Hoja za bunge

AMKA

Member
Jul 9, 2011
94
11
Hellow waungwana hebu tujaribu kuwaza na kuwazua hoja zinavyoendeshwa bungeni. Utamsikia mweshimiwa mbunge anapopewa nafasi ya kuchangia hoja ananza na kusema mimi naunga mkono hoja asilimia mia moja alafu ananza kwa kusifia hotuba na kutia mbwembwe na madoido kibao. Badae unashanga ananza kuelezea tena madhaifu yanayojitokeza kwenye muswada husika. Anaukosoa wee!! mara anapomaliza kukosoa anasema naunga mkono hoja. Sasa sisi wananchi tunashindwa kumwelewa anasapoti kua hayo madhaifu yaliyopo kwenye muswada hayana shida yaendelee kuwepo au anamanisha nini?? Haswa waheshimiwa wabunge wa chama tawala sijui ni sera ya chama kua usipinge hoja inayotolewa na mweshimiwa waziri wa chama chako au mnamanisha nini??. Nawashauri waheshimiwa haswa wa chama tawala pitisheni hoja kulingana na maslahi ya wananchi waliowaweka madarakani badala ya kuangalia maslahi ya chama.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom