MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,565
- 836
Jamani nina swali. Nime kuwa niki pitia na kuchangia kwenye thread moja hapa ihusuyo Diallo kumjia juu Mkullo. Sasa ika tokea kitu fulani ambayo nimeona yafaa kuanzishiwa thread. Je ni busara mbunge kuwa waziri kwa mfumo wetu wa siasa? Waziri anaweza kutumikia taifa na jimbo kwa wakati mmoja? Kazi ya mbunge ni kuisimamia serikali na kazi ya waziri ni kuitetea serikali sasa waziri ambae ni mbunge afanye lipi? Waziri hawezi kutumia nafasi yake kupendelea jimbo lake? Waziri ana muda gani wa kushugulikia jimbo lake? Mimi naona mfumo huu una walakini wana JF mnaonaje hili? Huu mfumo wetu wa kiasi kikubwa tumeuazima toka Britain, je kwao mfumo huo ume fanikiwa? Mfumo huo kwa kwetu ume fanikiwa? Je mfumo wetu una hitaji kuangaliwa upya ili kwenda na wakati na hali halisi ya nchi yetu?