Katika vitu nilivyokuwa udogoni nakula kichapo nakesho narejeo vile vile na inaweza hata isifike kesho,nikala kichapo asubuhi na jioni nikarejea,ilikuwa ni kudokoa lishe hiyo.
Yaani katika udokozi wake aisee shetani alishinda,maana hadi nakuwa bado Jikoni kwa mke wangu nizikuta napiga nusu kijiko kisha nasepa.
Lishe nzuri mnoo,tena mno,hupenda sana kuitumie kwenye Uji,na mboga zama majani,kama kisamvu,mchicha,msusa,hata samaki,na hata kwenye Nyama pia ni nzuri mno kwa wale wa Kanda ya magharibi wanajua zaidi utumiaji wake hizi