Uchaguzi 2020 Hoja tatu ni kwanini wapinzani hawatoshi kwenye Uchaguzi huu

Amani Msumari

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
1,830
976
Wanajamvi,

Ninaomba nilete kwenu hoja tatu ni kwanini tusichague Upinzani. Hoja hizo ni Kama ifuatavyo:

1. Njia za kushughulikia janga la korona
2. Kushindwa kuwa mfano kwenye chama na majimbo
3. Kushindwa kuungana

Njia za kushughulikia janga la Corona

Wakati serikali ikija na mpango mkakati wa kushughulikia janga la korona, wapinzani nao walikuja na mpango wao. Serikali ilisisitiza kufuata masharti lakini watu walikuwa huru kufanya shughuli zao (there was no curfews). Kwa upande wao, wapinzani (hasa CHADEMA na ACT - Wazalendo), walisisitiza kufuata masharti lakini walitaka watu wafungiwe ndani (country lockdown).

Njia ya serikali ya CCM chini ya Rais Magufuli (akisaidiwa kwa Karibu na waziri Ummy Mwalimu) iliunganisha mambo mawili; ubunifu wa kisayansi uliozingatia mazingira yetu na kuweka imani kubwa kwa Mungu. Wapinzani walitaka kufanya "copying and pasting" pasipo kuzingatia mazingira yetu.

Unamfungiaje mtu ambaye mlo wake unategemea yeye kutoka? Watu si wangekufa njaa? CCM waliona hilo. Wananchi walipokea kwa furaha maamuzi ya Rais maana yalijaa matumaini, yalitoa Faraja na yalituvusha.

Rais Magufuli na serikali yake hawakulala. Walifanya majaribio, waliagiza NIMR na matabibu watafute suluhu. Mengi aliyoyafanya Rais Magufuli yalikuja kuthibitika baadae kuwa ni kweli na hakika ingawa wakati akiyasema alishambuliwa na maadui wa ndani na nje na kuitwa majina your mabaya.

Wakati Rais Magufuli na CCM wakichukua hatua hizo, wapinzani walikebehi, kubeza na kulaani. Walitutaka tusubiri kuokota maiti. Walienda mbali zaidi wakachukua posho halafu wakatokomea kusikojulikana, wenyewe wakiita "karantini ya kishua" huku wapiga kura wao wakihangaika kutafuta riziki zao.

CHADEMA walienda mbali zaidi kwa kutoa onyo Kali pamoja na kuwafukuza uanachama wabunge waliokataa mpango huo. Inashangaza wanajiita chama cha demokrasia.

Kwa hili tuu la ugonjwa wa Corona, ilitosha kabisa kuwakataa wapinzani na kuipa CCM kura zote.

Kushindwa kuwa mfano kwenye chama na majimbo

Ukipata nafasi unatakiwa uitumie vizuri. Wabunge wa Upinzani walitakiwa wajiongeze kwa kufanya kazi kwa bidii Sana, ubunifu wa hali ya juu na uadilifu usiotiliwa shaka. Vyama vyao vilitakiwa kuongozwa Kidemokrasia. Hii ingewasaidia sana kuwathibitishia watanzania kuwa hata wakipewa nchi wanaweza. Wanasema "Charity begins at home".

Kinyume chake, chamani na majimboni, ni "business as usual". Siku zote mchepuko unajitahidi kumfunika madhahausi. Wapinzani kwa hili mmeshindwa pakubwa. Mmeshindwa kuthibitisha kuwa mnaweza kuwa mbadala wa CCM. Endeleeni kujiandaa kwa sasa hamtoshi.

Kushindwa kuungana

Wapinzani kushindwa kuungana hasa mnapomkabili mgombea wa aina ya Rais Magufuli ni udhaifu mkubwa sana. Ni wazi kuwa hamuaminiani. Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe aliahidi ahadi hii hewa. Kama nyie binafsi hamuaminiani, sisi wananchi wa kawaida tutawaaminije?. CCM itawapiga kipigo cha mbwa koko mwaka huu. Hamna rangi mtaacha kuona.

Amani Msumari
Tanga
 
Taja "kiroja" kimoja tuu kwenye bandiko langu
Yaani unataka Jpm achaguliwe kisa
1.Corona
2.Upinzani haujaungana
3.Majimboni hakuna jipya

Hizi ni hoja au viroja?Yaani mtu apewe miaka 5 eti kwasababu hizo?Badala mumuulize sera ya viwanda imefia wapi?Vipi ajira mil 8 atafanya muujiza gani wakati ajira mil 1 hata 1% hakufikia kwa miaka mitano iliyopita!Aeleze kwanini mzunguko wa fedha umedorora na ana plan gani kuinua uchumi wa watu wake badala ya vitu vya kuonekana pekee?Muulizeni,hatma ya sekta ya kilimo ni nini maana ndiyo inayogusa wananchi wengi zaidi nchi hii huku ikiachwa nyuma kama sio kipaumbele cha serikali yake!
Hayo ndiyo mambo ya msingi tunataka kusikia mtu akieleza sio hizi cheap politics za Corona,sijui wapinzani hawajaungana,period!
 
Wakati tunajiandaa na Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020: Tanzania yaongoza Afrika usambazaji umeme Vijijini
 
Yaani unataka Jpm achaguliwe kisa
1.Corona
2.Upinzani haujaungana
3.Majimboni hakuna jipya

Hizi ni hoja au viroja?Yaani mtu apewe miaka 5 eti kwasababu hizo?Badala mumuulize sera ya viwanda imefia wapi?Vipi ajira mil 8 atafanya muujiza gani wakati ajira mil 1 hata 1% hakufikia kwa miaka mitano iliyopita!Aeleze kwanini mzunguko wa fedha umedorora na ana plan gani kuinua uchumi wa watu wake badala ya vitu vya kuonekana pekee?Muulizeni,hatma ya sekta ya kilimo ni nini maana ndiyo inayogusa wananchi wengi zaidi nchi hii huku ikiachwa nyuma kama sio kipaumbele cha serikali yake!
Hayo ndiyo mambo ya msingi tunataka kusikia mtu akieleza sio hizi cheap politics za Corona,sijui wapinzani hawajaungana,period!
Treni ya kwanza ya mizigo yafika Arusha baada ya miaka 30
 
Je, ni kweli flyovers na ndege zetu hazina msaada wowote kwa mwananchi anayeishi Nanyamba au Kyabakari?
 
Wanajamvi,

Ninaomba nilete kwenu hoja tatu ni kwanini tusichague Upinzani. Hoja hizo ni Kama ifuatavyo:
1. Njia za kushughulikia janga la korona
2. Kushindwa kuwa mfano kwenye chama na majimbo
3. Kushindwa kuungana

Njia za kushughulikia janga la korona

Wakati serikali ikija na mpango mkakati wa kushughulikia janga la korona, wapinzani nao walikuja na mpango wao. Serikali ilisisitiza kufuata masharti lakini watu walikuwa huru kufanya shughuli zao (there was no curfews). Kwa upande wao, wapinzani (hasa CHADEMA na ACT - Wazalendo), walisisitiza kufuata masharti lakini walitaka watu wafungiwe ndani (country lockdown).

Njia ya serikali ya CCM chini ya Rais Magufuli (akisaidiwa kwa Karibu na waziri Ummy Mwalimu) iliunganisha mambo mawili; ubunifu wa kisayansi uliozingatia mazingira yetu na kuweka imani kubwa kwa Mungu. Wapinzani walitaka kufanya "copying and pasting" pasipo kuzingatia mazingira yetu.

Unamfungiaje mtu ambaye mlo wake unategemea yeye kutoka? Watu si wangekufa njaa? CCM waliona hilo. Wananchi walipokea kwa furaha maamuzi ya Rais maana yalijaa matumaini, yalitoa Faraja na yalituvusha.

Rais Magufuli na serikali yake hawakulala. Walifanya majaribio, waliagiza NIMR na matabibu watafute suluhu. Mengi aliyoyafanya Rais Magufuli yalikuja kuthibitika baadae kuwa ni kweli na hakika ingawa wakati akiyasema alishambuliwa na maadui wa ndani na nje na kuitwa majina your mabaya.

Wakati Rais Magufuli na CCM wakichukua hatua hizo, wapinzani walikebehi, kubeza na kulaani. Walitutaka tusubiri kuokota maiti. Walienda mbali zaidi wakachukua posho halafu wakatokomea kusikojulikana, wenyewe wakiita "karantini ya kishua" huku wapiga kura wao wakihangaika kutafuta riziki zao.

CHADEMA walienda mbali zaidi kwa kutoa onyo Kali pamoja na kuwafukuza uanachama wabunge waliokataa mpango huo. Inashangaza wanajiita chama cha demokrasia.

Kwa hili tuu la ugonjwa wa korona, ilitosha kabisa kuwakataa wapinzani na kuipa CCM kura zote.

Kushindwa kuwa mfano kwenye chama na majimbo

Ukipata nafasi unatakiwa uitumie vizuri. Wabunge wa Upinzani walitakiwa wajiongeze kwa kufanya kazi kwa bidii Sana, ubunifu wa hali ya juu na uadilifu usiotiliwa shaka. Vyama vyao vilitakiwa kuongozwa Kidemokrasia. Hii ingewasaidia sana kuwathibitishia watanzania kuwa hata wakipewa nchi wanaweza. Wanasema "Charity begins at home".

Kinyume chake, chamani na majimboni, ni "business as usual". Siku zote mchepuko unajitahidi kumfunika madhahausi. Wapinzani kwa hili mmeshindwa pakubwa. Mmeshindwa kuthibitisha kuwa mnaweza kuwa mbadala wa CCM. Endeleeni kujiandaa kwa sasa hamtoshi.

Kushindwa kuungana

Wapinzani kushindwa kuungana hasa mnapomkabili mgombea wa aina ya Rais Magufuli ni udhaifu mkubwa sana. Ni wazi kuwa hamuaminiani. Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe aliahidi ahadi hii hewa. Kama nyie binafsi hamuaminiani, sisi wananchi wa kawaida tutawaaminije?. CCM itawapiga kipigo cha mbwa koko mwaka huu. Hamna rangi mtaacha kuona.

Amani Msumari
Tanga
Hoja zako zote hazina mashiko .Tueleze kwanini NEC imepokea mapingamizi 557, nasikia yamefika hadi 1000 mapingamizi yote hayana mashiko,tueleze pia kama unazijua sheria mpya za uchaguzi 2020 ambapo msajili wa vyama ndiye kiranja mkuu
 
Back
Top Bottom