Hoja ya Tundu Lissu yaigawa NCCR bungeni

Chadema kwa usanii wanatoka bungeni halafu baadae wanapita kuchukuwa posho!
 
ndugu yangu soby sijui una uelewa gani!kumbe wewe hata hujaelewa wanachokifanya kambi ya upinzani!hujui hata nani na muundo upi wa tume unatakiwa???mmhh vijana tushirikiane kuelimisha uma juu ya hili!
 
Ni jambo la kumshukuru Mungu kama wanafki wote watafahamika mapema wasije wakatupoteza mbele ya safari.
 
Kwa mbunge kijana Machalii nadhani tatizo ni kumsikiliza Mbatia,kwa upande wa Agripina Buyogela sidhani kama hata anaelewa nini maana ya Katiba Mpya. Kwa akina Mrema na Cheyo hawa kila mtu anaelewa matatizo yao. Wanakula wamekwisha kabisa. Wabunge ambao nashindwa kuwaelewa kabisa ni CUF ambao ningetarajia baada ya aibu ya Igunga wajipange upya na hasa wale wanaotoka huku bara,wameshindwa tena kusoma watanzania wanataka nini. CUF inazidi jichimbia ktk kaburi la kisiasa,na CCM haitakua na huruma kuwafukia siku itakapotimia!
<br><br>tatizo la nchi hii ni matumbo,viongozi wetu wana njaa sana!2015 ndio mwisho wa wanafiki wote!
 
hata mm nakumbali Machali hyseee najua tu hakutaka kutoka mana hataki kuonekana ana msimamo sawa na Kafulila. Tungoje atakapochangia tutajua.



Acha unafiki waliotoka hawakutoka kwa sababu ya Kafulila katoka nje, wapambanaji wa ukweli walitoka nje kufikisha ujumbe kua hawakubaliani na kusomwa kwa muswada kwa mara ya pili na mapungufu mengine makubwa ya muswada huo na hao ndo waliotumwa na wananchi(na hayo ndiyo maoni ya wanachi). Waliobaki wote wanafiki wanaongozwa na matumbo yao. Machali hawezi kuwa na msimamo tofauti na wa Mbatia na Mbatia siku zote amekua anapingana waziwazi na wapambanaji wetu kwa hiyo usitegemee mabadiliko yeyote kutoka kwa huyu bwana.
 
Tatizo wana magamba wanadhani wanatukomoa lakini siku zote haki inachereweshwa haiwezi kuzimwa tutashinda tu
 
Tatizo lako hausomi maoni ya wadau wengi umeishi kuandika masimulizi ya hao ccm uchwara kwamba watu wanalalamika tu. Kila kinachokosolewa wazo mbadala linatolewa. Tatufa uzi wenye hotuba ya Lissu leo bungeni usome (kama utaacha uvivu wa kusoma)

Hawezi soma nondo kama ILE!
 
Hapo kwenye nyekundu... It's ethical but impractical, kwa mfano tu hebu nieleze jinsi kundi mojawapo linavyoweza kuchagua mwakilishi wake, just tell me the process. Tuseme wawakilishi kutoka kundi la dini, hebu chakachua jinsi watakavyopata wawakilishi wao.... je, how many? or in what proportion hao wadini watawakilishwa compared to let say Political parties?, Na ni nani atawachagua?, waumini au Mkuu wa kambi ya upinzani?

mkuu sasa hii ndio hoja ya kukaa chini na kufanya research ni jinsi gani tutapata wawakiliski katika mfuu huu unaopendekezwa na wengi,lakini si kwa kutumia ule feki wa mheshimiwa kuteua wana ccm wenzake. kwenye kundi la dini unaweza kutumia dini zote ambazo zimesajiliwa nchini na pengine kwa ratio ya waumini wake kwa kukadilia(kwakuwa baba wa taifa alikataa swali la dini kwenye sensa), Vivyo hivyo kwa vyama vya siasa vyenye uwakilishi bungeni kwa ratio ya uwakilishi wao. NGO unaweza kutumia idadi sawa kwa active ones.
i stand to be corrected.
 
fwafwanua hapo yaani tupige kura kuchagua tume au? halafu katiba iandikwe lini? we have only four years remaining!! halafu kazi ya bunge ni hiyo?

kwa maoni yangu tayari ni viongozi karibu kila taasisi na wana umoja wao isipokuwa wananchi majority.

kuipata tume, tufuate mfumo ufuatao
1. Wabunge, kila chama kipendekeze wabunge idadi ya wabunge itakayokubaliwa labda tuseme 5. kutoka kila chama ambapo idadi italingana na watachaguliwa wanaoaminika kuwa na uwezo wa kutetea maslahi ya chama husika.
2. Wanaharakati wote, kupitia NGOS, CBOS na makundi mengine, nao wachaguane wao wenyewe ili kuleta wajumbe katika bunge la katiba. Idadi ya wachaguliwa iwe sawa kwa makundi yote.
3. viongozi wa dini nao wachaguane wao wenyewe idadi iwe sawa kabisa.
4. makundi maalumu nao wachaguane wao kwa wao idadi iwe sawa kwa makundi yote.
5. kwa wananchi, kuwapata wajumbe, tunaweza kutumia kila tarafa/jimbo kuwapata wawakilishi ambao tutawachagua kwa kura za maoni.

kufanya hivi, kila kundi litahakikisha halimchagui mtu ZUZU, watako chaguliwa watakuwa wamejitangaza kuwa wanauwezo gani na watachaguliwa kwa sifa zao, halafu itkuwa vigumu kwa CCM kuwateka wote, kwani kikipanga kuwahujumu siri zitafichuka tu
 
mkuu sasa hii ndio hoja ya kukaa chini na kufanya research ni jinsi gani tutapata wawakiliski katika mfuu huu unaopendekezwa na wengi,lakini si kwa kutumia ule feki wa mheshimiwa kuteua wana ccm wenzake. kwenye kundi la dini unaweza kutumia dini zote ambazo zimesajiliwa nchini na pengine kwa ratio ya waumini wake kwa kukadilia(kwakuwa baba wa taifa alikataa swali la dini kwenye sensa), Vivyo hivyo kwa vyama vya siasa vyenye uwakilishi bungeni kwa ratio ya uwakilishi wao. NGO unaweza kutumia idadi sawa kwa active ones.
i stand to be corrected.

kwa ratio ya waumini/wbunge wake tutaharibu, inatakiwa kama idadi ni tano, basi iwe tano kwa dini/vyama vyote ili linapokuja suala la kuamua, isionekane dini/chama kimoja kiliwazidi wengine. Kuwapata itakuwa rahisi iwapo wana dini wenyewe wakiachiwa kuchagua. Mfano kila dini inawatambua watu ambao wakisimama lazima wanaongea kuashiria kuitaka katiba mpya, hivyo wandini naamini watamchangua huyo kuliko yule anayekataa
 
kama ilivyo kawaida upinzani kwa hapa tz unafahamika , na wabunge wa upinzani wanafahamika ikiwa ni pamoja na wanachuo wenye uchungu na nchi yao. Kafulila ni jembe mimi nalikubali tena saana na hiyo ndo iliofanya akakubal kutoka ili asijinajisi km wengine ambao walikua wameamua kubaki ndani ya bunge huku wakijua ya kua wanaongelea unafiki. mrema naon akikombe cha babu alichokunywa kimemtia MAPEPO, ndo maana akamuita spika mungu. huyu mhhhhhhhhhhhhhhhhhhh Mungu amrehemu
 
Tunaongea lugha moja ila tunaachana katikati ya mistari,
Nne, raisi atachagua makada wa chama kuanzia wajumbe mpaka wenyekiti na katibu,
Kuna pendekezo la jukwaa la katiba(refer katibaforum) ya kuwa kwenye huu mswada tuweke ni makundi yapi na kwa idadi ipi yanatakiwa kutoa wawakililishi alafu kila kundi kwa utaratibu wake watachagua wawakilishi kuanzia vyama vya siasa,kijamii,dini makundi ya watu wenye mahitaji maalum n.k
Hii ilikuwa njia sahihi na pia lissu katoa pendekezo la katibu aombe kazi na ajira yake itoLewe na tume sio raisi,pia wajumbe wa tume walindwe na sheria kama majaji,kuna mengi ila soma na uelewe maoni ya lissu yanasema karibia kila kitu tunachohitaji.Ndio amana tunasema serikali ijumuishe maoni ya wadau mbalimbali sio wanasiasa tu,kifupi wasituandikie(ccm) katiba. Waache tuandike. Hiyo ahbari ya miaka kumi itakuuwa habari ay kugomea kona wakati penalt umekubali.

natafuta hayo mapendekezo ya Lisu, can you attcha the link kwenye uzi huu?
 
Wapinzani wabunge wa chadema na NCCR mageuzi wamefanya jambo jema. Na huu ni mwanzo wa kutafuta katiba mpya ya wananchi waacheni CCM Waendelee kutafuta katiba ya Nchi kwa maslahi ya CCM. Na naamini hata wakiipitisha haitadumu miaka kumi. Lazima tutapata katiba mppy a ya Taifa isiyo na mawaa ya KiCCM.
 
za mwizi arobaini,ss inajulikana dhahiri kwamba ni nani ameamua kuwatumikia watz kwa dhati.Hongera Kafulila na Shibuda kwani kufanya kosa si kosa ila kurudia kosa ndio kosa.
 
Back
Top Bottom