Serikali na wapambe wa DP World hawajajibu hoja za wananchi mpaka sasa

Fernando Wolle

JF-Expert Member
Aug 19, 2022
387
764
Katika kufuatilia mjadala huu mzito wa Sakata la Bandari, Kuna kitu nimejifunza kikubwa kwamba hoja za upande wa Wananchi ni Nzito na zina mashiko kuliko upande wa Serikali na wapambe wake.

Wananchi wanazo hoja nzito haswa, maswali magumu mno lakini upande wa serikali wanachojua wao Kila hoja kutoka kwa wananchi majibu yao ni yanahusu faida za uwekezaji tu, wakienda mbali sana basi wataelezea uwezo wa DP World na namna inavyoendesha shughuli za Bandari Kidigitali wanaishia hapo. Lakini wakibanwa sana vitisho vinaanza.

Kwa ufupi Serikali na wapambe wake wana majibu mepesi kwa Maswali magumu.

Mfano upande wa Wananchi wanauliza Muda kikomo wa huo mkataba ni miaka mingapi? Onesheni palipoandikwa kwenye Mkataba! Kinachojibiwa ni kwamba DP World ni kampuni yenye uwezo mkubwa sana msiwe na hofu. Sasa hilo ndo jibu?

Wananchi wanauliza kwanini muswada ulopelekwa Bungeni juzi juzi unataka kubadilisha Sheria yetu inayolinda rasilimali zetu ya "Natural Wealth resources Act" ya mwaka 2017 kuwafeva DP World?? hamuoni huo ni Uhaini ? Utakachojibiwa ni kwamba unaleta uchonganishi.

Sasa naona baada ya Kamati kuu ya Chama tawala kuketi ikaongeza point nyingine kwamba Kinachotakiwa Sasa ni kuwaelimisha wananchi ili waelewe. Watoa elimu wenyewe Sasa wanatiririka faida za uwekezaji na uwezo wa DP World kitu ambacho dhahiri Kila mtu anakijua.

Kwa ufupi hili sakata sio linahitaji elimu ila linahitaji majibu Stahiki kwa Maswali magumu yaliyoulizwa na wananchi basi! Na ni kitu ambacho hakiwezekani kwa serikali maana majibu ya hayo maswali kwenye Mkataba hayapo na yanatakiwa yatokane na kilichopo ndani ya mkataba. Maswali na hoja za msingi za kwenye Mkataba huo Serikali na wapambe wake wanakwepa kujibu.

Kwa ufupi anayekubaliana na mkataba huu Kuna mambo mawili tu kwa huyo mtu la kwanza kama mtu anakubaliana nao basi ujue ni Punguani na kama sio Punguani basi Kahongwa! No more No Less.
 
Eti maelezo yote ya vifungu aliyotowa Shivji jibu lake eti hata wajinga huzeeka. Hivi kweli Hilo ni jibu? Tuendelee kuamini mkataba unamanufaa kwa kujibu hoja za Shivji kuwa hata wahuni huzeeka😂😂😂😂☹️☹️☹️
 
Kwa kifupi serikali imebanwa mbavu na wananchi wake na inatapatapa kupata majibu, ndio maana majibu yake ni yaleyale kila mpambe wake anajititimua kujibu. Imeboronga na inaomba jambo hili liishe ki namna japo imekosea. Mkubwa akikosea huwa ni shughuli pevu kukubali kosa lake mbele ya wadogo. Kinachotakiwa ni wadogo kumstahi tu aibu ipite. Kukosea kupo ila kukubali makosa ni ishu kubwa
 
Nyie wapinga maendeleo mmegoma kabisa kuelewa makusudi, suala la muda mmeelezwa litawekwa kwenye mkataba wa kibiashara ambao utaeleza eneo mahususi la kazi, mnaleta upotoshaji ili mpate Kiki za kisiasa!
 
Kwa kifupi serikali imebanwa mbavu na wananchi wake na inatapatapa kupata majibu, ndio maana majibu yake ni yaleyale kila mpambe wake anajititimua kujibu. Imeboronga na inaomba jambo hili liishe ki namna japo imekosea. Mkubwa akikosea huwa ni shughuli pevu kukubali kosa lake mbele ya wadogo. Kinachotakiwa ni wadogo kumstahi tu aibu ipite. Kukosea kupo ila kukubali makosa ni ishu kubwa
Kabisa upo sahihi 100%
 
Back
Top Bottom