Hoja ya Tundu Lissu yaigawa NCCR bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja ya Tundu Lissu yaigawa NCCR bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Relief, Nov 14, 2011.

 1. Relief

  Relief JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wabunge wa Chama cha NCCR Mageuzi wamegawanyika bungeni jioni ya leo baada ya hoja ya Mh.Tundu Lissu.
  Baada ya hoja hiyo, wabunge David Kafulila wa Kigoma Kusini na Felix Mkosamali wa Muhambwe wameungana na wabunge wa CHADEMA kutoka nje huku wabunge Agripina Buyogela na Mosses Machali wamebaki ndani kushirikiana na CCM (MAGAMBA) katika mjadala unaoendelea.

  Ni wazi ya kuwa kubaki kwa wabunge hao wawili wa NCCR Mageuzi ndani ya Bunge kujadili jambo ambalo wabunge wenzao wa Upinzani wanalipinga kunadhihirishia Umma jinsi gani wao ni CCM-B na huenda uamuzi wao huo ni maelekezo ya Bw. James Mbatia ambaye huyu ndugu yetu Machali anamtetea muda wote na kuwalaani wenzie kuwa wanakosea kumwondoa madarakani.

  Mgawanyiko huu unaleta maswali juu ya wabunge hawa wa upinzani hususan NCCR Mageuzi;
  1. Je inawezekana kweli upinzani unatumiwa na MAGAMBA kuleta mpasuko Bungeni kwa faida yao na si ya Umma?
  2. Je, hali hii iliyojionyesha mapema ya kufarakana kwa NCCR katikati ya mchakato wa kuelekea Katiba Mpya na vyama vingine vya upinzani (TLP na CUF) kukubaliana na CCM juu ya MUSWADA wa Katiba ambao hauonyeshi dhamira ya dhati ya upatikanaji wa TUME adilifu kusimamia uundwaji wa KATIBA MPYA utatupatia KATIBA tunayoitazamia?
  3. Tutarajie Tanzania gani baada ya mchakato huu kuisha?
  Wana jamii naomba kuwasilisha!

   
 2. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nani ateue tume?
   
 3. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Aibu yao, aibu ya magamba...
   
 4. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Matukio kama haya yanatusaidia kujua wapinzani na CCM B. Dr Mrema kabwabwaja mpaka akamwita Speaker 'mh. Mungu' wakati wenzake wametoka, tutamuita huyu mpinzani kweli?

  Huyo Machali nae ni walewale, kibaraka wa mkt wake Mbatia, kazua mjadala hapa JF wa kwamba Zitto na Kafulila wanataka kuivuruga NCCR wanajamvi nao bila kuchambua mambo kiundani wakaweka chuki mbele na kumshambulia Zitto. Uzuri wa unafiki huwa unaumbuka ndani ya muda mfupi tu.

  Big up CDM, msikubali kuburuzwa bungeni, maoni yenu muhimu kwa maendeleo ya taifa letu, katiba ni dira muhimu sana kizazi na kizazi.
   
 5. Ibra Mo

  Ibra Mo JF-Expert Member

  #5
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 795
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Siamini kama kubaki kwao wanamaanisha kuunga mkono huo muswaada hasa Machali,bado nina imani na Machali na inawezekana kabisa kubaki kwake anatafuta nafasi yakuchangia nakutoa dukuduka lake kwakupinga huo muswaada wa ovyo kisha aungane na Makamanda.
   
 6. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #6
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Hapo sasa....
   
 7. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #7
  Nov 14, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mbona tunapenda kulalamika kama mazezeta?..... NANI ATEUE/CHAGUE TUME YA KUKUSANYA MAONI?
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  Nov 14, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Tatizo lako hausomi maoni ya wadau wengi umeishi kuandika masimulizi ya hao ccm uchwara kwamba watu wanalalamika tu. Kila kinachokosolewa wazo mbadala linatolewa. Tatufa uzi wenye hotuba ya Lissu leo bungeni usome (kama utaacha uvivu wa kusoma)
   
 9. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #9
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Mh! Kaazi kwelikweli...
   
 10. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #10
  Nov 14, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,785
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Kwa mbunge kijana Machalii nadhani tatizo ni kumsikiliza Mbatia,kwa upande wa Agripina Buyogela sidhani kama hata anaelewa nini maana ya Katiba Mpya. Kwa akina Mrema na Cheyo hawa kila mtu anaelewa matatizo yao. Wanakula wamekwisha kabisa.

  Wabunge ambao nashindwa kuwaelewa kabisa ni CUF ambao ningetarajia baada ya aibu ya Igunga wajipange upya na hasa wale wanaotoka huku bara,wameshindwa tena kusoma watanzania wanataka nini. CUF inazidi jichimbia ktk kaburi la kisiasa,na CCM haitakua na huruma kuwafukia siku itakapotimia!
   
 11. April

  April Member

  #11
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Naungana mkono na wadau, jamani wapinzani baadhi wameshanunuliwa na MAGAMBA tukaeni macho, itakapobidi kuingia barabarani na tuwe tayari maana hilo BUNGE LA KATIBA litakaloenda kuundwa na Rais sina imani nalo hata chembe.
  Uchaguzi wa Tume urudishwe kwa wananchi upitishwe na wabunge kwa namna ambayo Kafulila amependekeza.
   
 12. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #12
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  CUF watoke ndoa yao ivunjike? Wanaogopa kuachika!
  Umesema vizuri kuhusu Machali, watu huku JF walikuwa hawamuelewi vizuri.
  Agripina, Mrema na Cheyo sina cha kuongeza.
   
 13. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #13
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Dharau nayo ni dhambi
   
 14. j

  jigoku JF-Expert Member

  #14
  Nov 14, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hivi watanzania bado kweli mna imani na raisi ambaye amepindisha sheria za nchi mara nyingi tu?rejeeni suala la ufisadi wa EPA,Rada,Kiwira,Richmond,na mengine mengi,na kwa reference ya ufisadi uliokwisha tendeka nchini na yeye raisi kushindwa kushughulikia kwa lengo la kuwalinda hao mnadhani kuna haki na ukweli katika madaraka yote anayotarajiwa kupewa raisi.acheni kuongopeana kuna tatizo kubwa hapa.
   
 15. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #15
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,924
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Nshachoka kusoma sihasa...ngoja nkalale
   
 16. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #16
  Nov 14, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hakuna wazo mbadala lililotolewa, ukisema kwamba unapendekeza vyama vya siasa, wasomi na NGOs, bado hujasema specifically how you gonna get intellectuals, who is to appoint those intellectuals, and how?

  Je, 83% ya hiyo kamati itaundwa na wabunge wa CCM?, how many intellectuals and NGOs, religious lewaders? in what proportion?
  Hiyo hotuba aielezi chochote kuhusu composition in terms of proportionality..... in short is just a complaint rather than an alternative solution.

  Usituletee ushabiki hapa!
   
 17. a

  anold Tumaini Member

  #17
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unaelewa maana ya mapendekezo?
   
 18. h

  hmzuyu Member

  #18
  Nov 15, 2011
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yah ni complaint na ndio maana tunasema ilibidi usomwe kwa mara ya kwanza ili ammbo kama hayo ya propotionalitity yajadiliwe ikiwa pamoja na sifa an kila kilichokosolewa.kwanza utambue kosa hiyo ni moja ya utatuzi wa tatizo,then njoo mezani tutafute alternative.
  Sasa watu ahta tatizo hamlioni,mtalitatuaje????
   
 19. Mpatanishi

  Mpatanishi JF-Expert Member

  #19
  Nov 15, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  hata mm nakumbali Machali hyseee najua tu hakutaka kutoka mana hataki kuonekana ana msimamo sawa na Kafulila. Tungoje atakapochangia tutajua.
   
 20. S

  Singili Member

  #20
  Nov 15, 2011
  Joined: Oct 3, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ingekuwa vizuri iwapo sentensi ya mwisho ungeandika -WANAMAGWANDA NAOMBA KUWASILISHA!-
   
Loading...