Hoja za Waombaji Ajira za Waalimu

Hoja za Waombaji Ajira za Waalimu

index namba ya form four mwaka 1995 haina maana yoyote cha msingi chuo umemaliza mwaka gani sio kila anaemaliza form four anaunga moja kwa moja inawezekana alikaa bula kwenda shule akaja kusoma form six private mwaka 2010 akamaliza chuo 2016
fikiria vizuri mwisho ilikuwa kuomba wenye miaka isizidi 45 sasa kama index namba anaonekana amemaliza 1995, uyo lazima awe above 45 hadi saivi sas inakuaje mfumo umemchukua au nikuhulize mtu amemaliza form 1995 had now atakuwa na miaka mingap?
 
nani kakidanganya chukua kamaliza form four na miaka 17 mwaka 1995
kapata ajira mwaka 2022 toka 1995 mpaka 2022 ni miaka 27 chukua 27+17 ni 44 ivyo sio lazima kuwa alifika zaisi ya 45
 
fikiria vizuri mwisho ilikuwa kuomba wenye miaka isizidi 45 sasa kama index namba anaonekana amemaliza 1995, uyo lazima awe above 45 hadi saivi sas inakuaje mfumo umemchukua au nikuhulize mtu amemaliza form 1995 had now atakuwa na miaka mingap?
usijione we unaakili kuliko serikali wanaoajiri wenyewe sio wajinga waende kinyume na sheria huyo mtu hata akimaliza firm four mwaka 1995 akiwa na miaka 18 au 17 mpaka mwak jana 2022 havuki 45
 
TAMISEMI MSAIDIENI MHE RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN KUZUIA MALALAMIKO YA NAFASI ZA AJIRA 21,200 ZILIZOTANGAZWA KADA YA ELIMU NA AFYA

Na. Matuguta Zax

Nampongeza sana Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka miwili na sasa ameanza mwaka wa tatu kwa kishindo cha kumwaga ajira za kada ya Afya na Elimu 21,200. Kwa kweli mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni, katika suala la kutoa ajira nyingi kiasi hiki Mama amethubutu, ameweza na anatosha kabisa tumuunge mkono 2025.

Aidha, naipongeza Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kuendelea kumsaidia Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwatumikia watanzania kwa kuandaa mfumo mzuri sana wa kupokea maombi ya nafasi za ajira, mfumo mzuri wa kuchakata maombi na hatimaye kuwasambaza vijana hawa wazalendo kwenye maeneo mbalimbali kwa ajili ya kwenda kutoa huduma kwa watanzania wenzao. Kwa kweli Kazi kubwa na nzuri mnayoifanya inampa heshima kubwa sana Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Chama cha Mapinduzi kwa ujumla. Hivyo nathubutu wazi kuwashukuru Mhe Angellah Kairuki Waziri TAMISEMI, Festo Dugange na Deogratius Ndejembi Manaibu Waziri TAMISEMI.

Pamoja na Kazi yenu njema kama timu imara ya Ofisi ya Rais TAMISEMI bado usemi wa wahenga umeendelea kuthibitika kwamba Mtu hujikuna panapowasha.

Ni ukweli usiopingika kabisa kwamba vijana wanaoomba nafasi za ajira wamekuwa wakilalamikia mapungufu mbalimbali yanayojitokeza katika kuajiri. Siyo vijana pekee yao bali hata wazazi wao na walezi wao wameyalamikia mapungufu hayo ya namna gani vijana wao hupewa ajira hizo na Serikali. Kwa kuthibitisha kuwa vijana wanapitia wakati mgumu hata wabunge wao wamejitahidi kuelezea hisia na masikitiko ya mapungufu ya michakato ya ugawaji wa nafasi za ajira kwa vijana wanaotuma maombi yao.

Kwa umuhimu wa suala lenyewe, naomba ikumbukwe kuwa mwaka 2021 zilitoka nafasi za ajira 9,675 kada ya Afya na Elimu na mwaka 2022 zilitoka nafasi za kada ya Afya ya Elimu 17,412. Katika michakato ya ugawaji wa nafasi za ajira kwa vijana waliotuma maombi yao kulikuwa na malalamiko kama haya:-

1. Nafasi za ajira zilizotoka 2021, baadhi ya wahitimu waliomaliza 2021 kupangiwa vituo vya Kazi wakiachwa waliomaliza mwaka 2015, 2016, 2017,2018,2019 na 2020. Kutowatendea haki namna hii vijana ni kuwalazimiaha kujiingiza katika vitendo visivyofaa kama vile umalaya, ushoga na utumiaji wa madawa ya kulevya.

2. Nafasi zilizotoka tena mwaka 2022, baadhi ya wahitimu wa mwaka huo huo 2022 walipangiwa vituo vya Kazi wakiwa na sifa zile zile za rundo la vijana waliomaliza 2015, 2016, 2017, 2018, 2019, 2020 na 2021 ambao waliachwa wakiwa na vigezo vyote vinavyotakiwa. Kutokana na kukosekana kwa utaratibu mzuri wa namna gani wahitimu hawa wazalendo kupewa haki yao wengine walichukua maamuzi magumu ya kujinyonga. Sasa inatosha tuwaonee huruma hawa vijana!

3. Kutokupewa kipaumbele wenye umri mkubwa zaidi kama vile 44, 45 ilihali kijana kama huyu asipopewa nafasi ya kipaumbele maana yake mwaka utakaofuata atakuwa nje ya vigezo. Kwa nini kuupa nguvu huu usemi wa wahenga kwamba aliyeshiba hamjui kabisa mwenye njaa!

4. Vijana wanaojitolea kwenye shule zetu wakihangaika kuwasaidia watoto wetu hawapewi kipaumbele na badala yake wanapewa kipaumbele vijana ambao wanajitolea kwenye mifuko ya wakubwa. Haki ya watoto wa masikini waliosoma kwa Shida wakauza mashamba yote ya urithi ili wapate Elimu lakini bado hata kuajiriwa napo inakuwa ngumu sijui tena wauze nguo zao za urithi ili wapate ajira? Inatosha tuwaonee huruma hawa vijana tuwape haki yao!

USHAURI WANGU TAMISEMI

Mosi, nawaomba msaidieni Rais Samia aliyewaamini kwa Moyo wake wote katika kufanya jambo hili la kuajiri watoto wa wapiga kura wake basi isafishe Serikali yake ya Awamu ya Sita iliyojizolea sifa ya Usikivu kwa kuhakikisha mnawajali watoto wa wapiga kura wake. Bado wananchi wake wanahitaji kumshika mkono Mama Samia na kuvuka naye 2025. Watendaji wa OR-TAMISEMI kataeni kuwa Kikwazo!

Pili, Kwa kuwa Ofisi ya Rais TAMISEMI imepewa dhamana ya kumsaidia Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kupokea maombi ya nafasi za ajira, kuyachakata na kuwasambaza vijana wa kada ya Afya na Elimu kwenye vituo mbalimbali nchini mapendekezo yangu katika ajira hizi 21,200 na zitakazoendelea kutolewa na Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan ni haya:-

1. Mwaka wa kumaliza Chuo upewe kipaumbele. Kwa hiyo kundi la 2015 lianze na baadaye miaka mingine ifuate. M/kiti wa CCM aliahidi kutatua Kero kwa wananchi wake naomba TAMISEMI tumie njia hii kumsaidia Mhe Rais kutekeleza alichokiahidi kwa wapiga kura wake.

2. Umri wa mwombaji upewe kipaumbele. Anzeni kuwapangia vituo kwanza wenye miaka kuanzia 30-45 halafu wengine wafuate. Mwenyekiti wa CCM na Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewapa imani kubwa TAMISEMI naomba tumieni hiyo kumsaidia Rais.

3. Wanaojitolea wapewa kipaumbele. Hili ni kundi jingine muhimu linapaswa kuangaliwa. Angalizo, kundi hili linaweza kuwa chanzo cha rushwa na kukosesha haki kwa kundi la kwanza na la pili hapo juu. Uadilifu, uaminifu na hofu ya Mungu ndiyo zinaweza kutetea haki za kundi hili.

4. Idadi ya kwamba mwombaji ameshaomba mara ngapi anakosa nafasi nalo lipewa kipaumbele. Kwa sababu kuna vijana wanaomba ajira hizi kwa mara ya kumi sasa. TAMISEMI tumie njia hii kumsaidia Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutatua Kero za wananchi na wapiga kura wake.

Mwisho siyo kwa umuhimu wake, kwa kuwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amewaamini ninyi TAMISEMI kufanya jambo hili la kuwapangia vituo vijana wanaoomba nafasi za ajira 21,200 kada ya Afya na Elimu, basi ilindeni haki ya kila mmoja na mtangulizeni Mwenyezi Mungu katika shughuli hii.
Ukishaweka kigezo cha kujitolea kama sifa ya kupewa ajira utasababisha RUSHWA na UPENDELEO wa kufa mtu!!. Tuwe wakweli!! Unamtaka kijana ajitolee niambie atajikimu kwa namna gani?? Hii itasababisha waliojitolea kwa dhati lakini hawawezi kutoa rushwa wasipewe nafasi!! Kuna kijana namfahamu alijitolea miaka ya kutosha kwenye shule moja ya sarikali lakini aliambulia patupu. Kuna watu watapata barua za uthibitisho wa kujitolea huku hawajawahi kabisa kujitolea na maumivu yatakuwa makubwa sana kwa watu!! Vigezo vizuri na vya haki ni 1. Mwaka wa kuhitimu upewe uzito wa kwanza. 2. Watu waliomaliza chuo mwaka mmoja wapangwe kwa umri. Mwenye umri mkubwa apewe kipaumbele miongoni mwa wahitimu wenzake waliohitimu mwaka mmoja. NASISITIZA: Umri ni kigezo cha pili na si cha kwanza!! Vinginevyo wahitimu wa mwaka jana watapata ajira kwa kuwa tu wana umri mkubwa. Ajilaumu mwenyewe kwa nini alichelewa kwenda shule!! Tunategemea waliohitimu zamani watakuwa na umri mkubwa pia kuliko wanaohitimu sasa!!
 
usijione we unaakili kuliko serikali wanaoajiri wenyewe sio wajinga waende kinyume na sheria huyo mtu hata akimaliza firm four mwaka 1995 akiwa na miaka 18 au 17 mpaka mwak jana 2022 havuki 45
Kuna scenario ambayo mwenye umri wa miaka 45 anaruhsiwa kuajiriwa. Kama tayari ni mtumishi wa serikali kwa mfano ni mhudumu, halafu akajiendeleza na kufanikiwa kupata cheti cha form 4, kisha cha form 6 na akaenda chuo na kupata diploma yake. Hawa wanaruhusiwa kuomba ajira kwa kupitishia barua yake kwa mwajiri wake!!
 
fikiria vizuri mwisho ilikuwa kuomba wenye miaka isizidi 45 sasa kama index namba anaonekana amemaliza 1995, uyo lazima awe above 45 hadi saivi sas inakuaje mfumo umemchukua au nikuhulize mtu amemaliza form 1995 had now atakuwa na miaka mingap?
Ni kwamba aliomba nafasi tayari akiwa kwenye utumishi wa umma kama vile mhudumu. Akajiendeleza na kufanikiwa kupata cheti, diploma au digrii. Huyo hata kama ana miaka 50, anaweza kuchukuliwa. Ili mradi alipopata ajira ya umma hapo awali alikuwa na miaka pungufu ya 45. Nina mfano halisi: Kulikuwa na kijana aliajiriwa kwenye shirika la umma kama mhudumu wa afya (alikuwa anafanya kazi ya kuzibua vyoo). Alikuwa na cheti cha form 4 division 4. Baada ya miaka kadhaa akaamua ku-resit na akafaulu. Akasoma A level kwa tuition kwa mwakla 1 akafanya mtihani na kufanikiwa kupata division 3. Akaomba chuo kusomea shahata ya elimu - sanaa. Watu wa namna hii huwa wanafanyiwa categorisation na mwajiri kama elimu yake ya sasa mwajiri anaihitaji. Vinginevyo wanaruhusiwa kuomba ajira zinazotangazwa kwa kupitishia barua kwa mwajiri!!
 
Hata mwaka wa kumaliza chuo utazamwe mkuu.

Waliohitimu 2014 kurudi nyuma wote walikuwa wanaajiriwa direct tena bila kuomba. Wapo waliokataa coz walikuwa busy na private sector, wengine walikataa mazingira magumu.

Leo hii 2023 mtu anaomba kazi ya ualimu na cheti cha 2010, huyo ana haki ya kuachwa unless awe na sababu zenye mashiko 2010 alikuwa wapi.
Acha roho mbaya!!
 
Naombeni ufafanuzi kati ya hizo 21000 za afya ni ngapi na elimu ni ngapi?
Ina maana hata hilo tangazo haujawahi kulisoma? kazi kweli kweli!!

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imepata kibali cha ajira za Watumishi wa Kada za Afya 8,070 kwa ajili ya Hospitali za Halmashauri, Vituo vya Afya na Zahanati pamoja na Ualimu 13,130 wa Shule za Msingi na Sekondari watakaofanya kazi chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.
 
Ni nani alifanikiwa kuomba nafasi ya ualimu kwenye shule ambayo idadi ya waombaji ni chini ya 10 kwenye shule hiyo hadi siku ya mwisho wa mambi tarehe 25/04/2023 saa sita za usiku.
 
Ni nani alifanikiwa kuomba nafasi ya ualimu kwenye shule ambayo idadi ya waombaji ni chini ya 10 kwenye shule hiyo hadi siku ya mwisho wa mambi tarehe 25/04/2023 saa sita za usiku.
Kuna binti aliomba mikoa ya kigoma tabora lindi sehemu waliokuwa wengi ilikuwa ni chemistry
Ila sehemu zingine zote walikuwa 6-8 Physics
 
Sorry ndugu naomba kuuliza ivi tamisemi wenyewe hawana issue za interview
 
Ni kwamba aliomba nafasi tayari akiwa kwenye utumishi wa umma kama vile mhudumu. Akajiendeleza na kufanikiwa kupata cheti, diploma au digrii. Huyo hata kama ana miaka 50, anaweza kuchukuliwa. Ili mradi alipopata ajira ya umma hapo awali alikuwa na miaka pungufu ya 45. Nina mfano halisi: Kulikuwa na kijana aliajiriwa kwenye shirika la umma kama mhudumu wa afya (alikuwa anafanya kazi ya kuzibua vyoo). Alikuwa na cheti cha form 4 division 4. Baada ya miaka kadhaa akaamua ku-resit na akafaulu. Akasoma A level kwa tuition kwa mwakla 1 akafanya mtihani na kufanikiwa kupata division 3. Akaomba chuo kusomea shahata ya elimu - sanaa. Watu wa namna hii huwa wanafanyiwa categorisation na mwajiri kama elimu yake ya sasa mwajiri anaihitaji. Vinginevyo wanaruhusiwa kuomba ajira zinazotangazwa kwa kupitishia barua kwa mwajiri!!
nimekuekewa chief
 
Back
Top Bottom