huyo aliripoti tukio hilo kituo cha polisi Osterbay, likafunguliwa jalada OB/RB/13915 la Agosti 5 mwaka 2009.
Kama ilivyokuwa kwa matukio ya awali, mbali na polisi kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo, hadi kesho wanashangaa na hawajafanya lolote kufuatilia tukio hilo na tokea Salha aripoti tukio hilo, hajarudi kituoni hapo wala namba ya simu yake ya mkononi aliyoacha kituoni hapo haipatikani.
Kampuni nyingi za Clearing and Forwarding zilizokuwa zikimilikiwa na Said na kutumiwa kuiba makontena ya bidhaa anazoingiza nchini kutoka nje, baada ya kuthibitika kutenda makosa hayo zimefungiwa, ingawa kila ikifungiwa moja nyingine inasajili Brela kwa majina bandia kwani TRA inapohitaji mmiliki wake anayetokea huwa ni Said.
Maovu hayo yamemnufaisha vilivyo mfanyabiasha huyo. Said tangu alipoingia nchini mwaka 2000 anamiliki nyumba sita za ghorofa eneo la Kariakoo pekee.
Moja yenye ghorofa saba ipo mtaa wa Swahili na Msimbazi. Sehemu ya juu amewapangisha watu lakini kwa TRA anadaganya kwamba ni hoteli, kuendeleza kamchezo ka kukwepa kulipa kodi.
La pili lenye ghorofa sita lipo mtaa wa Congo na Agrey. La tatu lipo barabara ya Uhuru mkabala na shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa, bado linajengwa ni ya ghorofa.
La nne lipo mtaa wa Livingstone na Uhuru, jingine la tano lenye ghorofa sita lipo mtaa wa Mkunguni Kariakoo Sokoni karibu na duka la Azam Ice Cream na la sita lipo mtaa wa Lumumba karibu na CCM makao makuu limepakana na Hospitali ya Burhan.
Hivi watanzania tutaendelea kuona watu wakigeuza nchi yetu shamba la bibi mpaka lini? Ina maana kuifadhili CCM mtu anaachiwa kufanya anavyotaka?
Hii inatia shaka kwamba hata CCM wamepungukiwa kidogo kwa sababu kama mtu anakwepa ushuru sh bilioni 50 akatumia 500 milioni"kuwadhamini" ni dhahili ni kupungukiwa kwa kiasi kikubwa.
Inaashiria nchi ipo mikononi mwa hatari sawa na kwamba imezungukwa mabomu hatari ambayo yakiripuka athari yake itagusa kuanzia kizazi hiki mpaka cha ishirini kijacho.
Je, wana CCM kukubali ufadhili wa watu wa aina hii hawaoni kama wanarejesha historia ya mikataba waliyokuwa wakiingia machifu wa zamani akina magunga na Kimweri na wakolini?.
Rais Jakaya Kikwete , TRA, Usalama wa taifa letu, Takukuru, Waziri wa Fedha Mustafa Mkullo chukueni hatua!
JamiiForums |The Home of Great Thinkers