Hoja ya Mkonge kuimaliza CCM Tanga - Zitto na Mnyika watikisa Korogwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja ya Mkonge kuimaliza CCM Tanga - Zitto na Mnyika watikisa Korogwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nice 2, Feb 20, 2012.

 1. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Zitto, Mnyika watikisa Korogwe
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Monday, 20 February 2012 07:27
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Boniface Meena, Korogwe
  WABUNGE wa Chadema, Zitto Kabwe wa Kigoma Kaskazini na John Mnyika wa Ubungo, wametikisa wilayani Korogwe baada ya wananchi kuwataka wawe mstari wa mbele kupigania hasa zao la mkonge, ambalo wabunge wao wanalisaliti.

  Pia, wananchi hao walimtaka Zitto kuhakikisha anarudisha hoja binafsi ya kutaka zao la mkonge liwe zao la mwaka 2012 kwa sababu mbunge wao, Yusuf Nassir, amewasaliti kwa kushawishi Spika wa Bunge kuzuia hoja hiyo.

  Wakizungumza kwa hasira mbele ya wabunge hao wa mkutano wa hadhara, wananchi hao waliwataka wawe watetezi wao kutokana na unyanyasaji wanaopata kutoka kwa wabunge wa CCM.

  Walimshtaki mbunge wao kwa Zitto wakitaka akamshughulikie ipasavyo kwa kuwa, anawasaliti wananchi wa Korogwe kwa kushindwa kutetea mkonge huku akijua ndiyo kazi yao kubwa.

  Katibu wa Wakulima Wadogo wa Shamba la Mwelya/Usambara, Ernest Mbezi, aliwaeleza Zitto na Mnyika kuwa wanashangaa mbunge wao na wengine wa Tanga kushindwa kuwatetea katika zao la mkonge.

  Akijibu hoja hizo, Zitto alisema atahakikisha anawasaidia wananchi hao kutetea hoja zao ili waweze kunufaika na mkonge, ambao ni zao linalowasaidia kwa maendeleo.

  “Tunataka kila mkulima amiliki shamba lake la mkonge na aweze kufaidika na kilimo cha zao hilo, ili maendeleo na uchumi wa Tanga uweze kukua,” alisema Zitto.

  Kabla ya mkutano huo, wabunge hawa walitembelea shamba la mkonge Mwalya/Usambara kujionea jinsi kilimo hicho kinavyofanyika na baadhi ya wakulima walisema kama wasipopigania zao hilo uchumi waoutaendelea kudidimia.

  Kwa upande wake, Mnyika alisema Serikali ya CCM na wabunge wake wamekuwa wakiwadanganya wananchi kuhusu mambo mbalimbali, ikiwamo suala la zao la mkonge ambalo linahitaji kusaidiwa.

  Mnyika alisema hali ya Serikali ya CCM sasa ni mbaya, imefanya uchumi wa nchi kuyumba kitendo ambacho kinafanya maisha ya wananchi kudidimia.

  Updates kutoka ukurasa wa Twitter wa Mh. Zitto 21/2/2012 - Ziara ya Tanga

  Jana tumemaliza Muheza.Tumekwenda kata ya Zirai-ambapo shule yao ya kata kati ya wahitimu 63 (form4),61 wamepata sifuri na wawili darajala 4.
  Tumehutubia Muheza mjini.Ujumbe wetu jana ni 'ukosefu wa ajira na ufisadi waweza kuangamiza Taifa iwapo hatua hazitochukuliwa.
  Sisi tunaelekeza nguvu kuisukuma Serikali kuweka fursa za uwekezaji kwenye Kilimo na viwanda vya Kilimo(uchumi wa vijijini) ili kukuza Ajira.
  Katika kupiga vita ufisadi, tutaendelea kuibua kashfa za ubadhirifu wa Mali za umma Kama njia ya kuzuia (deterrent).
  #ZiarayaTanga

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Mbwiga_Plus

  Mbwiga_Plus Senior Member

  #2
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WAlimchagua wa nini mtu anayewadidimiza?
   
 3. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Safi sanaaaaaaaaa!!!!

  Makamanda hakuna kulalaaaaaaaa!!!!
  Huu msako ni chumba hadi chumba.

  Hakuna kulala hata lepe ya usingizi!
  2015 nafikiri magamba watajisalimisha wenyewe Nchi

  Hawana adabu hata chembe,wanajaza matumbo yao tu!
  Mwisho wao waja!

  Pamoja Makamanda!


  Viva Chama cha Demokrasia na Maendeleo na chama makini kwa Watanzania!
   
 4. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hivi watu wa Tanga wanajua tofauti kati ya siasa na dini?
   
 5. d

  davidie JF-Expert Member

  #5
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 329
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe unajua tofauti kati ya ukweli na unafki?
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Feb 20, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,519
  Likes Received: 19,944
  Trophy Points: 280
  kila mwaka wanaipigia ccm kura hawa
   
 7. Prishaz

  Prishaz JF-Expert Member

  #7
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,939
  Likes Received: 1,476
  Trophy Points: 280
  iko siku kitaeleweka tuu! Hakuna barabara isiyokuwa na mwisho Ivuga
   
 8. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #8
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Zitto alivamia ajenda ya Wabunge wa Majimbo ya Korogwe, kwa vyovyote vile alitegemea wangempinga. Angetaka afanikishe ajenda yake, ambayo kimsingi ni nzuri, angewahusisha wenzake wenye dhamana na majimbo hayo. Tatizo lilikuwa ni njia na wala siyo malengo (kama kweli alikuwa nayo, na kama alikuwa na nia ya kizalendo ya kutaka mafanikio kwenye hili). Kama alikuwa anafanya siasa, kama inavyojidhihirisha sasa, matokeo ndiyo hayo - kukumbana na upinzani na ushindani mkali!

  Mimi binafsi nimejifunza: Hoja yangu binafsi ya uchimbaji dhahabu Nzega nliyoiwasilisha kwenye zaidi ya mikutano 5 ya Bunge haijawahi kupatiwa nafasi kwa visingizio visivyo na maana kwa vile tu ni ya kipambanaji na mimi niliifanya ni yangu binafsi, sasa nimeamua kuunganisha wadau wengi zaidi ili tushirikiane kuiweka sawa na kuiwasilisha tena. Na sasa nimeamua kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusiana na ajenda ya 'ajira kwa vijana' lakini nitawashirikisha wabunge wenzangu vijana kabla ya kufanya hivyo ili tufanikishe upatikanaji wa ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili...
   
 9. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #9
  Feb 20, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mkuu Hkigwangala wewe ni mpambanaji lakini huko ulipo hakukufai.
   
 10. M

  Molemo JF-Expert Member

  #10
  Feb 20, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hongereni makamanda wa CDM kwa kuivuruga ccm Korogwe
   
 11. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #11
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hao wabunge wa Korogwe walikua na hoja gani mkuu??
   
 12. Maruku Vanilla

  Maruku Vanilla Member

  #12
  Feb 20, 2012
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Vijana (Mnyika na Zitto),

  Poleni na kazi na heko kwa kazi nzuri ya kutetea rasilimali za wanyonge wa nchi hii.

  Natoa ombi maalumu; tafadhari sana mkimaliza ziara za "MKONGE" mtusaidie na sisi wakulima wa VANILLA. Tunao tuliowachagua kutuwakilisha lakini badala ya kutuwakilisha wanawakilisha ambao hawakuwatuma wala hawakuwa na haki ya kuwachagua. Tuko tayari kuwapa kila ushirikiano muweze kutufikishia kilio chetu panapohusika.

  Wakati mkoani kwetu zao la kahawa limekufa kwa kukosa watu makini wa kulitetea, Moshi na Arusha linazidi kuwa LULU. Sasa tumeamua kujidhatiti katika kilimo cha kibiashara katika zao la VANILLA lakini zaidi ya msaada wa watu binafsi wenye uchungu na mtu kama Mama Tibaijuka hatuna mtetezi mwingine.
   
 13. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #13
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Mheshimiwa tatizo la bunge letu ni kwamba linachanganya Siasa na Uhalisia wa mambo. Wanafikiri kuwa hizi ni enzi zile za "KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI......... ZIDUMU FIKRA SAHIHI ZA M/KITI WA CCM......"

  Inawabidi mnapokuwa bungeni muamke na siyo kulala usingizi, yawapasa kutetea Taifa letu. Angalia Uchumi wa nchi yetu unadolola kila siku lakini hakuna hatua zozote zinazochukuiwa, mfumko wabei unaongezeka siku hadi siku, hakuna hatua inayochukuliwa....

  Walalahoi tunaishi maisha ya shida sana ambao ndio sisi tuliowapeleka bungeni mkatuwakilishe lakini badala yake mmetusahau na kujitetea wenyewe kuwa mnaishi maisha magumu sana hivyo muongezewe posho. mnasahau kuwa kuna mtanzania ambaye anapokea Mshahara Tshs 80,000/= kwa mwezi (siku 31)

  kama wabunge wanaona ths 80,000/- haitoshi kwa siku moja je, huyu anayepokea kwasiku 31 anaishi vipi??????

  Kwa kweli Wabunge kwa hili hamtutendei haki kabisa wapiga kura wenu. Tunaomba mlitafakari kisha mchukue hatua


  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 14. mooduke

  mooduke JF-Expert Member

  #14
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 619
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Na wewe sijui Dr wa kitu gani sasa kwa Mbunge wa jimbo husika kuzuia hoja nzito ndio solutionn ya tatizo, kumbuka faida ipatikanayo na mkonge ni kwa taifa zima na sio Korogwe au Tanga peke kwa sasa ya ufinyu wa kufikiri na waliokuweka una-expose ujinga wako hapa barazani, Tanzania ya sasa sie ya zamani watu wanaweza kupambanua mambo. Ni chama chako ndicho kilicho tufikisha hapa tulipo, simamia maslahi ya taifa na sio ubinafsi Kigwangala acha siasa za kizushi.
   
 15. usininukuu

  usininukuu JF-Expert Member

  #15
  Feb 20, 2012
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siamini kuwa Mh. Zito alivamia ajenda kama ulivyoandika ila nadhani lengo lake lilikuwa ku-speedup process ambayo ilikuwepo. Kuhusu kulifanyia siasa sidhani kwani hata wananchi wanaonekana wangependa ajenda ile ijadiliwe mapema, hata hivo maamuzi ya bunge yalikuwa sahihi pia kwani ni vema ukafanyika kwanza upembuzi yakinifu kabla ya kutekeleza.
  Kuhusu suala la AJIRA KWA VIJANA naunganana na wewe kuwa hili ni suala la msingi ambalo linahitaji kuangaliwa kwa umakini kwani litakuja kulighalimu taifa, Haiingii akilini kuona tunaupungufu wa watumishi katika idara mbalimbali kwa mfano Idara ya Ardhi wanafunzi waliohitimu masomo yao mwaka 2009, 2010 na 2011 hawajapata ajira huku kukiwa na uhaba mkubwa wa watumishi ktk idara hiyo kwenye halmashauri nyingi Tanzania na kupelekea ujenzi holela na migogoro ya ardhi isiyoisha wakati watalamu wapo mtaani wanahangaika.
   
 16. Ericus Kimasha

  Ericus Kimasha Verified User

  #16
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 27, 2006
  Messages: 488
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 60
  HKigwangalla,

  Ajira kwa vijana ni suala nyeti sana. Na suluhu yake ni mtambuka hivyo lazima kila sekta ibainishe wazi mikakati yake jinsi ya kuzalisha na kuzilinda ajira kwa vijana. Iwapo utapenda kuwashirikisha watu wengi zaidi nje ya "Vijana Wabunge", basi nami nitakuwa tayari kukushirikisha nilichojifunza toka BEE Policy ya Afrika Kusini, jinsi ilivyoingizwa karibu katika kila sera ya uzalishaji na huduma za jamii, inavyotekelezwa na vyombo mbalimbali vya serikali na sekta binafsi na mafanikio na mapungufu yake. Naamini BEE Policy ina mengi ya kuchangia kuboresha hoja ya Ajira kwa Vijana.
   
 17. mooduke

  mooduke JF-Expert Member

  #17
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 619
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Piganieni nchi yenu wana wa nchi.
   
 18. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #18
  Feb 20, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
   
 19. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #19
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo lenu CCM kila kitu mnakifanya cha kisiasa! Kwa sababu ulizotoa ni kwamba wabunge wa Tanga walipinga kwa sababu za kisiasa!! wako tayari kuendelea kuwaumiza wananchi wa Tanga kwa masilahi yao ya kisiasa!!!! kweli akili ya mbayuwayu!!
   
 20. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #20
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Sioni namna BEE policy ya Africa Kusini inavyoweza ku-fit kwenye mazingira yetu, BEE inafaa Afrika Kusini kwa sababu za kihistoria! Tanzania hatuna siasa za Whites and Blacks! Kwa hiyo hatuhitaji "Black Economic Empowerment, BEE"
   
Loading...