Hoja ya Zitto Kabwe dhidi ya Pinda sasa yaimarika!

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
0001ngeleja.jpg

Waziri Ngeleja aliyeachwa katika Wizara ya Nishati na Madini


2895.png
Adam Kighoma Malima.............bosi wake Ngeleja kamwaga unga lakini kwenye uwajibikaji wa JK huyu ni mtu safi!










Khoja ya Zitto Kabwe ya kukosa imani na Waziri Mkuu imepata matumaini makubwa baada ya JK kurudia makosa yaleyale ya kuipuzilia mbali taarifa ya CAG ambayo iliyoweka hadharani matatizo makubwa ya wizi na ubadhirifu katika
Wizara (4) za kilimo, Nishati, Viwanda na Biashara na Serikali za mitaa lakini baadhi ya mawaziri au manaibu wao bado kurudishwa kwa maana ya uhamisho tu kwenye nyadhifa zao ikiashiria ya kuwa JK kaiponda taarifa tajwa.

Aidha uteuzi wa Prof. Maghembe kutoka wizara ya kilimo kwenda Maji unazua utata mkubwa na huku aliyekuwa naibu wake Chiza kupandishwa cheo katika wizara ileile kwa kazi chafu ya usimamizi wa wizara tajwa kulingana na taarifa ya CAG unaonyesha jinsi serikali ya JK inavyofanya kazi kwa upendeleo, mashinikizo na ya kuwa haijali maelekezo ya Bunge lake lenyewe.

Uteuzi wa Kighoma Malima aliyekuwa naibu wa Nishati chini ya Ngeleja unazua maswali mengi ambayo hayana majibu kwa sababu baadhi ya manaibu wamewajibishwa lakini huyu na Nyalandu wanaonekana kuwa ni
"the untouchables" kwenye hii serikali ya wababaishaji................

Mkuchika na Mwanri nao walivurunda sana wizara ya serikali za mitaa kulingana na taarifa ya CAG lakini JK na Pinda wake wametia pamba masikioni na hivyo kutia dosari kubwa katika zoezi zima la kuwawajibisha watendaji wakuu ndani ya serikali.

Lakini hii siyo mara ya kwanza kwa JK kukaidi maelekezo ya Bunge ambalo wengi wa wabunge wake wanatoka ndani ya chama chake cha ccm. Katika sakata la Richmond/Dowans manaibu kama Ngeleja walinusurika na leo imeonekana kwa uwazi kabisa ya kuwa kuwapandisha manaibu siyo dawa ya matatizo yaliyopo. Hata akina Dr. Hosea hawakuondolewa kule Takukuru kwa kulipotosha Bunge juu ya sakata la Richmond hadi muda wao wa kustaafu ulipofika na watendaji wengine ilikuwa ni pata shika kuwang'oa ikiashiria JK na Pinda wanalidharau bunge kwa kugoma kutekeleza maagizo yake.

Kutokana na upembuzi huo, nionavyo khoja ya kumn'goa Pinda bado ina mashiko manene na inapaswa kuendelea kutiliwa mkazo ili kumshurutisha JK na Pinda wake waache na kukoma kabisa kuiendesha nchi kisanii-sanii hivi
 
Tunasubiri Zito atasema nini... Kama akiondoa hoja ile itakuwa proof kwa Zito kutumiwa na CCM au lengo lake lilikuwa Mkulo atoke.
 
Mkuu! mimi nimeshachoka na huyu mkuu na serikali yake na sitaki kuumwa na kichwa tena i will sit and watch till he is gone maana jamaa uwezo wake ni mdogo mno na i have to be honest that i really do think i could make a best president compared to this honorable. I just do not understand him at all, Aaarghh what a frustrating creature.:wacko:
 
Tunasubiri Zito atasema nini... Kama akiondoa hoja ile itakuwa proof kwa Zito kutumiwa na CCM au lengo lake lilikuwa Mkulo atoke.

STEIN uko sahihi the ball is now on Zitto's court........kama akitetereka tunajua amenunuliwa na hawa wanamagamba.......
 
Last edited by a moderator:
Hapo ndio nimeshindwa kumwelewa JK unavurunda huku unapewa kule haina maana bora asingevunja kabla 2015 itakuwa yeye
[MENTION]
Blaki Womani[/MENTION] ni kweli, sera za Nyerere za kuhamishana yaelekea ndizo sera za ccm na bila kushinikizwa kamwe watakuwa wakiziimba kwenye majukwaa tu................
 
Bravo Zito, at least we are now experiencing the true color of opposition.

Imagine what Tanzania would have been without opposition?

Okada mageuzi haya ya shingo upande hayatoshi.....tuna dhiki nying sana tunahitaji mabadiliko ya haraka na yenye kutia matumaini na haya hakuna kitu hadi sasa ni kupooza mkaa unaowaka ukitarajia utazimika kumbe unaukoleza zaidi.......
 
Last edited by a moderator:
Watuhumiwa kwenye ripoti za CAG na zile za Kamati za Bunge sio mawaziri tuu. In fact mawaziri wamekuwa responsible politically. Wako wakurugenzi, makatibu wakuu na watumishi wengine wa ngazi za juu. Kwa hiyo, kama Rais atabadilisha mawaziri tuu bila kuwachukulia hatua hao walio chini ya hao mawaziri ni kama vile hajafanya kitu. Kwa hiyo hoja bado ni ya msingi unless walio chini ya mawaziri watachukuliwa hatua pia. Kumbuka kwenye ripoti ya kamati yake Augustino Mrema alisema halmashauri zote zimeoza.
 
Not on Zitto but with all Tanzanians

yeah Mbinga you are right lakini hiyo khoja iko bado kwa Zitto kazi yetu ni kumshinikiza afanye the right thing...................
 
Last edited by a moderator:
Watuhumiwa kwenye ripoti za CAG na zile za Kamati za Bunge sio mawaziri tuu. In fact mawaziri wamekuwa responsible politically. Wako wakurugenzi, makatibu wakuu na watumishi wengine wa ngazi za juu. Kwa hiyo, kama Rais atabadilisha mawaziri tuu bila kuwachukulia hatua hao walio chini ya hao mawaziri na kama vile hajafanya kitu. Kwa hiyo hoja bado ni ya msingi unless walio chini ya mawaziri watachukuliwa hatua pia. Kumbuka kwenye ripoti ya kamati yake Augustino Mrema alisema halmashauri zote zimeoza.

EMT huoni yakuwa kama Mkuchika na Mwanri wanaonekana bado wanafaa sasa hao wakurugenzi n amakatibu wakuu si wanafaa zaidi katika wizara ya serikali ya mitaa? Hakuna nia ya kuirekebisha nchi hii ndani ya ccm.........sioni hata dalili.................mengineyo aliyoongea JK leo ni ushahidi kuwa anacheza na maneno tu lakini moyoni anafurahia ufisadi uendelee kushamiri.......
 
Last edited by a moderator:
Tunasubiri Zito atasema nini... Kama akiondoa hoja ile itakuwa proof kwa Zito kutumiwa na CCM au lengo lake lilikuwa Mkulo atoke.


Hukumuelewa kabisa alisema mawaziri wenye kashfa wasipowajibika wao kama wabunge(not only ZK) watamuajibisha waziri mkuu. Wameshaondolewa kwenye wizara kwa itabidi ashauriane na wenzake cha kufanya kama ni kuiendeleza au kuiacha.
 
Yaani unachafua bedroom ya kawaida,badala ya kuadhibiwa,unapelekwa masterbedroom !!!

Politics!Politics! Politics!!!!

marejesho.............you are very spot on.........mkuchika kachafua sebule sasa kahamishiwa ikulu ambako ni master bedroom........is it not polluting the whole government really?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom