Hoja: Bei Ya Kutuma SMS Ipandishwe Sana!

PakaJimmy

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Messages
16,231
Likes
351
Points
180
PakaJimmy

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2009
16,231 351 180
Wanabodi,

Nasikiliza Redio One stereo, kipindi kinachoitwa Yaliyomo Yamo.

Kuna hoja inaendeshwa ikitaka ifanyike petition kwenye makampuni ya simu kupitia TCRA ili bei ya SMS ipandishwe sana ili kuwakomesha watu waliozua mitindo inayokera ya kutunga meseji za kila tukio linalotokea nchini ikiwa ni pamoja na kuzua vifo vya watu. Walitoa mfano kuwa kuna meseji zilizosambazwa jana kuwa MwanaBongo Flavor aliyezikwa jana amekutana na Kanumba na Mafisango...!

Aidha walisema kuna sms nyingi za matusi na mambo yasiyo ya kistaarabu zinazotungwa na kusambazwa kila kukicha, bila kujali umri wa mtumiwa, kisa ni bei poa ya utumaji.

Wamesema makampuni ya Mawasiliano yafute meseji za offer na kupansdisha sana bei ya sms, wakidai itawakomesha waharibifu hao wanaozua au kuamsha simanzi kwa waliofiwa.

Mdau,
Unaionaje hoja hiyo?...je ndiyo mwarobaini wa hizi meseji?
 
Kennedy

Kennedy

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2011
Messages
14,886
Likes
5,926
Points
280
Kennedy

Kennedy

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2011
14,886 5,926 280
Sio dawa japo ni ukweli msg nyingine si nzuri bora watumaji wenyewe wajirekebishe
 
MZIMU

MZIMU

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Messages
4,080
Likes
36
Points
145
MZIMU

MZIMU

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2011
4,080 36 145
Na mimi nadhani, hoja hiyo ni sawa na kusema kua kilimo cha ngano, miwa, na nafaka zote kipigwe marufuku kwa sababu watu hutengeneza pombe kwa kutumia mazao hayo. Unajua tatizo Watangazaji wengi wa Hivi viredio hua sio Wenye weledi ya kutosha kuhusu mambo ya maana na mambo yasio na maana. Hua inatokea kama bahati mbaya kufanikiwa kusikiliza vipindi vyao.
 
Vin Diesel

Vin Diesel

JF Gold Member
Joined
Mar 1, 2011
Messages
8,701
Likes
1,244
Points
280
Vin Diesel

Vin Diesel

JF Gold Member
Joined Mar 1, 2011
8,701 1,244 280
Kuna haja ya kupima akili za producer wa hicho kipindi.....kipindi kijacho ataleta mada kuwa ili kuondokana na ajali basi magari yote yapigwe marufuku watu watembee kwa miguu...
 
Emanuel Makofia

Emanuel Makofia

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2010
Messages
3,849
Likes
29
Points
145
Emanuel Makofia

Emanuel Makofia

JF-Expert Member
Joined Jan 5, 2010
3,849 29 145
nimesikiliza ila watangazaji wenyewe akili zao zinawatosha wenyewe hawakuwa na hoja
kisa kikubwa kuna sms zilisambazwa jana kuwa RAY C kafa badala ya kuhoji kwa nn mwanzishaji asitafutwe
kwa kuwa simu zimesajiliwa wanataka bei za sms zipandishwe............loh!
 
Mwana Mtoka Pabaya

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Messages
13,300
Likes
10,129
Points
280
Mwana Mtoka Pabaya

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2012
13,300 10,129 280
Mawazo mafu haya, hawa wakina mama wanadhani umbea na ufanyaji maamuzi vinaenda sambamba. SMS ziongezwe gharama eti kwa sababu Ray C kazushiwa kifo. Kwa maoni yao ya saluni, SMS zinatumika vibaya kwa hiyo gharama zipande.

Sasa swali langu kwa hawa kinamama: Ikiwa watu wanapofika Posta wanachafua mji kwa kutupa takataka, nauli za usafiri wa kwenda huko zipandishwe ili watu wasiende holela?
 
M

Mkeshaji

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2011
Messages
4,263
Likes
7
Points
0
M

Mkeshaji

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2011
4,263 7 0
Wanabodi,

Nasikiliza Redio One stereo, kipindi kinachoitwa Yaliyomo Yamo.

Kuna hoja inaendeshwa ikitaka ifanyike petition kwenye makampuni ya simu kupitia TCRA ili bei ya SMS ipandishwe sana ili kuwakomesha watu waliozua mitindo inayokera ya kutunga meseji za kila tukio linalotokea nchini ikiwa ni pamoja na kuzua vifo vya watu. Walitoa mfano kuwa kuna meseji zilizosambazwa jana kuwa MwanaBongo Flavor aliyezikwa jana amekutana na Kanumba na Mafisango...!

Aidha walisema kuna sms nyingi za matusi na mambo yasiyo ya kistaarabu zinazotungwa na kusambazwa kila kukicha, bila kujali umri wa mtumiwa, kisa ni bei poa ya utumaji.

Wamesema makampuni ya Mawasiliano yafute meseji za offer na kupansdisha sana bei ya sms, wakidai itawakomesha waharibifu hao wanaozua au kuamsha simanzi kwa waliofiwa.

Mdau,
Unaionaje hoja hiyo?...je ndiyo mwarobaini wa hizi meseji?
Hivi laini za simu zilisajiliwa ili iweje?
 
Matola

Matola

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2010
Messages
38,928
Likes
19,607
Points
280
Matola

Matola

JF-Expert Member
Joined Oct 18, 2010
38,928 19,607 280
This people they can't be serious, wakati watu tunapambana Gharama za simu zishushwe na sms ziwe bure kumbe kuna mabundi ambayo source of income zao ni kupewa pesa na mabwana wanatuletea mawazo ya Salon!! Pumbavu kabisa.

Redio one nayo imeshakuwa cheap this much kuendesha mijadala ya kijinga na ya hovyo kama huu!!?
 
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
42,580
Likes
38,995
Points
280
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
42,580 38,995 280
siku hizi kwa internet unaweza kutuma sms, pia kuna application kama whatsapp watu watahamia huko
Wanabodi,

Nasikiliza Redio One stereo, kipindi kinachoitwa Yaliyomo Yamo.

Kuna hoja inaendeshwa ikitaka ifanyike petition kwenye makampuni ya simu kupitia TCRA ili bei ya SMS ipandishwe sana ili kuwakomesha watu waliozua mitindo inayokera ya kutunga meseji za kila tukio linalotokea nchini ikiwa ni pamoja na kuzua vifo vya watu. Walitoa mfano kuwa kuna meseji zilizosambazwa jana kuwa MwanaBongo Flavor aliyezikwa jana amekutana na Kanumba na Mafisango...!

Aidha walisema kuna sms nyingi za matusi na mambo yasiyo ya kistaarabu zinazotungwa na kusambazwa kila kukicha, bila kujali umri wa mtumiwa, kisa ni bei poa ya utumaji.

Wamesema makampuni ya Mawasiliano yafute meseji za offer na kupansdisha sana bei ya sms, wakidai itawakomesha waharibifu hao wanaozua au kuamsha simanzi kwa waliofiwa.

Mdau,
Unaionaje hoja hiyo?...je ndiyo mwarobaini wa hizi meseji?
 
PakaJimmy

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Messages
16,231
Likes
351
Points
180
PakaJimmy

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2009
16,231 351 180
siku hizi kwa internet unaweza kutuma sms, pia kuna application kama whatsapp watu watahamia huko
Ingekuwa ni zamani ningesema Watanzania wenye access na Internet ni 4% tu.
Lakini sasa hivi mchina katusaidia, hata Tecno zinatembeza internet mbaya!
 
Rasib

Rasib

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Messages
395
Likes
4
Points
35
Age
32
Rasib

Rasib

JF-Expert Member
Joined Apr 23, 2012
395 4 35
This people they can't be serious, wakati watu tunapambana Gharama za simu zishushwe na sms ziwe bure kumbe kuna mabundi ambayo source of income zao ni kupewa pesa na mabwana wanatuletea mawazo ya Salon!! Pumbavu kabisa.

Redio one nayo imeshakuwa cheap this much kuendesha mijadala ya kijinga na ya hovyo kama huu!!?
good say, like it
 
Domy

Domy

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Messages
4,701
Likes
12
Points
135
Domy

Domy

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2011
4,701 12 135
Nafikiri hatua zichukuliwe kwa wale tu wanaojihusisha na hizo sms hasa muanzishaji kama vile kumpa onyo na akiendelea line ifungwe.ndio sababu ya kusajili namba
 
2hery

2hery

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2011
Messages
4,149
Likes
3,000
Points
280
2hery

2hery

JF-Expert Member
Joined May 27, 2011
4,149 3,000 280
wauaji wa Barlow si walikamatwa kupitia mitandao ya simu?
 
Nivea

Nivea

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2012
Messages
7,466
Likes
112
Points
160
Nivea

Nivea

JF-Expert Member
Joined May 21, 2012
7,466 112 160
'''jana nilipita plae geto kwako kumbe majambazi yalikuwa yamekuvamia,nikasikia yakikuamuru tukubake au tukuue,chagua moja fasta ,niliposikia hivo nikakimbia,kama unaisoma meseji hiikweli ulifanya maamuzi magumu''''

hii messeji nim,etumia na rafiki yangu this morning nilikasirika sana sana ,ni siku chache tu jirani yangu alivamiwa na house gal wake kubakwa nakuambukizwa ukimwi alafu mtu anakutumia sms kama hiyo kweli nimekasirika sana
 
Lily Flower

Lily Flower

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2009
Messages
2,555
Likes
10
Points
135
Lily Flower

Lily Flower

JF-Expert Member
Joined Oct 16, 2009
2,555 10 135
Sioni hoja hapo alietuma hiyo sms atafutwe apewe onyo kali na faini, ndio maana ya kusajili line.
 
Forum statistics

Threads 1,250,942
Members 481,523
Posts 29,751,684