Jamani nimefuatilia sana posts kadha wa kadha kuhusu mashine za kutotolesha vifaranga humu JF na pia kupitia mitandao mingine ya kijamii. Nimegundua kuna nadharia tofauti tofauti kiasi kwamba mtu asipokuwa makini ni rahisi kuchanganyikiwa. Hivyo basi naomba kueleweshwa mambo yafuatayo ili niweze kufanya maamuzi ambayo sitakaa nijutie baadaye maana inahusisha kuteketeza hela isipoleta matokeo chanya inakuwa majuto.
Mashine za kuagiza nje na hizi za kutengeneza nchini zipi ni imara, zinastahimili, zinabana matumizi ya umeme na ina ufanisi mkubwa? Ukizingatia vigezo vingine vyote (kama setting ya joto, humidity, maji, na upatikanaji wa umeme) vibaki constant. Na je, kwa matumizi ya incubator ndogo ya mayai kati ya 100 hadi 200, matumizi ya umeme kwa mwezi yanaweza kunigharimu kiasi gani kwa wastani?
Tafadhali tuongee from experience.