Naombeni ushauri wa haraka, nimevurugwa mie

OIL CHAFU

JF-Expert Member
Jun 8, 2012
996
773
Jamani baada ya kuona maisha ya mshahara ni majanga tuu, nikaamua kujiongeza nifanye ujasiriamali. Nikapata wazo, na hili wazo nimelipata baada ya kusoma sana post za hapa JF kuhusu ujasiriamali na biashara. It goes like this;
  1. Nilinunua kiwanja cha kujenga (ni kubwa kiasi), naweza kujenga nyumba mbili za kawaida na bado space kubwa ikabaki. As for now nimepiga msingi, imebaki kunyanyua ukuta.
  2. Nimenunua shamba ekari 3, nimeshalima mahindi na hivi navuna. Matarajio yangu ni kuwa mwezi wa nane nitafute mkwanja nichimbe kisima nifanye irrigation farming na pia nifuge kuku.
  3. Nimenunua incubator machine na nimeanza kutotolesha vifaranga tayari (bado nipo kwa nyumba ya kupanga, sema tu ina nafasi ya kutosha). Sasa, hapa ndo kwenye matatizo. Plan yangu ilikuwa nisake mkwanja flani na ilitakiwa mwezi huu wa sita niwe nimeshahamisha vifaranga site kwa kujenga mabanda na servant quota ya kuishi kijana atakayesimamia hao kuku ili mimi niendelee na ujenzi kwa miezi kadhaa ndo nije nihamishe familia yote. Sasa mkwanja umeyumba kidogo na ratiba imevurugika, ingawa vifaranga tayari wanakua na space inaanza kubana kwa sababu wanazidi kuongezeka kila wiki moja au mbili wanatotoleshwa wengine. Nina kuku wachache ambao wanataga na ndio natotolesha hayo mayai.
Mgogoro:
Mwenye nyumba ameanza kumind sana na kunisema sema mpaka na mimi nimechukia, natamani muujiza utokee nipate fedha ndani ya mwezi mmoja niwe nimehamisha mifugo site, hapa nibakize familia tuu. Nimeenda bank kwa minajili ya kutop up loan, wananizingua wanasema wamesitisha mikopo mpaka July/August ndo niende. Nimekereka usipime. Nikafikiria niuze gari bado muafaka hauji kichwani, nikiangalia jinsi inavyonirahisishia mizunguko yangu na kubalance muda wa kazini na pia majukumu yangu binafsi. Nimemshirikisha mwenzangu naye hajawa tayari kuuza gari.

My point: Wapi naweza kupata mkopo wa at least kuanzia 5m hadi 8m bila kuzungushwa sana na kupoteza muda? At least kwa hiyo hela naweza kuhamisha mradi site bila wasiwasi wowote na kuanza kupata faida kutoka kwa mradi as soon as possible.

Nina uwezo wa kutotolesha vifaranga 500 kwa mwezi kutokana na mashine niliyo nayo yenye capacity ya 700 eggs. Na hao vifaranga nikiwakuza kwa miezi hata minne tuu nikaanza kuwauza ni hela ndefu aisee. Kwa sasa ni kwamba hiyo mashine naiunderutilize. Nimeandaa andiko la mradi lakini wazoefu wananiambia taasisi za fedha sasa hivi zimeyumba ndo maana wanasita kutoa mikopo fasta fasta. Mwisho wa yote nikifeli plan B inabidi nirudie plan A ya kusubiri staff loan ofcn kama walivyoniahidi bank mwezi wa 7/8.

Nishaurini wadau.
 
Usiuze gari, vuta mda mpk miezi hiyo sio mbali. Coz hata ukiuza gari inawezekana ukashindwa kukava matatizo yote kwa maramoja

Nakupata mkuu hata mimi nawaza hivyo. Unajua mazingira yetu ya kibongo usafiri ni shida, hivi sasa kwa gari langu nikiwa na shughuli shamba au site, any time naweza kuchomoka nikacheki kinachoendelea na wakati mwingine naweza enda kufanya shughuli flani, alafu ndani ya muda ninaopanga naweza kurudi fasta na nikawahi job mtu asinishtukie. Ila bila gari, kwenda site tuu kama ni public transpot kwenda tu ni issue, na kukodi ni gharama sana
 
pole mkuu.pia nakupongeza kwa kuona mbali kwamba mshahara pekee hauwezi fanikiwa maisha haya..mungu atakusaidia utafanikiwa kuipata hyo hela na miradi yako itaendelea kama kawaida
 
Sikiliza mfuate mwenye nyumba ongea nae kiume mweleze hali yako halisi na mipango yako kiunagaubaga nakwambia atakuelewa tu na baada ya hapo subiri mpk mwezi july kavute mkopo benki. Pia sitisha kutotoa vifaranga mpk ukikaa sawa kuku wakitaga uza mayai
 
Nakupata mkuu hata mimi nawaza hivyo. Unajua mazingira yetu ya kibongo usafiri ni shida, hivi sasa kwa gari langu nikiwa na shughuli shamba au site, any time naweza kuchomoka nikacheki kinachoendelea na wakati mwingine naweza enda kufanya shughuli flani, alafu ndani ya muda ninaopanga naweza kurudi fasta na nikawahi job mtu asinishtukie. Ila bila gari, kwenda site tuu kama ni public transpot kwenda tu ni issue, na kukodi ni gharama sana
Uza gari nunua bodaboda iliyotumika
 
weee shindwa mwanamke yupi atakaa na mume hana gari?
unataka aanze kuchepuka?
akope tu jamaa
Ukisoma vizuri maelezo yake ni kwamba wife wake nae anazungusha (ana gari), ila hajaafiki kuliuza. Ndo nikamshauri jamaa aongee na wife ili yeye jamaa aliuze gari lake halafu ategemee lift za wife.
 
Mkuu hongera sana kwa kuthubutu kuanzisha mradi...mimi nafikiri usiuze gari kwanza kama umekosa mkopo.
1. Plan A- ongea na mwenye nyumba kinyenyekevu..jishushe kabisa kwake na ujifanye mjinga...atakuelewa tu...ikishindikana muahidi pesa kidogo.
2. Plan B- jifanye mjinga na huelewi..mwezi wa saba ni karibu sana.
Plan C - Ongea na mwanamke uuze gari.
 
Ukisoma vizuri maelezo yake ni kwamba wife wake nae anazungusha (ana gari), ila hajaafiki kuliuza. Ndo nikamshauri jamaa aongee na wife ili yeye jamaa aliuze gari lake halafu ategemee lift za wife.

Mkuu gari ni moja, siyo mawili bana
 
Kiukweli ndugu mtoa mada,kilicho chako ndicho kinachoweza kukusaidia,kama una uhakika na mradi wako baada ya miezi kadhaa au mwaka m1 utaweza kua unaingiza pesa ya kutosha nakushauli uza gari,gari utanunua tu jingine mambo yakienda sawa.mi mwenyewe hapa juzi nimetoka kuipiga bei gari ili hyo pesa inivushe kutoka A to B na tayali niko katikati navuka.kama mikopo inasumbua kilicho chako ndicho cha kukuokoa,kweni kabla ya kununua gari hukuwahi kuishi?maamuzi magumu hua yana manufaa sometimes
 
Mkuu Uza Tu Hiyo Gari Ili Mambo Yako Yaende Sawa ... Kama Vipi Tupia Picha Ya Hiyo Gari Tuione ... Kuna Watakaoipenda Wanaweza Kuinunua ...
 
weee shindwa mwanamke yupi atakaa na mume hana gari?
unataka aanze kuchepuka?
akope tu jamaa
Mawazo ya kizamani hayo sana ....yan una mawazo hayo hata wakati huu ....uchepuke kisa mume hana gari ?? What nonsense...hapo point ya msingi niliyoiona hapo ni kua mke ameona kua gari itamsaidia ktk shuhul zake ama mishe zake za kufatilia miradi na kwenda site on time na kufanya mishe nyingi kwa mda mfupi thus why amemshaur asiuze na sio ishu ya kuchepuka ambayo haina mashiko kabisa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom