PreGE2025 Hoja sita za ACT Wazalendo kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025, yataka Tume huru ya Uchaguzi iwe ya kweli

PreGE2025 Hoja sita za ACT Wazalendo kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025, yataka Tume huru ya Uchaguzi iwe ya kweli

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Chama cha ACT Wazalendo kimeainisha hoja sita muhimu ambazo kinasisitiza kuwa utekelezaji wake na Serikali pamoja na Tume ya Uchaguzi ni msingi wa kujenga mazingira ya kuaminiana kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Akizungumza katika Kongamano la Tatu la Operesheni Linda Demokrasia lililofanyika jana, Aprili 6, 2025, katika Jimbo la Kigoma Mjini, mkoani Kigoma, Makamu Mwenyekiti Bara wa ACT Wazalendo, Isihaka Mchinjita, alisema hoja hizo ni muhimu kwa kuimarisha misingi ya demokrasia nchini.

Kwa mujibu wa Mchinjita, baadhi ya masuala hayo hayahitaji mabadiliko ya kisheria, bali utekelezaji wa sheria zilizopo kwa ufanisi na kwa haki. Hoja hizo ni kama ifuatavyo

1. Tume Huru ya Uchaguzi Iwe ya Kweli

"Wajumbe wa sasa waondolewe, nafasi zitangazwe wazi, usaili ufanyike, na Watanzania wenye sifa wateuliwe kwa uwazi na kwa mujibu wa sheria."

2. Vyombo vya Dola Vikae Pembeni

"Jeshi la Polisi na Usalama wa Taifa visijihusishe tena na hujuma za uchaguzi kama ilivyojitokeza kwenye chaguzi za 2019, 2020 na 2024."

3. Wakurugenzi wa Halmashauri Wasiwe Wasimamizi

"Tume isimamishe uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri kuwa wasimamizi wa uchaguzi kutokana na uhusiano wao wa karibu na chama tawala."

4. Zuiwa Kura Feki – Uwazi Katika Mchakato

"Uzalishaji, usambazaji na udhibiti wa karatasi za kupigia kura ufanyike kwa uwazi na kwa ushirikiano wa wadau wote wa uchaguzi."

5. Mawakala wa Vyama Wapewe Uhuru

"Mawakala waruhusiwe kuwepo vituoni kikamilifu, wapatiwe nakala za matokeo na waondolewe tu kwa sababu halali na kwa mujibu wa sheria."

6. Hakuna Kuengua Wagombea kwa Makosa Madogo

"Tume iweke utaratibu wa kuruhusu marekebisho ya makosa ya kiuandishi badala ya kuwaengua wagombea – hasa wa upinzani."
 
Hizo hoja bila kuwalazimisha Watawala haziwezi tekelezwa kamwe.

Ndo mana tunasema NO REFORM NO ELECTION. Hii ndo lugha pekee wanayoelewa watawala wa nchi hii.
 
Punda haendi bila mijeledi. Huu si muda wa kubembelezana ...
 
Back
Top Bottom