Hoja ya Udikteta wa Magufuli: Tundu Lissu isn't Right. Haupingwi kwa kupaza sauti kupiga tu Kelele!

Hoja ya Udikteta wa Magufuli: Tundu Lissu isn't Right. Haupingwi kwa kupaza sauti kupiga tu Kelele!

Kwa sasa mahakama kuu ya Tanzania sio Taasisi huru,majaji wanaingiliwa kwenye shughuli zao mpaka wanaamua kujiuzuru,

Na kama mahakama inaingiliwa kwenye kutenda haki,haki zetu tuzitafutie wapi?je kuna haja ya kupeleka kesi mahakamani katika hali hii au tuangalie namna nyingine? Kama unazizuia mahakama zisitupe haki,na sisi kama nchi tunataka haki na tumekubaliana kikatiba tutaipata mahakamani,na wewe umezizuia mahakama zisitoe haki,nchi nzima ikiamua kutafuta mbadala wa mahakama nchi hii itakalika?

Wabunge bungeni mnawafukuza na kuwatisha,mnataka taifa lisemee wapi? Bunge ni mahala pa mijadala ya taifa,wakianza kujadili mnawafukuza na kuwatisha

Serikali nayo ikisikia watu wanatumia Uhuru wao kujadili,wanatuma polisi kuwakamata

Kuna kihadithi fulani kinasema kwamba hata umuwekeee vifaranga mia,ukimuachia tu,mwewe atapaa na kuondoka,Uhuru ni kitu cha asili cha binadamu,

Mkoloni na mabomu yote na mabunduki,hakufanikiwa kumnyamazisha Nyerere,kenyata,Mandela,Mugabe,

Leo karne ya 21 unawaza kuzuia watu wasiongee?

Wapinzani waliongea tena kwa ruksa na kukingiwa kifua na Nyerere baada ya tume ya Nyalali,

Leo wewe ni nani wa kumshinda Nyerere busara? Wewe unaweza kumshinda baba wa taifa kwa maono? Ccm walikataa vyama vingi,Nyerere akawaambia acheni ujinga,na wakati Mkapa anaomba urais,nyerere hakuzuia wapinzani wasipige kampeni,alisema muacheni Lyatonga mashabiki wake wamsukume gari lake,mrema yuko mwanza kwenye kampeni ,nyerere yuko mbeya,hakuamuru lyatonga akamatwe

Mtoto wa Nyerere alikuwa NCCR,Nyerere wala hakuumia kichwa... Leo hii unataka kufukia jalalani busara za Nyerere? Kwa ugwiji upi wa kisiasa ulio nao?

Mwinyi alitaka kuleta Tanganyika,Nyerere akamwambia ilani tuliyokupa haina hiyo hoja,umeitolea wapi? Leo ilani INA hoja ya mimba za wasichana,unaikataa,kwa hiyo kwenye kampeni mlikuwa mnawadanganya watu? Ccm itwambie kwamba ilani yao iko kichwani kwako au wana kitabu maalum cha ilani kinachoongoza mambo mbalimbali ikiwemo Uhuru wa mahakama
Umeongea mambo ya msingi mno, lakini hutaeleweka na walio wengi kwasababu hii nchi inawajinga wengi sana,ujinga unakuja pale walio wengi wanapoongozwa na mihemko badala ya akili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lissu ameshaiona hatari ya kutorudi bungeni 2020. Anajaribu kujidhatiti kimkakati zaidi, bahati mbaya mbinu anayojaribu kuitumia haina manufaa sana, binafsi ningelikuwa Lissu ningejikita jimboni kwangu zaidi kuliko kupoteza mda kwenye media ambazo kwa hakika wananchi wa Singida Mashariki hawatamwelewa. Watanzania wengi hasa vijijini wanachotaka ni kuona shughuli za maendeleo zikifanywa bega kwa bega na mbunge wao, kama afanyavyo profesa Jay wamitulinga kuliko huu upuuzi wa kwenye media wa huyu wakili msomi wa chadema.

Lissu apambane na ukanda na ukabila uliopo kwenye chama chake kwanza ndoo amseme magufuli,maana hata dada yake alichaguliwa viti maalumu chadema kama sikosei.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe binafsi huna uwezo hata wa kujishauri ndio sembuse umshauri Lisu mtu mwenye akili nyingi ambazo nyinyi mkijijumrisha ukoo wenu mzima hamfikii IQ yake hata robo?
 
Lissu ameshaiona hatari ya kutorudi bungeni 2020. Anajaribu kujidhatiti kimkakati zaidi, bahati mbaya mbinu anayojaribu kuitumia haina manufaa sana, binafsi ningelikuwa Lissu ningejikita jimboni kwangu zaidi kuliko kupoteza mda kwenye media ambazo kwa hakika wananchi wa Singida Mashariki hawatamwelewa. Watanzania wengi hasa vijijini wanachotaka ni kuona shughuli za maendeleo zikifanywa bega kwa bega na mbunge wao, kama afanyavyo profesa Jay wamitulinga kuliko huu upuuzi wa kwenye media wa huyu wakili msomi wa chadema.

Lissu apambane na ukanda na ukabila uliopo kwenye chama chake kwanza ndoo amseme magufuli,maana hata dada yake alichaguliwa viti maalumu chadema kama sikosei.

Sent using Jamii Forums mobile app

LISSU HATA AKISHINDA KWA ASILIMIA 100 JIMBONI MAGUFULI ATAMPOKONYA...KILA MTU ANALIJUA HILO
 
LISSU HATA AKISHINDA KWA ASILIMIA 100 JIMBONI MAGUFULI ATAMPOKONYA...KILA MTU ANALIJUA HILO
Sikatai hoja yako lakini pia Lissu analalamikiwa sana kutofika jimboni kwake kuhamasisha maendeleo, amekalia kesi na kuutetea umma wa Watanzania kwa ujumla wake kama adaivyo yeye, jimboni hayo hawayajui wanataka shughuli za maendeleo zionekane zikifanywa na kuhimizwa na mbuge wao. Atanyolewa 2020 mubaki kusema, KAKATWA.
 
Lisu alitaka Urais wa TLS, alizani sijui atafanya jipya gani, na Ubunge anao pia.. Atatamani kila cheo cha Nchi hii ili awe mzungumzaji wa kila jambo katika nchi
 
Wanabodi,

Declaration of Interest, mimi Paskali, sio mwanachama, mshabiki au mfuasi wa chama chochote cha siasa, bali hoja zangu zote hutanguliza mbele maslahi ya taifa kwa kuzitoa truthfully, with objectivity, impartiality na balance. Kwa vile watu humu wana vyama vyao na viongozi wao ambao wengine wana waabudia, hivyo nakijua fika kinachomfika mtu atakayepandisha hoja, kuwapinga waabudiwa wao!. Wajemini haya ni maoni na mtazamo wangu tuu and not necessarily I must be right, hivyo Mhe. Tundu Lissu might be right and I might be wrong!.

Naomba nianze kwa kumpongeza Mhe. Tundu Lisu Kwa kutokuwa muoga kuizungumzia dhana ya udikiteta Tanzania bila uoga, japo the way anavyoielezea anazungumza kwa style ile ile ya uropokaji, the Magufuli style, hivyo kuonekana kama insane fulani, lakini ujumbe umefika.

Kwanza naomba kukiri kuwa mimi Paskali sio mwanasheria, Mhe. Tundu Lisu ni mwanasheria, hivyo mimi nazungumza kama a layman, na Tundu Lisu, japo kwanza mwanasheria kisha ndipo akawa mwanasiasa, mtu kuwa mwanasheria hakukufanyi always kuwa right, na mtu just a layman, anaweza kabisa kutofautiana na mwanasheria mbobezi na akawa right, mfano ni huu
Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele! | Page ...

Katika jinsi ya kupinga udikiteta Tanzania, Tundu Lisu ametuasa tupaze sauti zetu kuupinga huu udikiteta kwa kupiga kelele ambako huku ni kuipinga kisiasa, wakati hoja halisi ya udikiteta, sio hoja ya kisiasa ni hoja ya kisheria. Hoja za kisiasa zishughulikiwe kisiasa, na hoja za kisheria, zishughulikiwe kisheria. Kushughulikia kisiasa kwa hoja za kisheria, ni kujifurahisha tuu, kamwe hakutaleta matokeo yoyote chanya.

Naomba kutofautina na Mhe. Tundu Lisu katika hili la udikiteta, kwa hoja kuwa udikiteta haupingwi kwa Press Conference, kwa maandamano, kwa mikutano ya hadhara, kwa kupaza sauti na kupiga kelele.

Udikiteta unapingwa kwa njia moja tuu, Court Review kupitia Mamlaka ya Mahakama Kuu kutoa kitu kinachoitwa Prerogative orders ziko 6, ila maarufu zaidi ni 3. (
  • certiorari, an order by a higher court directing a lower court to send the record in a given case for review;
  • mandamus, an order issued by a higher court to compel or to direct a lower court or a government officer to perform mandatory duties correctly;
  • prohibition, directing a subordinate to stop doing something the law prohibits;
  • habeas corpus, demands that a prisoner be taken before the court to determine whether there is lawful authority to detain the person;
  • quo warranto, requiring a person to show by what authority they exercise a power.
  • procedendo, to send a case from an appellate court to a lower court with an order to proceed to judgment) mtanisamehe sizijui Kiswahili chake.
Hivyo Lisu kama mwanasheria mbobezi, Mwenyekiti wa TLS na Mwanasheria Mkuu wa Chadema alipaswa kwanza kutumia the legal local remedies available, kwanza kuuthibitisha huo udikiteta, zikishindikana ndipo sauti zipazwe ili kusaidiwa na jumuiya ya kimataifa.

Udikiteta wa Magufuli Ulianza Lini?.
Kuna wengi humu wanaousikia udikiteta wa Magufuli wakidhani umeanza leo, no!, kuna aina mbili za vyanzo vya udikiteta na aina mbili za udikiteta.
Vyanzo vya udikiteta ni
1. Hulka ya Udikiteta nimeizungumza hapa -
Yajue Makundi 10 Top Ten wa CCM, Ambamo Watatoa Top 5, Top 3 na ...

2. Mazingira ya Udikiteta nimeyazungumza hapa
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...

Aina za udikiteta
1. Udikikiteta Katili nimeuzungumza hapa-
Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta Katili ...

2. Udikiteta Uzalendo nimeuzungumza hapa-
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...

Jee ni Kweli Tanzania Tuna Udikiteta?.
Hili ndilo swali kuu la msingi la kujiuliza, jee ni kweli Tanzania tuna udikiteta?.
Hili nimelizungumzia hapa
Udikiteta ni Dhana Tuu or ni Real?. "Lets Call A Spade A Spade ...
Udikiteta: Uongo Ukisemwa Sana na Kuachwa Bila Kukanushwa Hugeuka ...

Udikiteta wa Vyama: CCM ni chama cha Kidikiteta, Ila pia Chadema ni Chama cha Kidikiteta.
Udikiteta wa vyama ni jinsi vyama vinavyoendesha mambo yake, haswa wakati wa uchaguzi wa viongozi wake, vyama karibu vyote vinahubiri demokrasia, lakini vinaendeshwa kidikiteta.
Udikiteta wa CCM katika uchaguzi wa viongozi wake, nimeuzungumza hapa
Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC! | Page 9 ...

Kwenye hili la udikiteta, hata Chadema hawana demokrasia hiyo wanayoihubiri, tena kuna hatari, hata kama ni Chadema wengeshinda uchsaguzi wa 2015, wangeweza kuendesha nchi hii kwa udikiteta wa ajabu kuliko hata huu tunaoushuhudia sasa. Hili nililiona na nililizungumza hapa
CHADEMA Ikipewa Nchi, October 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala ...

Chadema na Matumizi ya Busara: Chama Cha Kiharakati, Hakiwezi Kupewa Nchi Kutawala!.
Chadema kuna tatizo kubwa la matumizi ya busara katika kauli za baadhi ya viongozi wake. Unaweza kukosoa kwa lugha ya kistaarabu na kwa unyenyekevu ukafikisha ujumbe vizuri zaidi kuliko kutumia lugha kali, machukizo, matukano na lugha isiyo ya staha. Wakati tukielekea uchaguzi wa 2015, tulishauri humu, ili Chadema kiweze kuaminiwa na kukabidhiwa nchi, ni lazima kionyeshe ukomavu, maturity, kufuatia kwa muda mrefu Chadema kujitanabaisha kama ni chama cha kiharakati, tulishauri Chadema kujibadili kutoka chama cha kiharakati, kuwa chama tawala chenye uwezo wa kuongoza nchi.
CHADEMA: Tujadili Utayari wa Kutawala Nchi 2015 | Page 7 ...
Kuelekea 2015: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If ...

Hata walipounda UKUTA, akina sisi tuliwashauri humu
Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane ...

A Way Forward Kuelekea 2020, Kwa Kwa Udikiteta Huu Uliopo, na Siasa Hizi za Chadema, Do They Stand A Chance?.
Naomba kuwasilisha.
Hakuna kitu kigumu kukizungumza humu jf kama ukweli mchungu!, wengi wetu humu wataanza kuizungumzia 2020 on 2019, by that time it will be too little too late!, sisi waona mbali, tunaizungumzia 2020 sasa, ili kutoa muda wa gestation period ya kujipanga and to do something worthwhile before its too late.
CHADEMA Hamkujipanga, hamjajipanga, hamjipangi na hamtajipanga ...
Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible ...
CHADEMA Chama cha Ajabu Sana!.Kwenda Mahakamani Kwa Non Issue ...

Kwa siasa hizi Chadema inazokwenda nazo, kwenye mazingira ya udikiteta huu uliopo, kama hawatabadilika, I'm very sorry to say....
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020 ...

Je, Kasi ya Magufuli itaua Upinzani Uchwara na Kuimarisha Upinzani ...

In 2015 Election, Tanzania had A Choice To Choose From. Jee Kwa ...

Paskali
Rejea Kuhusu Udikiteta.
Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia ...

Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...

Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The ...

Je, Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya ...

Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote | Page ...

Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais ..

Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na ...

Rejea Kumhusu Tundu Lisu
Vurugu za Bungeni: Mhe.Tundu Lissu, Anastahili Adhabu Kali?!. Ni ...
Mhe. Tundu Lissu, Please Acha Kumsulubu Spika Wetu!, Unammaliza ...
Usiyoyajua Kuhusu Nyerere: Shuleni Alikuwa Toto Tundu!, Almanusura ...
Kazi nzuri Tundu Lissu Antipas! | Page 10 | JamiiForums | The Home ...
Swali la Kizushi: Kwa Nini Job Ndugai Anamuogopa Tundu Antipasi ...
Opinion: Kung'atuka Kwa Zitto, CHADEMA, Msishangilie, Mkajisahau ...

Paskale mara nyingi uwa nakukubali ila kwa ili hauko sahihi.
SA, Mozambique, Angola, Zimbabwe, Namibia, South Sudan, Rwanda, Russia, Bosnia, Brazil, Venezuela etc walifanyaje?
 
LISSU HATA AKISHINDA KWA ASILIMIA 100 JIMBONI MAGUFULI ATAMPOKONYA...KILA MTU ANALIJUA HILO
Tusimpe Magufuli nguvu ambazo hana. Usidhani kama ccm majimbo yaliyochukuliwa na upinzani waliyatowa kama sadaka.

Mkilegea kulinda kura na kusimamia majumuisho hata Bashite anatosha kabisa kuwapora ushindi kwa kutumia Polisi na hawa wakurugenzi.

Msinyeke kiasi hicho, 2020 ingieni kwenye uchaguzi na Do or die, na jino kwa jino style, otherwise kaeni kimya acheni ccm wafanye yao.

Sipendezwi na watu kumpa Magufuli nguvu ambazo hana, mkiendelea na mawazo haya ni kweli atajipachika nguvu hizo.

Umeshamkia kuwaza hata kutembelea Keybeat?
 
Sikatai hoja yako lakini pia Lissu analalamikiwa sana kutofika jimboni kwake kuhamasisha maendeleo, amekalia kesi na kuutetea umma wa Watanzania kwa ujumla wake kama adaivyo yeye, jimboni hayo hawayajui wanataka shughuli za maendeleo zionekane zikifanywa na kuhimizwa na mbuge wao. Atanyolewa 2020 mubaki kusema, KAKATWA.

acha kuongea vitu usivyovijua.....Wewe unaambiwa sisi tunaishi huko....Lissu anapendwa sana Jimboni....ameondoa bughudha nyingi sana kwa wananchi.....

Mwaka 2015 lissu hakupiga kampeni kabisa
 
Tatizo la mayala Ni mtu ambaye huwezi jua anasimamia upande gan . Ni mjanjamjanja hataki kumuudhi mtu kwa hiyo anakua katikati.
 
Wanabodi,

Declaration of Interest, mimi Paskali, sio mwanachama, mshabiki au mfuasi wa chama chochote cha siasa, bali hoja zangu zote hutanguliza mbele maslahi ya taifa kwa kuzitoa truthfully, with objectivity, impartiality na balance. Kwa vile watu humu wana vyama vyao na viongozi wao ambao wengine wana waabudia, hivyo nakijua fika kinachomfika mtu atakayepandisha hoja, kuwapinga waabudiwa wao!. Wajemini haya ni maoni na mtazamo wangu tuu and not necessarily I must be right, hivyo Mhe. Tundu Lissu might be right and I might be wrong!.

Naomba nianze kwa kumpongeza Mhe. Tundu Lisu Kwa kutokuwa muoga kuizungumzia dhana ya udikiteta Tanzania bila uoga, japo the way anavyoielezea anazungumza kwa style ile ile ya uropokaji, the Magufuli style, hivyo kuonekana kama insane fulani, lakini ujumbe umefika.

Ukweli Mchungu wa 2020.
Hakuna kitu kigumu kukizungumza humu jf kama ukweli mchungu!, wengi wetu humu wataanza kuizungumzia 2020 on 2019, by that time it will be too little too late!, sisi waona mbali, tunaizungumzia 2020 sasa, ili kutoa muda wa gestation period ya kujipanga and to do something worthwhile before its too late.
CHADEMA Hamkujipanga, hamjajipanga, hamjipangi na hamtajipanga ...
Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible ...
CHADEMA Chama cha Ajabu Sana!.Kwenda Mahakamani Kwa Non Issue ...

Kwa siasa hizi Chadema inazokwenda nazo, kwenye mazingira ya udikiteta huu uliopo, kama hawatabadilika, I'm very sorry to say....
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020 ...

Je, Kasi ya Magufuli itaua Upinzani Uchwara na Kuimarisha Upinzani ...

In 2015 Election, Tanzania had A Choice To Choose From. Jee Kwa ...

Paskali
Rejea Kuhusu Udikiteta.
Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia ...

Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...

Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The ...

Je, Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya ...

Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote | Page ...

Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais ..

Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na ...

Rejea Kumhusu Tundu Lisu
Vurugu za Bungeni: Mhe.Tundu Lissu, Anastahili Adhabu Kali?!. Ni ...
Mhe. Tundu Lissu, Please Acha Kumsulubu Spika Wetu!, Unammaliza ...
Usiyoyajua Kuhusu Nyerere: Shuleni Alikuwa Toto Tundu!, Almanusura ...
Kazi nzuri Tundu Lissu Antipas! | Page 10 | JamiiForums | The Home ...
Swali la Kizushi: Kwa Nini Job Ndugai Anamuogopa Tundu Antipasi ...
Opinion: Kung'atuka Kwa Zitto, CHADEMA, Msishangilie, Mkajisahau ...

pascal Mayallla habari za siku nyingi sana mkuu. Bila shaka umemaliza maonyesho ya sabasaba na wale mabinti wawili wamekuachia sasa unaweza kurudi JF kujifunza siasa japokuwa upo jukwaani.

Kama hiki unachotaka kumshauri Mh. Tundu Lissu unakiamini ulipaswa kuwa wa kwanza kukifanya, vinginevyo utakuwa unaendeleza unafiki ule ule wa siku zote na pengine this time utakuwa unaonyesha unafiki wa "kiwango cha lami".

Siku Raisi JPM alipokutana na wahariri Ikulu nawe ulikuwa mmoja wao na ukapata fursa ya kumuuliza maswali mawili juu ya ukiukwaji wa sheria na katiba anaoufanya lakini akaishia kukujibu kuwa Mayalla kwa kikwenu (wewe na yeye) ni njaa, wala hakujibu maswali yako.

Baada ya kupata majibu hayo yasiyoendana na swali lako uliishia kucheka cheka tu na wala hukuchukua hatua yoyote kati ya hizi unazojaribu kuaminisha watu kwamba ndio njia sahihi, badala yake umemsubiri Mh. Tundu Lissu amezungumza ndipo unakuja kutafutia "kick" ili kuwafurahisha hao jamaa wa upande wa pili, bila shaka unaogopa kunyimwa matangazo sabasaba ijayo...!!!

Kwa leo haya yanakutosha.
 
Mwana bodi.

Nimesoma ujumbe wako ulioutoa dhidi ya tundu lissu, na umetoa maoni yako kwamba Mh Tundu lissu amekosea approach aliyoitumia kataika kupinga udikteita.

Umetoa utaratibu unaotakiwa kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria ili kupinga udikteita Mahakamani, sas basi ni ama umekosea makusudi au umepitiwa kidogo katika kutoa mtazamo wako,Hivi ni katika mazingira gani Dikteita anakuwepo then mifumo mingine kama mahakama bado ina-function fully free from intervention? Katika tawala za kidiktaita Mtu mmoja ndo anakuwa Judge and jury, Kwahiyo basi ni wazi huwezi kwenda katika mfumo wa sheria mahali ambapo sheria haipo. no longer at ease my friend
 
Kaka yangu Pascal ninae kuheshimu sana kwenye hi tasnia ya habari, naomba nikusahihishe kidogo. NI kweli unaweza kua huna KADI ya chama chochote cha siasa (hata mimi sina pia na sijawahi kua nayo) but the truth is, kila mtu anao upande kwenye hivi vyama, is either unashabikia ccm kimtindo au upinzani na hasa Chadema au Cuf ya Maalim Seif, kusema huna upande hiyo sio kweli, nakataa brother.
Kuhusu uliyoyaongea, let kina Tundu and the co wajifunze.
 
pascal Mayallla habari za siku nyingi sana mkuu. Bila shaka umemaliza maonyesho ya sabasaba na wale mabinti wawili wamekuachia sasa unaweza kurudi JF kujifunza siasa japokuwa upo jukwaani.

Kama hiki unachotaka kumshauri Mh. Tundu Lissu unakiamini ulipaswa kuwa wa kwanza kukifanya, vinginevyo utakuwa unaendeleza unafiki ule ule wa siku zote na pengine this time utakuwa unaonyesha unafiki wa "kiwango cha lami".

Siku Raisi JPM alipokutana na wahariri Ikulu nawe ulikuwa mmoja wao na ukapata fursa ya kumuuliza maswali mawili juu ya ukiukwaji wa sheria na katiba anaoufanya lakini akaishia kukujibu kuwa Mayalla kwa kikwenu (wewe na yeye) ni njaa, wala hakujibu maswali yako.

Baada ya kupata majibu hayo yasiyoendana na swali lako uliishia kucheka cheka tu na wala hukuchukua hatua yoyote kati ya hizi unazojaribu kuaminisha watu kwamba ndio njia sahihi, badala yake umemsubiri Mh. Tundu Lissu amezungumza ndipo unakuja kutafutia "kick" ili kuwafurahisha hao jamaa wa upande wa pili, bila shaka unaogopa kunyimwa matangazo sabasaba ijayo...!!!

Kwa leo haya yanakutosha.
Tundu Lissu nilianza kukosa imani naye baada ya kuona anampuuza Baba wa Taifa na kumkashifu Rais aliyeko madarakani. Pale nikajua ana dosari kichwani na amekosa uungwana na weledi kwa kuwa hata Mbowe na Lowassa( aliyemuweka kwenye orodha ya Mafisadi zama zile siku zote anawalamba viatu na hajawahi kuwashambulia! Nikashangaa kama anaelewa maana ya Mamlaka!
 
Back
Top Bottom