HOJA MBADALA: Tuhamasishe CCM imsimamishe Membe 2015?

Watakuuliza, kwanini wewe kama mwana CCM unawapa hints CDM? ... watakwambia kuna jambo hapo!
 
Nianze kwa kukiri kuwa mimi siipendi CCM na ni mpinzani mkubwa wa yeyote yule anayejaribu kwa njia moja ama nyingine kulitetea hili genge la wezi kwa sababu yoyote ile. Pasco, labda mimi niko gizani lakini unapodai kuwa ndani ya CCM kuna "spotless names" unaniacha hoi kwa sababu kwangu naamini kwa dhati kuwa kule kuhusishwa na CCM ni doa tayari.

  • Hao "spotless names" wengine wao ni wajumbe katika vikao vya juu vya CCM vilivyokaa vikabariki na kupitisha maazimio ambao mengi yake yametufikisha hapa tulipo.
  • Hao "spotless names" wengine wao kwa kukaa kimya na kufumbia macho vitendo vya kifisadi kama wizi na hujuma, moja kwa moja wanakuwa "washiriki silent".
  • Hao "spotless names" kwa kuwa "washiriki silent" wanakuwa wamejiondolea kabisa sifa zozote zile za usafi na kwa kiwango fulani wanakuwa hatari kuliko hata hao wanaotetea wazi wazi vitendo hivyo.
Mimi, tofauti na Mwanakijiji, yeyote yule atakayesimamishwa na CCM kama ilivyo, hawezi kukwepa lawama anazopewa awe Kikwete, Mkapa, Lowassa, Sitta, Membe na wengineo. Adui mkubwa wa taifa ni CCM na kama tunataka kuendelea kujizika tukiwa hai, mwaka 2015 tuichague CCM na laana ya kuchagua hovyo itutafune kwani it's what we deserve!
 
Last edited by a moderator:

Mchambuzi: Maelezo yako yanaelimisha haswa!! hii ni kutokana na jinsi yalivyo objective. Suala la Mshindi ni Mshinindi ni jambo la kuangaliwa kwa undani ili Tanzania iweze kusimama katika utawala bora. Wananchi wapatiwe elimu ya uraia na maana ya matokeo ya upigaji kura. Kwa kufanya hivyo watakuwa na uelewa wa kuweza kuliingiza suala hili kwenye katiba mpya kwa lengo la kulifanyia marekebisho ya kudumu.
 
Kuna namna kwa sasa system imejiimarisha(ki-system siyo kisiasa). Na mgombea wanayemtaka(siyo anayetakiwa na siasa) ndiye atakayepita hata awe kiraza wa mwisho kabisa. Kuhusu kukubalika kwa wananchi, hilo siyo tatizo...system itahakikisha anakubalika na mtavaa fulana zake na kumpigia makofi. Na kura zitapigwa sawa...lakini system itazipa macho baada ya kupigwa ili zione kwa jicho la system.

Hizo nini nini 4C zitaongeza tu idadi ya wabunge hasa maeneo ambayo system itazidiwa nguvukazi lakini Urais...ni yule atakayewekwa na system.

Lengo ni kuendeleza utawala wa JK 'POST 2015' ili asije kuvuna uhasama aliopandikiza mwenyewe. Ndiyo maana BMW mpaka NEC, wamo mashangazi, wajomba, minihouse n.k.

Na kwa mtaji huu, Membe ni 'the best candidate'.

 
Mwanakijiji bado una imani na CCM? Kweli u mvumilivu na bila shaka utakula mbivu!!! Day in day out the same old story of theMAGAMBAS who pretend to be impeccable. Historia imeonyesha kila MAGAMBA achukuae madaraka ya Urais baada ya Baba wa Taifa anakuja na vituko vya kuudhi kuliko mwingine. Sisi wengine si wavumilivu sana tunataka mabadiliko potelea pote hata kama ni mbichi zitaiva tu maradi ziwe zimekomaa.
 

Au Dr. Asha Rose Migiro aliyestaafu UN.
 
Membe alivyo handle mambo ya Libya na Arab spring kwa ujumla, kauli zake ktk media Naye hafai.Kwani kama ni Kashfa tayari kumtetea Ghaddafi kipindi waLibya wakifa, kumtetea hadi kumfanya awe Mwenyekiti wa AU.Baadaye kujulikana kuwa hela ya Libya ilitumika sana kuwafanya viongozi wetu kuwa wapambe wa Ghaddafi.Atakuweje rais wetu huyu katk dunia inayohitaji umahiri na ujasiri katk kila maamuzi,ataishia kuwapa amri watu wa ndani kwa nguvu zote .Amri zilizotoka kwa watawala wa nchi nyingine.
 
Watakuuliza, kwanini wewe kama mwana CCM unawapa hints CDM? ... watakwambia kuna jambo hapo!

Na kuna jambo kweli..CDM imefika hapo bila ushauri wa mwana CCM leo iweje CCM wajidai kutoa ushauri kwa CDM na si kwa NCCR,ADP na wengine?Yupo Jirani yangu kila siku ni mshauri wangu ila juhudi zake za kuniangusha kila mtu anaziona.Baada ya kutoka hatua chache.
 
Watakuuliza, kwanini wewe kama mwana CCM unawapa hints CDM? ... watakwambia kuna jambo hapo!

Natoa hints za kuboresha demokrasia chini ya Dhana ya Tanzania Kwanza, Siasa baadae; Isitoshe, nionavyo mimi, katika siasa, hakuna kitu chenye kuleta faraja moyoni zaidi ya ufahamu kwamba umeshinda kihalali, umeshinda ndani ya mazingira yanayo heshimu sheria, umeshinda huku ukiwa unaheshimu haki za raia, na umeshinda bila ya kuitia doa demokrasia; Nitaiunga mkono CCM yenye mtazamo wa namna hii, vinginevyo iwapo Mwasisi wa CCM (Nyerere) aliwahi sema CCM sio mama yake, na anaweza kuachana nayo wakati wowote, kwa mtu mdogo kama mimi, nipo tayari kujiunga na chama chochote kinachokidhi hayo juu, Chadema ikiwa kimoja wapo, au CCM itakayojirekebisha kabla ya 2015;
 
Hypothetical question: akisimama Zitto na Edward Lowassa utampa kura nani?
Mind you, wewe bado upo CCM>
 
Ila mimi kama jirani yako na unaniuliza kama ukileta wi-Fi litakuwa jambo la maana, mimi nitasema poa tu!
Kwa sababu najua nitaibeep.
 

Mzee Mwanakijiji,
Umeshafanya mahojiano na mtu wako?
Amekwambia, amekuomba umpigie chapuo?

Kwa wale wanaofatilia mada zako za muungano wataelewa sera ipi ya muungano unaisimamia. Serikali moja.
Kutoka serikali mbili kuelekea moja.

Natumai umeanza kufunguka. Je utampatia kura yako Membe atakapochaguliwa kuwa mgombea wa chama unachokipigia debe?

Kuna thread ya zamani alianzisha, yaya au yoyo kuhusu wewe, bado naikumbuka vyema.

Hawa ndio wanaharakati wetu wa JF, wanatuhamasisha tutoe maoni ya kudai serikali moja na leo wanatwambia Membe atashinda uchaguzi mkuu 2015, CCM itashinda.

Nashindwa hata kushangaa.
 
Mwanakijiji
Kuna wakati unakuwa na busara lakini ukishapita pale mtaa Togo kidogo unapoteza mwelekeo; kwa mimi mwanaccm huru nisiye na kundi nitamuunga mkono mgembea wa uraisi ambaye atatea msalahi ya watanzania. wapo wanasiasa hawa wa mtandao ambao ndiyo walioifkisha nchii hapa tulipo wanautaka uraisi sijui kwa kutetea watanzania au matumbo yao. Mimi ni mpiga kura huru kura yangu si kuchezea kama CCM itasimamisha mwanasiasa wa mtandao; basi hata Sugu kama atasimamishwa na Chadema kugombea nitampa kura yangu; nisingependa kuona nimechangia kurudisha nyuma maendeleo ya Tanzania; naamini wapo wanasiasa wengi ndani CCM ambao ni safi na wana nia njema kwa watanzania.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Ni Tanzania pekee ambapo fisadi anapendwa. Kweli Tanzania tunakosa option za viongozi mpaka watu wanamfagilia Lowassa kisa anathubutu! Kuthubutu kwa kutuuza! Kama Rais atatoka CCM, kwa wanaotajwa basi ningeomba awe Membe. Nakuunga mkono Mzee Mwanakijiji!
 
tatizo wana cdm wenzangu sio wavumilivu mnataka kujadili ya kwenu tu yakiwekwa ya ccm tlp na cuf mnaanza dharau kwa hali hii 2015 kila mtu atakuwa raisi
 

Mkuu Mwanakijiji ni mtunzi wa riwaya jaribu kutuliza kichwa utamuelewa; Mwanakijiji na Pasco wanachopigania ni CCM kusimamisha mgombea dhaifu ili ishindwe; hiyo ni moja ya mbinu wanayoipigania ili Chadema ishinde; hili neno mgombea wangu linatumiwa sana na kamanda Pasco si kwa manufaa yetu CCM bali Chadema; hata anachokisema Mwanakijiji haamishi anaitakia CCM mema ni riwaya kamanda funguka!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Changuzi zilizopita je zilikidhi hivi vigezo ulivyojiekea? Au vigezo hivi utaanza kuvitumia 2015?

Unataka kusema kuwa hujui kuwa CCM inabebwa na tume ya uchaguzi, vyombo vya usalama na polisi ili ishinde kwa "kishindo"?

Kwa nini usubiri 2015 wakati leo unaona CCM inatumia "habari za kiintelijensia"/polisi kuzuia mikutano na maandamano ya vyama vya upinzani na anaepata kisago hasa ni CHADEMA? Hulioni hili?Umelala au umefumba macho?

Hivi kweli unategemea au una imani kuwa CCM itajirekebisha kabla ya 2015? Jamani, watanzania kiboko kwa porojo!!!
 
Hivi ni kweli bado watu wazima wanajadili kupata rais bora ndani ya CCM?
Mimi nilidhani tunapigana kuondoa mfumo na mapandikizi yake, kumbe tunatafuta mwenye afadhali...
 
Hypothetical question: akisimama Zitto na Edward Lowassa utampa kura nani?
Mind you, wewe bado upo CCM>

Naweza kumuunga mkono Lowassa lakini nisiende kupiga kura, au naweza kwenda kumpigia kura Zitto lakini nisimuunge mkono;
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…