Hoja ya Wabunge kuwa Mawaziri

Hii thread nzuri sana..hivi kuna viongozi wanafika hapa kupata haya mawazo?

Je as a society are we ready kubadilika?

Why is it taking so long?

Je nani atatetea na kuleta haya mabadiliko?

Kwa nini mjadala wa katiba mpya usianze sasa?

Kenya pamoja na matatizo yao wamedhamiria kuwa na katiba mpya..why not in Tz?

What is the problem???
 
Kitu kinacho nimaliza ni kuwa waziri mkuu nae ni mbunge. Sasa waziri mkuu ana muda gani kutumikia wananchi wa jimbo lake? Wewe tayari ni kiongozi wa nchi nzima lakini bado kuna baadhi ya watu wana kuita mbunge wao. Mimi naona ingefaa kama mtu akipewa uwaziri aachie ngazi kwenye ubunge ili ashugulikie maslahi ta taifa. tatizo ya hilo ni moja tu kuwa akishaachia ngazi nani achukue nafasi yake. Ila nina amini kabisa tuki taka kubadilisha hili tunaweza kuja na mfumo mbadala.
 
Hii thread nzuri sana..hivi kuna viongozi wanafika hapa kupata haya mawazo?

Je as a society are we ready kubadilika?

Why is it taking so long?

Je nani atatetea na kuleta haya mabadiliko?

Kwa nini mjadala wa katiba mpya usianze sasa?

Kenya pamoja na matatizo yao wamedhamiria kuwa na katiba mpya..why not in Tz?

What is the problem???

The problem is that leaders are looking after themselves and not the people. Hawawezi kubadilisha mfumo mpaka wajue una manufaa kwao. Kenya wali badilisha ila kuongeza nafasi ya uwaziri mkuu ili wampachike Odinga laa sivyo na wao ndiyo wale wale. Mimi nadhani ni sisi wananchi wenyewe kudemand what is best for us. Ukweli ni kwamba kuna umuhimu wa kuangalia katiba yetu upya. mimi nadhani tatizo ni sisi wenyewe wananchi(tulio weng) hatujui hata katiba yetu ni nini na nini faida na hasara zake.
 
Tatizo letu ni kujifananisha na nchi nyingine, kuiga taratibu zao nusu nusu bila hata kuzingatia hali halisi ya nchi yetu.

Mfano uliouchukulia wa Muungano, nadhani una maana kubwa sana. Tulipobadili Katiba yetu na kuweka Mgombea mwenza, hatukuzingatia makubaliano ya Muungano na hasa nafasi ya Rais wa Zanzibar. Tulidhani tu kuwa kama tukiwa na Rais wa Muungano kutoka bara/Zanzibar na kuchukua mgombea mwenza kutoka upande wa pili tutakuwa tumemaliza matatizo yanayoweza kujitokeza. Kumbe ndio tumeyaanzisha.

Sasa Rais wa Zanzibar hana nafasi yoyote katika Muungano zaidi ya kuwa kwenye Baraza la Mawaziri (bila kuwa Waziri). Matatizo mengi ya Muungano yanaanzia hapo. Nadhani hofu ilikuwa kama Rais wa Zanzibar au Muungano akitoka chama tofauti na mwenzake wa upande wa pili inaweza kuwa vigumu kifanya kazi pamoja. Lakini hii haiwezi kuwa tatizo. Kwa maana kinachotakiwa ni kuweka bayana wajibu wa viongozi hao wawili katika kutekeleza majukumu yao.

Inatakiwa kubadilisha Katiba na kurudisha nafasi ya Rais wa Zanzibar kwenye serikali ya Muungano. Kama ni lazima kuwa na mgombea mwenza, basi kuwe na Makamu wa Rais wawili (Rais wa Zanzibar akiwa Makamu wa pili wa Rais).

Je unaona ni mfumo upi uta tufaa sisi?
 
Na pia nina wasi wasi na idadi ya wabunge wetu. Hivi majimbo yetu ya uchaguzi yana zingatia idadi ya watu na mahitaji yao? Au wenye mamlaka wana gawa tu majimbo kwa faida yao?
 
Jamani nina swali. Nime kuwa niki pitia na kuchangia kwenye thread moja hapa ihusuyo Diallo kumjia juu Mkullo. Sasa ika tokea kitu fulani ambayo nimeona yafaa kuanzishiwa thread. Je ni busara mbunge kuwa waziri kwa mfumo wetu wa siasa? Waziri anaweza kutumikia taifa na jimbo kwa wakati mmoja? Kazi ya mbunge ni kuisimamia serikali na kazi ya waziri ni kuitetea serikali sasa waziri ambae ni mbunge afanye lipi? Waziri hawezi kutumia nafasi yake kupendelea jimbo lake? Waziri ana muda gani wa kushugulikia jimbo lake? Mimi naona mfumo huu una walakini wana JF mnaonaje hili? Huu mfumo wetu wa kiasi kikubwa tumeuazima toka Britain, je kwao mfumo huo ume fanikiwa? Mfumo huo kwa kwetu ume fanikiwa? Je mfumo wetu una hitaji kuangaliwa upya ili kwenda na wakati na hali halisi ya nchi yetu?

ni lazima awe mbunge kwa sababu sheria za bunge uwezi kuingia bungeni kutoa hoja mpaka uwe member wa bunge sasa mwaswali ya kila siku wataulizwa na-ni na wanasiasa wenywe ndio wabunge.
 
sasa tunatokaje kwenye hili jamvi na mawazo yetu mazuri kuhusu katiba kwenda kuleta mabadiliko, ni wazi kuwa viongozi wa nchi wanajua tunachojadili lakini hawatutilii maanani kwani maneno yetu hayafuatiwi na vitendo,tumetoka mbali,nyezi,youngafrican,majira chatrooms .
 
Ni kweli mkuu lakini kabla ya kufanya mabadiliko lazima ujue unaenda kubadilisha nini. Ndiyo maana hapa tuna jadili kama mfumo uliopo unafaa au haufai. Kutokana na maoni na hoja za watu ndiyo tuta jua nini tufanye. Kama tukiona mfumo haufai sasa tuna jadili mfumo upi una faa. Tuki toka nje ya hapa kwenda kuleta mabadiliko lazima tuta ulizwa kwa nini tuna misimamo tuliyo nayo? Kwa hiyo kuongelea hapa ni mwanzo tu mkuu tupo kwenye njia kuelekea huko usemapo.
 
- Mfumo hauna tatizo, tusitafute excuses tatizo ni viongozi wenyewe hawana uwezo wa uongozi, wengi wao ukichunguza records zao za uongozi ni aibu tupu lakini wanapewa anyways, na hili halikuanza leo toka awamu ya kwanza tunapewa viongozi wasio na uwezo na wenye uwezo huishia kupigwa vita tu,

- Na sisi wananchi ndio kabisaa kazi yetu kualalamikia viongozi tunaowachagua wenyewe, mtu tunajua kwamba hafai lakini tunampa ubunge anyways, akipewa uwaziri tunaanza kulia amepewaje? Ni mara chache sana kukuta Rais amechagua kiongozi kwa ridhaa yake tu binafsi na kumchomeka mahali, siku zote huwa sisi wenyewe wananchi tunawachagua kwanza and then tunamlilia rais, oooh mdini, oooh anapendelea, oooh mtandao!

- Cheki this out, Lowassa, Karamagi, Msabaha, Rostam, Serukamba, Nchimbi na the likes hawa wote ni wabunge wa kuchaguliwa na sisi wananchi, sasa mfumo una kosa gani hapo? Tujaribu kuwamsha wananchi vijijini kuhusu elimu ya siasa ya taifa letu, ama sivyo hatutabadili chochote na wala hatuendi kokote itakua kelele za mlango, kiongozi mmoja mzito wa serikali ya sasa aliwahi kuniambia hayo makelele yenu JF hamuwawakilishi wananchi wote wa Tanzania, infact wengi wenu inaonyesha wako nje maana Tanzania huwa hatuongei lugha kama hizo zenu huko JF.

- Hata yakifanyika mabadiliko kama viongozi wetu bado ni hawa hawa ni kazi ya bure!

Respect.

FMEs!
 
Asante mkuu kwa maneno yako. Lakini je kama thread inavyo sema unaonaje mbunge kuwa waziri? hauoni mfumo huo una matatizo? hapo ndiyo haswa nahitaji maoni yako. Maana hata mfumo mbovu ina changia kuwepo kwa viongozi wabovu. So labda utuambie kama unaona mfumo wa mbunge kuwa waziri una faa au laa. After all nia ni kutafuta maoni ya watu. Sija sema nilicho kisema mimi ni sahihi ila nataka kujua na wengine wanaonaje
 
Heshima mbele kaka,

- To me, mfumo hauwezi kuwa mbovu kabla ya kupima viongozi wa huo mfumo, kwa sababu ni viongozi makini ndio matendo yao yanaibua ubovu wa mfumo, wewe umeuona mfumo kuwa ni mbovu sio through ubora wa viongozi tulionao sasa, in other words unawapa viongozi wa sasa a pass kwamba sio wabovu ila ni mfumo tu, ndipo ninapopata tatizo mkuu kukubali theory yako, mbovu sio mfumo ila ni viongozi wetu na sisi wananchi tunaowachagua, turekebishe hilo kwanza la uongozi mbovu!

- Kenya ni mfano mzuri na wa kuigwa sana, kwamba wananchi wameikataa serikali ya KANU yaani the CCM likes, lakini wamegoma kata kata kubadili mfumo, meaning kwamba walikuwa siku zote wakiamini kwamba ubovu uko kwenye uongozi sio mfumo wao, kwa sababu ni mfumo huo huo uliolishamirisha taifa lao, under Wakoloni na hata utawala wa Kenyatta.

Respect.

FMEs!
 
Kusema kweli mi nakubaliana kabisa na ES. Nimeona makampuni yakibadili organizations structures every now and then only ending up in the same problems. Kubadili uongozi mara nyingi imekuwa ndo suluhu! Uongozi kwanza, mfumo baadaye.

Tatizo letu ni viongozi wabovu, end of story! Ikiwa hao viongozi wabovu ndio tulio nao, ndio tulioweza kuzalisha so far, basi tutaendelea na matatizo yetu mpaka hapo tutakapozalisha viongozi bora.

Mfumo wa kutawala ni power map. Kiongozi mzuri huweza kufanya vema katika mfumo wowote. Katiba yetu inampa rais nguvu nyingi mno including kuubadilisha mfumo. Ikiwa rais wetu angeona mfumo uliopo mbovu anao uwezo mkubwa wa kuubadili kulingana na matakwa yake. Rais wa nchi yetu has only himself to blame.

Mwalimu aliwahi kusema katiba ya Tanzania inamruhusu rais kuwa dikteta. Ana uwezo wa kufanya chochote anachoona kitaleta matokeo mazuri. Rais ana uwezo wa kuwapunguza hao viongozi tunaolalamika ni wengi. Baraza la mawaziri ni discretion ya rais. In fact rais wa Tanzania anaweza kuamua kuweka baraza la mawaziri lenye mawaziri kumi tu. Na hao wote anaweza kuwaweka kutoka kwenye wabunge wa kuteua yeye mwenyewe.

Rais anaweza kuunganisha mikoa au kutenganisha mikoa ili iwe michache au mingi. Rais anauwezo wa kufuta wilaya na kuanzisha mpya. N.K.

Huwezi kusema mfumo ni mbovu ndo maana hatufanikiwi. Katiba yetu kwa kiongozi mzuri ni katiba bora kabisa kwani inampa flexibility ambayo haiko regulated by anybody or any organ. Kwa hiyo failure yetu blame lazima iende kwa viongozi wakuu kabisa, marais wetu. Marais wetu wameshindwa kutumia flexibility waliyopewa na katiba kuleta mabadiliko yanayotakiwa. Pengine la kujiuliza, je viongozi wetu wanashare the same sentiment kwamba we are not succeeding? Sidhani!

Sitaki mfumo ambao kiongozi wa nchi akiingia ataanza kulalamikia hiki na kile. Kwa mfumo wetu kiongozi wa nchi hana chochote cha kulalamikia. Ni yeye mwenyewe.

Cha kufanya ni kuhakikisha tunapata viongozi wazuri. Viongozi bora na wenye ubora usiokuwa na mashaka. Je wapo? Kizazi chetu kinawazalisha? Tunawaanda? Au tunasubiri wadondoke kwa nadra tu? Hizo ndo changamoto tulizo nazo.
 
Mawazo mazuri sana mkuu. Mimi nina machache yakusema, natumai utaelewa huu ni katika kuelewa zaidi. Swali la msingi la thread ni jee hii mbunge kuwa waziri haileta conflict of interest? Kwa maana mtu akiwa waziri atumikie taifa ua jimbo? Pia mtu akiwa waziri aka fanya vitu fulani jimboni kwake haita onekana upendeleo? Na je aki hudumia taifa akaiacha jimbo lake si ata kuwa kawa angusha wananchi? Wewe umebase sana kwenye uraisu lakini hauja jibu hoja ya kuwa mbunge kuwa waziri ina weza kuleta conflict of interest.

Cha pile ni kwamba je mfumo ukiwa mbovu hi siyo kichocheo cha kupata viongozi wabovu? Kama mfumo ni mzuri haita jenga mazingira ya walau kupata viongozi wengi wazuri hata kama siyo wote. Nakubaliana na wewe kama viongozi ni ovyo basi haki tendeki kitu lakini pia mfumo ukiwa mbaya basi kupata viongozi wazuri ni ndoto.

La tatu na la mwisho ni kwamba hauoni raisi ni tatizo? Je serikali yoyte kutokuwa na checks and balances halita leta tatizo? Umesema mwenyewe kuwa raisi anaweza kuwa hata dikteta. Kwa maana hiyo mayai yote tume weka kwenye kikapu kimoja, raisi akiwa ovya ndiyo basi tena tusha kula hasara. Kuwa na balance of power hauoni ni muhimu kuzuia raisi, mtu mmoja kuwa dikteta? Kwa ulivyo sema wewe basi raisi akiwa corrupt na serikali nzima ita kuwa corrupt.

Kama nilivyo sema mwanzo asante sana kwa maoni yako mkuu.
 
Mbunge wa kuchaguliwa na wananchi atawajibika kwa wananchi wa jimbo lake. Je akiteuliwa uwaziri ambapo anatakiwa kuwajibika kwa rais aliyemteua Ubunge wake utakuwaje?

La kujiuliza zaidi ni kuwa, je rais anawajibika kwa nani? Ikiwa rais anawajibika kwa wananchi, waziri vile vile atawajibika kwa wananchi. Suala hapa ni wananchi gani wa jimbo lake au wa nchi nzima?

Ndo maana nasema huwezi kujadili hili bila kujadili package nzima. Yaani ikiwa mbunge ameteuliwa kuwa waziri, kazi yake ya uwaziri itatawaliwa na utekelezaji wa sera za serikali inapokuja suala la kuleta maendeleo. Kwanza tukubaliane maendeleo hayaletwi na serikali. Maendeleo huletwa na watu. Mbunge kama muwakilishi analo jukumu la kulobby serikalini kuhakikisha eneo lake linapewa kipaumbele inapokuja kwenye vitu vinavyosaidia kupush maendeleo kama miundo mbinu yaani bara bara, maji, umeme, n.k. Je anapokuwa waziri uwezo wake wa kulobby kwa ajili ya jimbo lake umepunguzwa au umeongezwa? Umeongezwa, hivyo kwa wanajimbo hii ni plus. Lakini kwa nchi nzima je?

Sasa hapa tunajadili mbunge waziri. Je hakuna mkabala wa maslahi katika kulitetea jimbo lake kama mbunge, na kutekeleza sera za serikali kama waziri? Ni kweli kuwa utendaji wa kazi kama waziri utamtaka aangalie picha kubwa zaidi, yaani nchi nzima. Hapa ndo linapoingia suala la urais. Anapotekeleza majukumu yake kama waziri anawajibika kwa rais.

Ikiwa kweli rais ni wa watu wote na anawajibika kwa wananchi wote suala la mbunge waziri kutekeleza vipaumbele vya serikali haliwezi kuleta mgogoro. Wananchi wa jimbo lake hawawezi kulalamikia kupokwa muwakilishi wao na serikali kwani uwezo wake wa kulitetea jimbo umeongezeka. Sasa jee huyu waziri hataweza kulipendelea jimbo lake tuu ukizingatia kuwa watu wa jimboni kwake ndo wanaompa kura za kurudi serikalini (kwani akikosa kura na uwaziri basi)?

Hili litajibiwa na uongozi mzima. Rais akiwa mkuu wa serikali anayewajibika kwa wananchi wote anao wajibu wa kuwa na vipaumbele vya kitaifa ambavyo kutekelezwa kwake husimamiwa na mawaziri. Vipaumbele vya kitaifa vinaweza visiwe kwenye vipaumbele vya jimbo moja moja. Lakini vile vile ni wajibu wa serikali kuhakikisha majimbo yanajua kuwa yenyewe ni sehemu ya Taifa kubwa. Hapo ndipo linapokuja suala la uongozi bora. Uongozi bora unaosimamia masuala yote ya kitaifa kwa vipaumbele kama inavyotakiwa uta-galvanize public trust. Kukiwa na public trust suala la utendaji wa mbunge mmoja mmoja haitakuwa issue. Mafanikio ya serikali yatapimwa kwa jinsi ambavyo imeweza kushughulikia vipaumbele vya kitaifa. Hata kama havitakuwa na matokeo ya moja kwa moja kwa jimbo la mhusika bado hakuna tatizo hapo.

Tatizo linakuja pale ambapo vipaumbele vya kitaifa vimemezwa na udhaifu mkubwa uliomo ndani serikali kiasi cha watu kuamini kuwa bila kuwa na muwakilishi serikalini hakuna kitakachoendelea katika majimbo yao. Hapo ndipo tulipofika. Lakini sasa tukishafika hapo, muwakilishi bungeni hana maana, kwa sababu Bunge halitekelezi vipaumbele. Muwakilishi serikalini ndo anakuwa na maana zaidi.

Kwa kifupi ni kuwa, ikiwa serikali inasimamia na kutekeleza vipaumbele vya kitaifa, whether jimbo lina uwakilishi wa moja kwa moja Bungeni, Au mbunge wao amekuwa waziri haitakuwa na matatizo kwani serikali yenye ufanisi lazima itafika kama si leo kesho.
 
Kikao cha Bunge

Vuguvugu la maandalizi ya uchaguzi mkuu mwakani linaendelea kushika kasi, huku zikijionyesha dalili za wazi kwa baadhi ya wanasiasa wakijaribu kuvutia kamba upande wao ili wachaguliwe.

Katika kikao cha Bunge la bajeti kinachoendelea mjini Dodoma, kila mbunge anayepata nafasi ya kuzungumza anajitahidi kuelezea kero za jimboni kwake ambazo serikali iliahidi kuzitekeleza kipindi cha nyuma lakini hadi sasa hazijatekelezwa.

Katika hatua fulani, imetokea hata baadhi ya wabunge kuwashambulia mawaziri kwa kushindwa kupatia ufumbuzi kero mbalimbali na hasa miradi ya maendeleo majimboni mwao.

Pia wengine wakionyesha dhahiri kwamba maeneo yao yamesahauliwa huku mengine yakionekana kupendelewa zaidi katika kutatuliwa kero zake.

Kwa kumaliza tatizo hili la upendeleo, Mbunge wa Ilemela, Anthony Diallo(CCM), wiki hii ametoa ushauri ambao tunadhani ipo haja kwa serikali kuutafakari na kuona kama ukitekelezwa utapunguza au kuondoa kabisa malalamiko ya wananchi.

Mheshimiwa Diallo amemshauri Rais Jakaya Kikwete kuangalia uwezekano wa kuacha kuteua wabunge kuwa mawaziri.

Akasema kuwa uteuzi huo unasababisha baadhi ya mawaziri kupendelea majimbo wanayowakilisha kibunge.

Bila kutaja majina, alisema kuwa baadhi ya mawaziri wameonyesha kubadili mfumo na kupanga miradi kulingana na vipaumbele na kujichomekea miradi katika maeneo yao.

Kama hiki anachosema mheshimiwa huyu ni kweli kinatokea, hakika viongozi wetu wanaelekea kusiko kwani hizi ni dalili mbaya zinazoashiria matabaka kimaendeleo.

Tukiendekeza tabia hii, nchi yetu itajikuta imejigawa ambapo yatakuwepo maeneo yenye barabara nzuri sana huku mengine wakibaki na barabara mbovu na hivyo kuzidi kudidimia kimaendeleo.

Au maeneo mengine yatakuwa na shule nzuri na nyingi, zahanati nyingi huku mengine wananchi wake wakitegemea mitishamba kuokoa maisha yao.

Tunakubaliana na mheshimiwa Diallo kwamba ipo haja kwa serikali kutizama upya jambo hili la wabunge ambao pia ni mawaziri ili kuondoa dhana hiyo ya upendeleo ambao umeanza kujionyesha wazi.

Kwa wabunge ambao ni mawaziri, wanapokwenda jimboni hujitutumua zaidi na kuonyesha wananchi kuwa wanao uwezo mkubwa wa kusukuma maendeleo katika eneo lao kwa kutumia cheo cha uwaziri.

Athari ambayo inaweza kujitokeza hapa ni kwamba endapo atajitokeza mgombea ambaye siyo waziri, uwezekano wa kushinda utakuwa mdogo kwa kuwa waziri atawashawishi wapigakura kwa kupeleka miradi mingi.

Swali ni je, wale wengine wenye uwezo wanaojitokeza kugombea, kwa mtindo huo watachaguliwa?Hii haina tofauti na kiongozi wa serikali ambaye pia ni mfanyabiashara.

Kama ni waziri na wakati huo huo ni mfanyabiashara, kwanini asitumie ofisi yake kutoa vipaumbele kwa miradi yake ya biashara?

Kama kweli tunataka dhana ya utawala bora iliyodhamiria kutoa huduma sawa kwa wote idhihirike, ni muhimu mambo haya yakatenganishwa ili raslimali za nchi yetu ziwanufaishe wote bila upendeleo.

Mbunge abaki kuwa mbunge na waziri abaki kuwa waziri. Hali kadhalika, kiongozi wa umma abaki kuwa kiongozi na siyo mfanyabiashara.

Ni matumaini yetu kwamba, yanayojitokeza hivi sasa kama alivyotoa dokezo Mheshimiwa Diallo, yataangaliwa kwa mapana na kuona namna sahihi ya kuyashughulikia mapema kabla hayajatupeleka mahali pabaya huko tuendako.

Na zaidi ya yote, tuondokane na mfumo huu tuliorithi toka kwa wakoloni ambao unaelekeza kwamba serikali inaundwa ndani ya Bunge, kwa maana kwamba mawaziri wanatokana na wabunge.

Kwamba mtu hawezi kuwa waziri hadi kwanza awe mbunge bila kujali kama ni mbunge wa jimbo ama wa kuteuliwa na rais au kutokana na viti maalum.

Pengine baada ya athari ambazo zimeanza kujitokeza sasa, tubadilike kulingana na wakati uliopo na hasa kwa kuangalia kule tuendako.

Kama mfumo huo umeanza kuleta manung’uniko, basi tuachane nao na kuelekeza nguvu zetu katika kutenganisha maeneo hayo.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Back
Top Bottom