Hofu ya mafisadi dhidi ya anti-virus movement............... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hofu ya mafisadi dhidi ya anti-virus movement...............

Discussion in 'Celebrities Forum' started by only83, Dec 11, 2011.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  HONGERA Watanzania wenzangu kwa sherehe za kutimiza miaka miaka 50 ya uhuru wetu zilizofikia tamati jana. Mungu azidi kutupa neema za mafanikio zaidi.

  Baada ya hapo, niweke wazi kuwa sina ugomvi na mtu au kundi la watu kwa haya nayotarajia kuyaweka wazi mbele yenu.Msingi wa hoja yangu ni kutoa tafsiri yenye lengo la kuweka mambo sawa katika mtazamo wa vuguvugu la kudai haki na uhuru wa kufanya sanaa ya muziki nchini.Nimebaini mambo kutokwenda vizuri kutokana na kweli kufichwa, lakini kupitia 'vuguvugu la kudai haki sawa na Uwanja huru wa kufanya sanaa', maarufu kwa jina la "Anti virus", naamini hii ni fursa ya kufungua milango ya uwazi na ukweli

  Anti virus ni mkusanyiko wa watu wenye taaluma na uwezo, ambao wanaamini sanaa ya muziki inaweza kuwasaidia vijana wengi.Sanaa ya muziki pia ikitumia vizuri, ni tija kwa taifa kwa vile itasaidia serikali kupata kodi itakayotumika kwa maendeleo ya nchi kwa jumla.

  Kinachodaiwa hapa ni haki na usawa katika sanaa na malipo sahihi kama wanavyolipwa wanamuziki wengine wakija nchini kufanya maonyesho.
  Unakuta wasanii wa nje wanakuja kufanya maonyesho na ndani ya masaa machache wanavuna mamilioni ya shilingi toka kwa watanzania, ambao wasanii wao wa ndani wanaishi maisha mabovu kupindukia.

  Sanaa na soka ni fursa pekee ya kumfanya mtoto wa masikini kujikomboa kupitia ajira binafsi.Ni kama soka nchini Brazil ilivyowanyanyua vijana wengi. Soma historia za wanasoka kama Ronaldo de Lima na Pele soka walivyofanikiwa kimaisha.

  Ukweli ni kwamba, 'Anti virus movement' ni vuguvugu la kutaka mageuzi lililoanzishwa na wasanii wa zamani wanaoamini sanaa ya muziki inakwenda kusikotarajiwa.Pamoja na uwapo wa Basata (Baraza la Sanaa Tanzania) na Cosata (Chama cha Haki miliki), bado vyombo hivyo vimeshindwa kuwaletea mafanikio wasanii.

  Katika hili, hoja kubwa ni kuundwa upya kwa vyombo ili na kuvipa nguvu vifanye kazi kwa ufanisi mkubwa na kuleta tija kwa wasanii.Hii ndio sababu ya 'Anti virus' na hakika kadiri muda unavyokwenda ndivyo Watanzani wanazidi kupanuka kiakilia na kimawazo.

  Joseph Mbilinyi, maarufu kama 'Sugu', ndiye msanii anayeweza kusimama mbele na kujiita 'Shujaa' katika muziki huu.Ana kiu ya kuona mabadiliko yanafikiwa na ameamua kuwashirikisha wengine wenye mawazo na mtazamo kama wake wa kudai mageuzi.

  Ikumbukwe, vuguvugu la kupinga unyonyaji dhidi ya wasanii haukuanza jana. Msanii wa Hip Hop, Solo Thang aliwahi kuingia katika mzozo na kituo kimoja cha redio nchini akidai haki ya wasanii.

  Kilichotokea ni kwamba, alipigwa vita iliyolenga kumpoteza kwenye sanaa ya muziki kwa sababu tu ya kuwa mbele kudai haki.
  Tujiulize tukiwa na ushahidi wa mifano ya kweli, ni wasanii wangapi nchini wanaishi maisha mazuri na kumiliki vitega uchumi vinavyowaingizia mapato?

  Majibu tunayo, lakini ukweli unabaki pale pale kuwa, wasanii wengi wa muziki nchini hawajafaidika kama ambavyo ingetarajiwa.
  Wengi wao wamekuwa wakipata umaarufu kupitia kutangazwa kwenye vyombo vya habari, redio, televisheni na magazeti, lakini kwa suala la tija hakuna wa kujivunia.Wale wanaoibuka na kupinga 'Anti Virus' waje na ushahidi wenye hoja za msingi badala ya kuendelea kushabikia propaganda za kitoto.

  Miaka hii watu wameamka, wanafahamu haki zao za msingi, wanatambua nini wanastahili na nini hawastahili.
  Huu si muda tena wa kuendelea kuwavumilia wanyonyaji wa kazi za wasanii. Mapambano yaliyoanza yatakuwa na mwisho mzuri.

  Mtu mwenye uelewa mdogo ndiye atakayeamini kuwa huu ni ugomvi kati ya makundi mawili, lakini ukweli ni kwamba hoja zimejengwa na majibu yakapatikana ambayo ni kudai haki na usawa katika sanaa.Hofu kubwa ya wanyonyaji wa kazi za wasanii hapa Bongo ni kwamba, hawataki mambo yawe wazi kwa vile watakosa fursa ya kuendeleza ufisadi wao dhidi ya wasanii.

  Kwa hofu hiyo, sasa tunawaona wakitumia muda mwingi na hata pesa pia kuwazima wale wote wanaofungua mdomo na kutaka kudai haki.Nguvu ya kudai mabadiliko inapoungwa mkono na wengi, hapatatokea nguvu nyingine ya kuzuia, ingawa kutakuwapo na wachache watasikikia wakipiga vijembe.

  Ieleweke, nguvu ya mabadiliko ya watu haipingwi kwa vijembe redioni wala maneno ya shombo, bali kwa hoja zenye msingi wa kueleweka.
  Sasa tunasonga mbele na kutaka kila msanii apate kipande chake halali na kuacha kutengenezewa wasanii na kikundi kimoja cha watu kwa maslahi yao.Nimalize kwa kusema, mimi ni mdau wa muziki kwa muda mrefu na naielewa sanaa hii kwa upana wake hasa hapa nyumbani.

  Msingi wa hoja yangu unabaki katika kutetea haki ya wasanii wanaolaliwa kimaslahi na watu wachache na hivyo kukwaza maendeleo ya fani hii.Sibahatishi, naongea nachokifahamu kwa ushahidi usiokuwa na chembe ya mapungufu ya kile kinachoendelea kwenye fani ya muziki nchini.

  Sasa ni wakati wa kufunga pingu unyonyaji dhidi ya wasanii wetu, kazi iliyoanza itamalizika vizuri na kutoa fursa kwa wasanii kuchekelea matunda ya kazi zao.

  SOURCE:Mwananchi
   
 2. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Eti anitivirus ni mkusanyiko wa watu wenye taaluma. He he he he he acha nijichekee mieeeeeeee.
   
 3. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #3
  Dec 11, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,993
  Likes Received: 1,002
  Trophy Points: 280
  Siku zote ninasemaga wewe ni "she" lakini watu hawaamini
   
 4. i

  issaramso New Member

  #4
  Dec 11, 2011
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Afadhali bana
   
Loading...