Hoja binafsi: Nawapa changamoto BAVICHA, muda wa kuiua CCM ni huu chukueni hatua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja binafsi: Nawapa changamoto BAVICHA, muda wa kuiua CCM ni huu chukueni hatua

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Albedo, Mar 23, 2011.

 1. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni Chama Kilichofanikiwa kwa kiasi kikubwa kujipambanua kama Chama kinachopigania Maslahi ya Uma, na Kwa Bahati nzuri Kimeeleweka hivyo machoni mwa uma, na ikumbukwe namna Nguvu ya Uma ilivyofanikisha kwa Wabunge zaidi ya Ishirini (2) wa CHADEMA katika Uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwaka 2010. Ni Chama ambacho kimeonekana kujizolea Uungwaji Mkono Mkubwa katika Kada Mbali Mbali, Kuanzia Watoto wa Shule za Msingi mpaka wazee!
  Ni Chama ambacho kinazidi kukua ( Kwa maana ya Kuvutia zaidi Vijana) tofauti na CCM ambacho kinaelekea kufa kutokana na Kuchukiwa na Vijana wengi ( Chama kisipoungwa na mkono na Vijana Mwisho wake ni Kifo tu)
  Toka kuanzishwa kwake kimefanya Jitihada nyingi sana katika Kuhakikisha kinapata Wanachama wengi kila pembe ya Nchi. Mifano ya Kampeni ilizowahi kufanya ni pamoja na Operesheni Sangara ambayo kwa Kiasi Kikubwa Ilisaidia kukitambulisha chama hicho hata kuweza kuipa JambaJamba CCM katika uchaguzi uliopita!

  Je Wakati wa CHADEMA kuiua CCM Umefika? Na kama Umefika Silaha gani CHADEMA iitumie? Majibu ni Rahisi sana
  1: Ndiyo Muda wa CHADEMA kuiadhibu na kuiua CCM umefika, CHADEMA wamepewa Fursa ya Buren a Wananchi na CCM yenyewe, CCM imejipeleka machinjioni na kuweka Kichwa chake kwenye Gogo la kuchinjia na CHADEMA wameshika shoka. Swali ni Je nani kwa Mtazamo wako asushe Shoka hilo kwenye Kisusio kiitwacho CCM?
  Naamini wanaopaswa kufanya Hivyo si Mbowe, si Slaa, Si Baregu wala si Arfi, Bali Wanaopaswa Kufanya Hivyo ni Jeshi la BAVICHA likiongozwa na Makamanda kama Halima Mdee, Zitto Kabwe, John Mnnyika, John Mrema, David Silinde, Godbless Lema, MsandoAlberto na Wengine.
  Nashauri CHADEMA Waanzishe “Operesheni Mavuno”, na Main Objective ya Operesheni hiyo iwe ni “Maziko ya CCM”. Waitangaze na Waikabaidhi kazi hiyo kwa BAVICHA. Naamini BAVICHA iliyo na Nguvu itaweza kuwavutia zaidi vijana Wengi Zaidi kujiunga na kuwa Wanachama wa CHADEMA
  Naomba CHADEMA wasiipoteze Fursa hii Adhimu Kabisa, CCM wanakaribia Kufa na Hawapaswi waachwe wafe Natural Death, wanapaswa kufa kifo cha Aibu, Kifo cha Kukataliwa. Kazi Hiyo BAVICHA wanaiweza wakabidhini.
   
 2. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Well said mkuu, Bavicha ichaguwe uongozi wenye vision ili wasije kuharibu taswira ya chama iliyojijengea na kuaminiwa na umma, mpaka sasa watu wanaipenda CHADEMA kutoka mioyoni mwao lakini sio kwa kupewa Tshirt na kanga au posho, na hapa Dar es salaam ndio mkoa unoongoza Tanzania kwa wajinga, kwahiyo inabidi ifanyike kazi ya ziada kwa sababu CCM bado mtandao ni mkubwa licha ya kutokupendwa lakini bado wana miradi ile ya kulaza magari na ndio inayowafanya ukifika uchaguzi wao wa ndani waanze kutoana roho. halafu mimi bahati mzuri uchaguzi uliopita nilishiriki vilivyo, bado organisation ya chama sio nzuri sana, maofisa wa kuzungukia maeneo wakati wauchaguzi kwa upande wa jimbo na kata yangu walifeli, pili hakukuwa na mtu alikyekuwa anapita kuchukuwa matokeo ya urais, wote tulikuwa tumeyatolea macho matokeo ya udiwani na ubunge, ili eneo ndilo CCM wanajuwa kulicheza vizuri kuliko eneo lingine lolote. nina mengi ya kueleza hapa lakini nitawachosha wasomaji. yangu machache ni hayo tu.
   
 3. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  BAVICHA Mungu awape nini tena? Gunia la Chawa?


   
 4. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Good CHADEMA, Jina Zuri cha Msingi mtekeleze

   
 5. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Penye RED nilitaka kuwapa changamoto. kama kizazi kipya ni vizuri wawe na mtazamo chanya wa kukifanya Chadema iwe na muundo na sura ya kitaifa na sio kama ilivo sasa ina sura na muundo wa kikanda, kikabila na kidini.

  Hiyo ni changamoto kubwa sana kwenu Baavicha.
   
 6. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye RED hiyo ndio sifa ya CCM mwenyekiti JK MZARAMO ( MAANA MODS WAMESHALIHUJUMU HILI JUKWAA UKIANDIKA ****** WAO WANAWEKA NYOTA NA SIO ULICHOANDIKA ) ni mwislamu na anatoka ukanda wa pwani, katibu mkuu ni Yusuf Makamba, ni Mwislamu na anatoka ukanda wa pwani, kwahiyo CCM ndio chama cha kikanda na kidini na sasa hivi mmempata na yule Mufti Simba aliyeishia darasa la saba.
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kigezo gani umetumia kusema dar ina wajinga wengi hapa Tanzania wakati tuna wabunge wawili na mmoja alichakachuliwa....tatizo la watu wengi dar misheshe mingi hata kufatilia vyombo vya habari wengine inakuwa shida maana mida hiyo huwwa kwenye vyombo vya usafiri ama wakilejea makwao au wakienda kibaruani....
   
 8. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kubali au kataa lakini ukweli upo pale pale.

  Chadema kimejikita zaidi na kina sura dhahiri kabisa ya Ukanda na Udini.

  Changamoto kwa hawa vijana hususan katika uchaguzi na mwelekeo wao waliangalie hilo
   
 9. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #9
  Mar 25, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  CCM ni chama cha KIISLAMU sasa hivi, katibu mwenezi ni mufti Shaaban bin Simba yule ambaye ameishia darasa la saba.
   
 10. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hata mgombea urais mwenza wa Dr Slaa alifikia hilo hilo darasa la saba.

  Pole sana
   
 11. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #11
  Mar 25, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Nasisitiza CCM ni chama cha Kiislamu na mufti Simba ni Darasa la saba PERIOD.
   
 12. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #12
  May 26, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kila le heri BAVICHA
   
Loading...